Ndoa Zingine Bwana

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
218
Jumapili nilipata bahati ya kutembelea baadhi ya maeneo ya mtaani kwetu ninakoishi , katika pita pita zangu nilikuta zogo sehemu moja kati ya wanandoa wawili wa jinsi tofauti yaani mke na mume , samahani kidogo niliposema mke na mume jinsia tofauti , kuna sehemu zingine kuna wanandoa wawili wa jinsia moja yaani mume kwa mume wanaishi pamoja ndoa hizi zipo ila hao walikuwa ni jinsi tofauti .

Huyo mwanaume alikuwa anamshambulia mkewe kwa makofi , na matusi moto moto huku akitamka maneno kama SIKU ZOTE NAKUOMBA HUNIPI , UNATAKA NANI ANIPE , mwanamke analia tu hataki kusema nini kinachoendelea .

Walipoamuliwa na majirani kesi ikaanza mwanamke anasema anataka majibu ya vipimo vya ukimwi vya yule mwanaume wake ndio ajue wako wapi wanaenda wapi na ndio hapo ukurasa mpya ufunguliwe .

Ilionyesha mwanamke bado kiumb dhaifu katika hizi ndoa hadi anakubali kupigwa kudhalilishwa na kusingiziwa mambo mengine mengi tu wakati yeye anatetea masilahi yake .

Wanasema haya ni mambo ya ndani kwahiyo hajaenda kushitaki hata kwa wazee wa mtaa serikalini wala kwa chombo chochote kile cha sheria anaona kupigwa vile ni haki yake pengine ndio mvuto katika ndoa yake .

Kesi iliendelea mwisho wa siku katika kikao hicho wakamshauri mwanamke amvumilie mumewe watumie kinga basi kama hamwamini lakini mwanaume apate haki yake ya ndoa ambayo ni lazima .

Hii haki inayoongelewa hapa ya tendo la ndoa kama vile waliandikishiana mahakamani kwamba ni lazima apate kwahiyo analazimisha kama mwenzako hataki , hajisikii na anasababu zake za msingi hakuna haja ya kulazimisha

Tena huyu mwanamke anaweza kumshitaki mumewe kwa shambulio la aibu , na kujaribu kumbaka , majirani wapo na walisikia maneno ya kidume alivyokuwa anaongea ikifanyika hivi leo kwa huyu mmoja naamini vidume vingine vyote vinashika njia ya kujua majukumu yao ni nini .

Dunia ya sasa sio ya enzi zile sasa hivi kila mtu ni kichwa katika familia na nyumba kwa ujumla kila mtu anatakiwa haki na heshima ndani ya nyuma na kila mtu pia anastahili huduma na mambo mengine ya kifamilia bila kujuli jinsia , mvuto , muonekano wala uwezo wake wa kitu Fulani hivi ni vitu vya kupitwa na wakati tu .

Jamii ya kike sasa iamke ichangamkie haya matatizo katika ndoa na majumbani mwao iyaandike , iyakemee na itoe mafunzo kwa wengine ambao hawaelewi haki na misingi ya familia bora .

Na kukumbushia ule msemo wa mwanamke na maendeleo
 
Shy,
Hii inaonyesha wazi ni jinsi gani wanawake bado wanashindwa kutambua haki zao muhimu katika maisha ya ndoa!
Huu mfano wako ni hai kabisa na hata mimi ninayo mifano kama hii na ambayo inawahusisha wanawake wenye elimu nzuri na kazi nzuri lakini wanapata harassment kutoka kwa waume/boyfriend zao kwa kudhania hayo ni masuala ya ndani ya nyumba(Ndoa).

Ni wakati mzuri sasa wakina dada wote wajue kwamba kupigwa/kunyanyaswa/kubakwa na wenzi wao ni kosa sawa na kama vile angefanyiwa na mtu asiyemjua na amchukulie sheria ili watu wenye tabia hizi waache.
La pili linatokana na sisi wanaume... sisi tunajulikana tuna nguvu na pia ndio kichwa cha familia lakini kwa nini tunatumia vibaya haya majukumu tunayopewa kama akina baba?? Nafikiri tungeonekana waungwana sana kama tungetreat wake zetu kwa heshima kubwa na kuwafanya nao waige kile tunachokifanya kwao!!

Kwa kweli ndoa kama hiyo Shy haina raha cos huwezi jua huyo mama anawaza nini haswa baada ya kichapo na kubakwa .... inaweza kuwa suicide au murder!!!!
 
Hapa tunayo Kesi.
1.Je, Sheria ipi inaweza kutumika, kama mke akiamua kulichukua suala hili kisheria?
2.JE, Sheria ya ndoa inasema nini katika tukio kama hilo?

Naomba tujadili.
 
Hapa tunayo Kesi.
1.Je, Sheria ipi inaweza kutumika, kama mke akiamua kulichukua suala hili kisheria?
2.JE, Sheria ya ndoa inasema nini katika tukio kama hilo?

Naomba tujadili.

66. For the avoidance of doubt, it is hereby declared that, notwithstanding any custom to the contrary, no person has any right to inflict corporal punishment on his or her spouse.
Hiyo hapo mkuu
ila hata bila hiyo kuna sheria za kila siku na tunajua kwamba huyo jamaa anaweza kwa njia moja au nyingine kuwa linked na ubakaji, intention to infect his spouse with HIV etc!

Its just a matter of getting deep down into the details na kuwanail the culprits!! Ladies i insist piganieni haki zenu wenyewe wala msisubirie sisi wanaume tutengeneze NGO za kuwatetea.... Unite your voices!
 
aache upumbavu atoe haki ya mumewe si alikubali kuolewa na alijuilishwa mapema moja ya jambo la lazima ni kutoa huo mchezo kwa bwana wake.

sasa nyinyi mlitaka huyo bwana akapate wapi hio haki yake?


pengine shy hapo walikuwa wakivuta spidi yakwenda kupeana vizuri nimesikia kuna makabila hayaoni raha mpaka kichapo kianguke ndio atoe.
 
Unajua mtu wa pwani you have raised a very important question; Mume hiyo haki ya unyumba akaipate wapi kama mke hataki kumpa? na Je mwanamke hana haki ya kujua majibu kama kweli jamaa ni mzima au vipi? Au ukishaingia kwenye ndoa huna kauli?

Na jamani swala zima la uchumi katika ndoa lina nafasi gani katika ndoa imara na yenye furaha?

Tufike point tukubaliane kwamba hizi human rights bwana are more enjoyed by the elites hawa wanawake wasomi ndo unakuta wako mstari wa mbele wa kuzihubiri bila kureflect mazingira yetu ya kimaskini! hivi kweli familia za kijijini ambapo mzee anategemewa kununua chumvi na mafuta ya taa, mama ana watoto saba, peasant ambaye hata chakula anacholima hakiwatoshi.and on...bado tunasema tudai haki? wazidai wapi? na kwa nani? I strongly believe that cha muhimu ni kuwawewezesha wananchi kiuchumi. Mengine yatakuja. I support rights for ALL but reality check ni muhimu.

Ni maswali magumu lakini hatuna budi kuyafikiria. Hizi nyimbo za human rights katika lindi la umasikini, zitabakia kwenye makaratasi tuu na miradi ya NGO. Practically ni ngumu! Usawa hauwezi kuwepo wakati familia ziko kwenye lindi la umasikini.

Tusiige ya ulaya...jiulize mfano wanawake waliruhusiwa lini kupiga kura huko magharibi? tuhangaike kwanza watu wapate mkate..haki zitakuja tuu!
 
Chakwanza kuangalia ni kama kweli watu hao ni wanandoa halali,aidha kama wamefunga ndoa ya kimila,kikristu,kiislam,kiserikali hiyo haijalishi.Vilevile tunapaswa kujua watu hawa ni vimada au ni wapenzi tu.Kitu kingine cha kuangalia ni muda walionao wanandoa hao then unaweza ukachangia mada hii tofauti na hapo tutachekesha.Hivyo mtoa mada alikua bado anajukumu la kutujulisha wagomvi hao ni wapo katika kundi gani kati ya hayo niliyoyataja hapo juu.

Kimsingi ili ndoa ikamilike there must be "EJACULATION".Kama hii itafeli then hakuna ndoa.Samahani kidogo,naomba kwanza kabla sijaendelea nieleze maana ya ndoa:NDOA NI MAKUBALIANO YA WATU WAWILI WENYE JINSIA TOFAUTI NA KWA RIDHAA ZAO WENYEWE WAKIWA NA KUSUDIO LA KUISHI PAMOJA KATIKA MAISHA YAO.

Kwa hiyo ndoa inakamilika kwa kukamilisha badhi ya taratibu kutegemea na aina ya ndoa kama nilivyoziainisha hapo juu bila ya kusahau "EJACULATION".

Nije kwa suala la HIV problem,suala lilitakiwa liangaliwe mapema kabla ya kwenda kanisani ili kujua afya zao kabla ya ndoa.Kama mwanaume angegundulika kama ameathirika then mwanamke alikua na hiari ya kukataa kufunga ndoa.Lakini kama mwanamke ataridhia kufunga ndoa na mtu aliye athirika na HIV then hilo ni jukumu lake.Vivyo hivyo kama mwanamke angekutwa ameathirika.

Lakini hata kama ndoa itakua imekwishafungwa na mwanamke akahisi kwamba mumewe nyendo zake sio nzuri then anahaki ya kwenda kucheck afya zao ili kujua mustakabali wa life utakuaje.

Kwa kitendo alichokifanya mwanaume huyo dhidi ya huyo mkewe,mke anaweza kumfungulia shitaka la kumdhalilisha.

Pamoja na hayo yote,tunaposema ndoa tunamaanisha ni UNYUMBA na sio kitu kitu kingine,kama mwanaume atalazimisha au kwa vyovyote vile maadamu anataka unyumba,then kosa la kubaka halipo kama ni mwanandoa wake halali.
 
aache upumbavu atoe haki ya mumewe si alikubali kuolewa na alijuilishwa mapema moja ya jambo la lazima ni kutoa huo mchezo kwa bwana wake.

sasa nyinyi mlitaka huyo bwana akapate wapi hio haki yake?


pengine shy hapo walikuwa wakivuta spidi yakwenda kupeana vizuri nimesikia kuna makabila hayaoni raha mpaka kichapo kianguke ndio atoe.


Kama kweli hataki hilo tendo na mumewe halali anangoja nini hapo nyumbani? Inawezekana sana ana dume lingine hapo jirani yeye humaliza naye. Kushaurian ni muhimu nasio kunyimana. ampe tu.
 
Yawezekana si wanandoa hao huenda jamaa alivuta tu mzigo akaweka ndani...Kwani kama ni wanandoa unyumba hauombwi kwa ngumi na matusi. na hata kama mwanamke anahisi jamaa ameathirika hilo ni jambo la wao kulizungumza wawili tena kwa utulivi sana ili wakubaliane nini cha kufanya..Kwani katika mazingira ya kawaida kwenye ndoa kunapotokea matatizo wa kwanza kuyatafutia ufumbuzi ni mume na mke kabla ya kutaka ushauri mahali pengine.

Vinginevyo kama mwamanmke alikuwa ana wasiwasi sana na afya ya jamaa bora angeondoka ili kuepuka kushiriki ngono na mtu anayemuhisi ameathirika sio unakaa kwa mwanaume ukiombwa mchezo unaleta nyimbo...
 
Maswala ya ndoa si marahisi kama tunavyotaka kuona au kujibu. Mila na desturi hazitoi majibu ya maswali yote ya ndoa.

Sheria na taratibu za kidini hazijibu maswali yote ya ndoa. Na mifano mingi ambayo watu wanaelekezwa wafuate ya wanandoa wengine katika jamii haitoshelezi kujibu maswali yote ya ndoa. Ndoa ina mambo mengi kweli makubwa na madogo madogo ambayo hayafanani kwenye kila ndoa. Hivyo ni muhimu wanandoa wakatailor made ndoa yao kwa kuchukua/kuazima kutoka kila fungu hapo juu ili kukidhi haja za au kuweza kujibu maswali yao.

Story tuliyopewa hapa ni fupi kweli, kwani kuna mengi hatuwezi kuuliza. Kama walivyochangia jamaa wengine kuna mengi hatuyajui.

Kukimbilia haki za kinamama kuna uzuri na ubaya wake. Kubaki tu kwenye mila na desturi kuna uzuri na ubaya wake na kuzingatia tu sheria na maelekezo au mifano tuonayo toka kwa wanandoa wengine katika jamii kuna athari zake nyingi tu. Ukienda kwenye dini nako ni hivyo hivyo.
 
Kila siku nimekuwa napata mkagasiko na ukakasi ninapojaribu kuifikiria ndoa na ni nani hasa ni chanzo cha matatizo kwenye ndoa. Niliongea na Babu mmoja mwenye umri wa miaka 76 last month nilipoenda kumtembelea akaniambia kwa mtazamo wake hapo baadae ingawa hajui ni lini kutakuwa hakuna ndoa kwenye nchi kama Tanzania kwa sababu ndoa nyingi sasa zimepoteza ule mtazamo wa kikwetu na kuleta ule mtazamo wa Kimagharibi. Kimsingi alisema kuwa kipindi cha nyuma ilikuwa ni ngumu sana kwa mwanaume na mwanamke kuachana halfu kesho yake ukakuta mmoja kati ya wale walioachana wana wapenzi wapya. Anasema kuwa watu hawa walioachana walikuwa wakikaa kwa muda kutafakari nini kilichopelekea muachano wao ndipo kama imeshindikana kusuluhisha basi waende kwenye mahusiano mengine wakiwa wamejiapanga barabara tofauti na siku hizi mtu anatoka na madhaifu kwenye ndoa au mahusiano haya halafu anakwenda nayo kwenye ndoa au mahusiano mengine.
Lakini pia alizungumzia hii tabia ya kuanza kuishi kwenye ndoa kinyemela ambayo ipo sana kwenye maisha ya sasa hasa kwa vijana walioko vyuoni na sehemu nyingine kuwa chanzo cha mifarakano kwenye ndoa hapo baadae. (hizi ndoa za kinyemela nitazungumzia wakati ujao
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom