Jambo usilolijua ni sawa na usiku wa kiza,inavyoonekana huwajui TFF weweeeeeeeeeeeeeee?!!ukishaona sehemu ambayo kamati ya TFF inafuta uchaguzi ama inawaondoa watu kwa sababu ambazo hazina mashiko ujue kwamba katika eneo hilo hakuna kundi lao ambao wanatarajia kwamba itakapofika wakati wa uchaguzi basi wanakwenda kuwapigia watu wao kura ili washinde na wao kama kamati waendelkee kula na kufaidi fedha za TFF.
Nakupa mifano michache tu hapa kama wewe ni mtafiti tafiti halafu usipobaini haya ninayokwambia basi ujue mimi ni muongo,angalia uchaguzi wa Mtwara namna ambavyo walifanya!,angalia uchaguzi wa Tabora TAREFA!,achilia mbali ucahguzi wa DRFA,angalia uchaguzi wa KATAVI kile ambacho wamekifanya wameufuta ule uchaguzi wakati tayari viongozi wamekaa madarakani kwa zaidi ya mwezi mzima.
Kanuni za uchaguzi ziko wazi kwamba kuna kamati ya uchaguzi ya eneo husika(MKOA) ambayo kazi yake haina tofauti na ile ya TFF ambayo ina mamlaaka kamili ya kushughulikia masuala yote ya uchauzi ikiwa ni pamoja na kuhakiki vyetu wa wagombea kupitia Baraza la Mtihani (NECTA) kama wana mashaka na vyeti vya muhusika,na inapofika kwa kamati ya TFF bado wanafanya vivyo hivyo kabla ya kuwaruhusu wagombea kuanza kampeni na hatimnaye kufanya uchaguzi.
Lakini cha ajabu yote hayo yanafanyika lakini cha ajabu baada ya mambo yoooooooote kukamilika kamati hiyo hiyo ya TFF inaibuka dakika za mwisho siku moja ama siku yenyewe ya uchaguzi ikidai inawaondo baadhi ya wagombea kwa kigezo cha kukosa sifa,ama kuwa na mashaka na vyeti vyao!!!!!!!!!!
Jamani kama si uonevuni nini ama kile ninachokisema kwamba ni kupanga safu yao ili siku ya uchaguzi wamchague mtu wao kwa maslahi yao ni nini???!!!!,hivi kama kweli ni hao hao TFF wamethibitisha wagombea wote kwamba wamekidhi vigezo mpaka wanaruhusiwa kufanya kampeni na kuingia kwenye uchaguzi nini kinatokea baadaye tena na kuibuka na hoja kwamba hawajakidhi vigezo,ndiyo maana tunasema kwamba Kamati ya Lyato ina walakini na inahitaji nayo kuvunjwa kwa sababu ndiyo inayoharibu mpira wa nchi hii.
Kwa kifupi ni kwamba kamati hii inataka kuwachukua watu ambao ni mbumbu ambao hawatakuwa na uwezo wa kuhoji matumizi mabaya ya fedha za TFF yaliyowasababisha wakina Tenda kujenga magorofa makubwa Dar,ikiwemo shilingi milioni 800 zinazotolewa kila mwaka na FIFA,shilingi Bilioni 1.4 zinazotolewa na Vodacom na ndiyo maana hata vilabu unaona haviambiwi ukweli wala kuoneshwa mkataba baina ya Vodacom na TFF.
Nakubali kwamba huenda Ndolanga anafanya makosa kama binadamu wa kawaida ama pengine anafanya makosa kwa makusudi kwa sababu anajua tu udhaifu ama pumba zinazofanywa na kamati ya Ucchaguzi ya TFF kwa sababu nayo inavurunda maeneo mengi,mfano ni huo uchaguzi wa FRAT wenyewe ambapo ni hiyohiyo kamati ya uchaguzi ndiyo iliyowapitisha wagombea na kuwaruhusu kufanya kampeni na siku ya uchaguzi asubuhi ndio wakatoa taarifa ya kuwaengua baadhi ya wagombea hao ambao walishinda na sasa wamefuta ushindi wao kwa madai kuwa hawakukidhi vigezo.
Swali la msingi la kujiuuliza hapa iweje wawapitishe na kuwaruhusu kufanya kampeni za uchaguzi na siku ya uchaguzi ndio wabainike kwamba hawana vigezo???!!hapa kuna tatizo na hasa kwa Lyato,lakini na yeye siku zake zinahesabiwa atabainika na kuanikwa haddharani bado naamini anavutiwa tu kasi.
Hata ukija kwenye sababu zilizosababisha wakaweka na vigezo vya elimu ya sekondari ni kwa sababu tu kuna vichwa vikali abavyo vilikuwa vikiwabana kila kona na kuwanyima usingizi kama wakina Abdalah Bulembo kwa hiyo wakajipanga namna ya kuwaondoa,lakini bado kuna taarifa kwamba kuna watu wao ambao wanawaingiza pamoja na kwamba hawana vigezo husika kwa sababu tu wanajua ni kura zao.
Ngoja kwa leo niishie hapa lakini nataka nikwambie kwamba siku za Kamati ya Ligi na TFF zinahesabika