Yona F. Maro
R I P
- Nov 2, 2006
- 4,201
- 235
Jumapili nilipata bahati ya kutembelea baadhi ya maeneo ya mtaani kwetu ninakoishi , katika pita pita zangu nilikuta zogo sehemu moja kati ya wanandoa wawili wa jinsi tofauti yaani mke na mume , samahani kidogo niliposema mke na mume jinsia tofauti , kuna sehemu zingine kuna wanandoa wawili wa jinsia moja yaani mume kwa mume wanaishi pamoja ndoa hizi zipo ila hao walikuwa ni jinsi tofauti .
Huyo mwanaume alikuwa anamshambulia mkewe kwa makofi , na matusi moto moto huku akitamka maneno kama SIKU ZOTE NAKUOMBA HUNIPI , UNATAKA NANI ANIPE , mwanamke analia tu hataki kusema nini kinachoendelea .
Walipoamuliwa na majirani kesi ikaanza mwanamke anasema anataka majibu ya vipimo vya ukimwi vya yule mwanaume wake ndio ajue wako wapi wanaenda wapi na ndio hapo ukurasa mpya ufunguliwe .
Ilionyesha mwanamke bado kiumb dhaifu katika hizi ndoa hadi anakubali kupigwa kudhalilishwa na kusingiziwa mambo mengine mengi tu wakati yeye anatetea masilahi yake .
Wanasema haya ni mambo ya ndani kwahiyo hajaenda kushitaki hata kwa wazee wa mtaa serikalini wala kwa chombo chochote kile cha sheria anaona kupigwa vile ni haki yake pengine ndio mvuto katika ndoa yake .
Kesi iliendelea mwisho wa siku katika kikao hicho wakamshauri mwanamke amvumilie mumewe watumie kinga basi kama hamwamini lakini mwanaume apate haki yake ya ndoa ambayo ni lazima .
Hii haki inayoongelewa hapa ya tendo la ndoa kama vile waliandikishiana mahakamani kwamba ni lazima apate kwahiyo analazimisha kama mwenzako hataki , hajisikii na anasababu zake za msingi hakuna haja ya kulazimisha
Tena huyu mwanamke anaweza kumshitaki mumewe kwa shambulio la aibu , na kujaribu kumbaka , majirani wapo na walisikia maneno ya kidume alivyokuwa anaongea ikifanyika hivi leo kwa huyu mmoja naamini vidume vingine vyote vinashika njia ya kujua majukumu yao ni nini .
Dunia ya sasa sio ya enzi zile sasa hivi kila mtu ni kichwa katika familia na nyumba kwa ujumla kila mtu anatakiwa haki na heshima ndani ya nyuma na kila mtu pia anastahili huduma na mambo mengine ya kifamilia bila kujuli jinsia , mvuto , muonekano wala uwezo wake wa kitu Fulani hivi ni vitu vya kupitwa na wakati tu .
Jamii ya kike sasa iamke ichangamkie haya matatizo katika ndoa na majumbani mwao iyaandike , iyakemee na itoe mafunzo kwa wengine ambao hawaelewi haki na misingi ya familia bora .
Na kukumbushia ule msemo wa mwanamke na maendeleo