Ndoto hii imenichanganya sana

mogulnoise

JF-Expert Member
Oct 28, 2014
2,434
5,535
Wasalaam na poleni kwa msiba mzito wa taifa,Yes ni wa kitaifa sababu kila mtanzania mwenye siha njema ya akili huu ni msiba mzito.

Nianze na kusimulia ndoto niliyoota usiku wa kuamkia leo kwanza nikiri kabisa lugha ninazozitambua hata kwa kiwango kidogo ni Kiswahili kwa ufasihi, Kifaransa na Kingereza kwa taabu sana.
Sasa la kushangaza ndoto hii nimeota ni ya Kiarabu mimi kiarabu sikijuia labda ile salamu yetu tu
Ila ndoto yenyewe niliona ile meli iloyokuwa pale kigamboni baada ya kukamatwa kwa uvuvi haramu ikiongozana na kivuko cha bagamoyo Dar zikiwa zimeongozana kwa mwendo kasi huku kile kivuko cha bagamoyo Dar kikiwa mbali kwa spiidi ya ajabu.

Watu walikuwa wengi wanaulizana kwa lugha ya kiarabu ambayo maneno mengi sikuwa na yaelewa zaidi ya majina ya sehemu zinapokwenda nilisikia ukerewe ngara na mwanza kwa vile nilikuwa na shahuku ya kujua ilibidi niulize ulize watu waliokuwa pale

Ndipo mzee mmoja wa makamo alikuwa amevaa kibarakashee na bakora akaniita kwa kuashiria nisogee karibu yake kwa kutumia ile bakora yake. Huyu mzee alikuwa anafahamu kiswahili kwa kiasi akaniuliza unashida gani, nikamjibu nataka kujua mbona watu wengi hivi wanashangaa meli iyokamatwa kwa uvuvi haramu na kivuko cha bagamoyo -Dar je kuna jambo gani lakustaabisha?

Yule mzee akacheka akaniambia kijana hiyo meli na hicho kivuko vinaelekea ukerewe toka hapa bahari ya Hindi hadi ziwa Victoria

Kwa kweli sikumuelewa yule mzee hiyo meli na kivuko vitafikaje ziwa Victoria tena vikiendeshwa kwa kasi kuanzia Dar

Pia nikawa najiuliza hii meli tuliambiwa imeibiwa vitu hadi kupekekea kuwa chuma chakavu pale magogoni vile vile nikajiuliza na hiki kivuko sikilishatolewa kwa jeshi letu tukufu?

Kwa kweli ndoto hii imenivuruga ila kwa vile ni ndoto nimeona niiwasilishe hapa pengine nitapata tafsiri au kuna mtu aliyeota ndoto kama hii au ilipokata kwangu iliendelea kwake karibuni
 
Ungekuwa uliiota kabla ya ajali na ulileta hii thread kabla ya ajali basi ndoto yako ingekuwa na maana sahizi hii thread ingekuwa inatrend kama "kaburi lililofukuliwa" ila kinyume na hapo hakuna tofauti na tunaootaga ndoto za tuliyoyafanya jana.
 
Back
Top Bottom