Ndolanga, el maamry marais wa heshima tff

KIM KARDASH

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
5,139
1,139
[h=3][/h]

WENYEVITI wa zamani wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Said Hamad El Maamry na Muhiddin Ahmad Ndolanga wameteuliwa kuwa Marais wa heshima wa shirikisho hilo, katika Mkutano Mkuu wa TFF unaoendelea kwenye ukumbi wa NSSF Water Front, Dar es Salaam.


Habari kutoka ndani ya Mkutano huo, ambao utaendelea hadi kesho, zimesema kwamba viongozi hao wa zamani nchini wamepewa heshima hiyo na Wajumbe wa Mkutano Mkuu kutokana na mchango wao katika soka ya Tanzania, enzi zao wakiwa madarakani wakati TFF ikiitwa FAT (Chama cha Soka Tanzania).


Aidha, Wajumbe wa Mkutano Mkuu wameambiwa kuwa Hati ya Uwanja wa Karume haishikiliwi na benki kutokana na deni la ziara ya timu ya taifa ya Brazil Juni 2012, zaidi ya Sh. Bilioni 3, kwani deni hilo lilidhaminiwa na Serikali.


Mkutano huo unatarajiwa kufungwa muda si mrefu katika siku yake ya kwanza leo, ili Wajumbe wakawahi kuangalia mechi ya timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Ngorongoro dhidi ya Sudan, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.


Mkutano huo, utaendelea tena kesho katika siku ya mwisho na tarehe ya uchaguzi Mkuu, utakaofanyika mwishoni mwa mwaka huu, inatarajiwa kupangwa rasmi hiyo kesho.


CHANZO:BONGO STAZ BLOG
 
Ndolanga pamoja na ufisadi wote huo bado wanampa madaraka ya kuhudhuria mikutano ya TFF?tanzania nchi ya ajabu
 
Ndolonga ni tuhuma tu hakukua na ushahidi wowote kumtia hatiani kwa ufisadi na mahakama ilimsafisha huku aliyekua katibu wake akihukumiwa kifungo,na baadae michael wambura kamati ya maadili ya tff ikaja kubaini kwamba ndio alikua fisadi kwa kuitumia vibaya nafasi ya ukatibu mkuu wa FAT ikiwemo kuchukua mkopo binafsi benki kwa kuweka dhamana hati ya uwanja wa karume
 
ndolanga jembe sana waulizeni waumini wa msikiti wa mwembe chai alivyodhiti wezi wa kandambili.
 

Habari kutoka ndani ya Mkutano huo, ambao utaendelea hadi kesho, zimesema kwamba viongozi hao wa zamani nchini
wamepewa heshima hiyo na Wajumbe wa Mkutano Mkuu kutokana na mchango wao katika soka ya Tanzania, enzi zao wakiwa madarakani wakati TFF ikiitwa FAT (Chama cha Soka Tanzania).

I see!!.....very interesting, nilikuwa sijui kama nchi hii imepiga hatuwa kubwa katika soka sasa ndio nafumbuliwa macho. what i can say the wonders shall never end in this country.
 
Back
Top Bottom