Mkuu mi nipo ila nahisi we ndo umeadimika na una siku special za kujitokeza humu.
...umeadimika aisee, kwema?
well,...sasa huu usasa unafaida kweli na ndoa kwenye kizazi hiki na
vinavyokuja, au ndio tutaishia kuzalishana watoto na kuishia na u single parent?
...hii taasisi si inapoteza muelekeo mama/baba anapojiona ana kibri cha kulea mwanawe bila mwenza?
Tunatafakari athari ya jambo hili kwa vizazi vijavyo jamani?
Mbu,
Kuna suala la heshima kwa taasisi ya ndoa. Nadhani hili limechakachuliwa sana hadi watu wanashindwa kuelewa maana yake. Pia watu wanaenda enda tu bila hata kujua haki na wajibu wao wanapoingia kwenye hii biashara!
Kazi iliyopo mbele yetu ni kubwa ila tutafika ingawa majeruhi watakuwa wengi sana!!
...Shauri yako Mkuu...bora utemee mate chini 🙂🙂 bucha nyingine nyama zao huwa ni vigumu sana kusahaulika....safi, laini na ladha yake huwa ni tamu sana...kamwe huwezi kusahau lol!
HEKIMA na BUSARA za babu ,DAIMA NITAZINGATIA.....thnks alot babu DC ,nikioa kwa maadili nitakayokuwa nayo kwa wife ,akiniuliza chanzo sitasita kumhabarisha kuhusu ww.:flypig:Hata wanaume bwana nao maadili yao yanaporomoka kwa kasi kiasi kwamba yanakaribia kwenye mstari wa zero!!
Mfano, utajiitaje mwanamume wakati unakimbia kimbia na vitoto vya majirani zako na hata wafanyakazi wao? Au unakwenda kwenye ufuska na kurudi saa 11 asubuhi!!
Wazee wetu walikuwa wanajua kuwa mama watoto ndiye nambari one...Wengine wote ni washika pembe, mama ndiye anayekamua. Sasa hivi mnawafanya wake zenu washika pembe...Is that fair??
Hao vijana wenu wa dot com wanayajua hayo?? Au wao wanamind kumwagiwa misitu ya maua, vocha za kumwaga, simu na sms kila sekunde, ..... na vidume kupewa ngono hadi wavimbiwe??
Mkuu mi nipo ila nahisi we ndo umeadimika na una siku special za kujitokeza humu.
Usasa hauna faida na kwa upande mwingine una faida pia,unaweza kufanya nini kama mtu amechoka kukaa na wewe
na ana uhuru wa kukuacha?na kwa upande mwingine amekupunguzia mzigo,ila tunakoelekea ndoa za kufunga kwa
mkataba wa miaka kadhaa itakuwa na nguvu zaidi kuliko zakufunga forever.
Mi nadhani tunakoelekea ndoa hazifungwi,na zikifungwa hazitadumu mana watu hawapendi kubughudiwa.
Mi namfahamu mama mmoja anatembea na rafiki wa mwanae,sasa hapo unategemea nini,hakuna malalamiko na
maisha bado yanasonga.
hahahaha...naam, naam, ....haya ndio ma Egoli aliyoyaandika mwj1....
yaani usipomnunulia mke maua valentine day, sijui birthday card, au ukasahau kum wish happy anniversary...yote mazuri uliyomfanyia yanageuka "ajua!".....aisee 'mapenzi' ya kisasa ni usanii wa gharama acha bana!
...Nakubaliana nawe Mkuu DC. Pia uvumilivu ambao ni muhimu sana katika kudumisha ndoa kama uliokuwepo miaka ile sasa hivi hakuna kabisa.
Nimeshasikia siku hizi hata wasichana hawataki kuolewa na wao wanataka kuoa! Siri hapo ipo kwenye Kuoana, kuoa au kuolewa?.
Watakaodumu ni wale wanao oana na si wanao olewa wala kuoa. Huo ni mtazamo wangu, na mimi binafsi yangu ni "proof" ya hilo. tume oana na Gozi langu. Hajanioa wala Sikumuoa. Nadhani vijana wa sasa na wajao wanatakiwa waelewe maana ya kuoana.
Mkuu mi nipo ila nahisi we ndo umeadimika na una siku special za kujitokeza humu.
Usasa hauna faida na kwa upande mwingine una faida pia,unaweza kufanya nini kama mtu amechoka kukaa na wewe
na ana uhuru wa kukuacha?na kwa upande mwingine amekupunguzia mzigo,ila tunakoelekea ndoa za kufunga kwa
mkataba wa miaka kadhaa itakuwa na nguvu zaidi kuliko zakufunga forever.
Mi nadhani tunakoelekea ndoa hazifungwi,na zikifungwa hazitadumu mana watu hawapendi kubughudiwa.
Mi namfahamu mama mmoja anatembea na rafiki wa mwanae,sasa hapo unategemea nini,hakuna malalamiko na
maisha bado yanasonga.
HEKIMA na BUSARA za babu ,DAIMA NITAZINGATIA.....thnks alot babu DC ,nikioa kwa maadili nitakayokuwa nayo kwa wife ,akiniuliza chanzo sitasita kumhabarisha kuhusu ww.:flypig:
Kuna swala nikuulize hapo kwnye kuoana, nnavojua kwenye usilam kijana wa kiume anapoozeshwa huambiwa " UMEKUBALI KUMUOA FULANI BINTI FULANI and so on" hakuna kitu mnaona, Je hii ibadilike nayo au imekaaje?
i wish muda wangu ukifika niwe on th right boat kwakweli.Thamani na maana nzima ya ndoa imebadilika na kushuka for the original meaning ya ndoa sasa imebadilika Mbu.... Hivo maadili na kuthamini ndoa kupungua haviepukiki.... Tukiangalia kwa upana sasa hivi kuna ndoa kati ya wanadamu wa jinsia moja, kuna ndoa ambazo zimehalalishwa kabisa na kua ni za mkataba... Kuna muingiliano wa dini siku hizi... Watu wa dini tofauti waona na ndoa kufanyika bomani.... Naaamini kua nidhamu ya uoga dhidi ya ndoa; spouses wenye woga zaidi dhidi ya ndoa zao ni wale walooana kwa dini moja kuliko wa bomani.
Tukiangalia kua nani alaumiwe.... Nadhani jamii nzima inwajibika kuweza laumiwa, kupokea na kukumbatia mambo mengine yasio faa na huchangia kupotosha vijana wadogog dogo kujiingiza katika maswala mbali mbali yasio faa kama vile ushoga...
Kusema twaweza epuka gharika hili? Siamini.... Haya mambo hayalazimishwi, evolution ni inevitable let us just hope that in the long run ita evolve for the better kuliko tulipo hapa.
...Nakubaliana nawe Mkuu DC. Pia uvumilivu ambao ni muhimu sana katika kudumisha ndoa kama uliokuwepo miaka ile sasa hivi hakuna kabisa.
Mbu kwanza kabisa naunga mkono hoja zote za waliochangia tayari. Nakubaliana na maelezo sawia aloyatoa AshaDii na wengineo ila naomba nitoe ufafanuzi kidooogo.
Kuhusu women's rights au kujitambua kwa wanawake kama ilivyosemwa na wengi waliotangulia. Kwa mtazamo wangu hiki si kitu kibaya hata kidogo. Sidhani kama ni vibaya kuwa au kuzitambua haki za kila mmoja wetu. Tatizo nilionalo hapa ni namna tulivyoyapokea haya "Mahubiri" ya Women's Rights. Wanawake wengi tumejikuta tukishabikia haki hizi kama wafungwa washabikiavyo msamaha wa rahic bila kufikiria ukitoka jela humu utaishije ili usiharibu tena. Wanawake wengi wamepotea mahubiri haya kwa ushindani ule wa ...haya sasa nasie tuna haki. Ushindani ambao umepelekea wengi wetu kujikuza na kujikweza huku tukizisahau staha zetu, heshima zetu na ustaarabu wetu.
Laiti tungeyapokea 'mahubiri' haya na kuyajazia kwenye kikapu chetu chenye staha, heshma na ustaarabu apaswao mwanamke badala ya kuzitoa staha, heshima na staarabu zetu na kuzitupa nje ili Women's rights zipate nafasi. (hapa ninayo mengi kuongea utafikiri nimelipwa na TAMWA)
Kuhusu Upendo:
Kwa mtazamo wangu mie haya mapenzi ya "Egoli" tuliyoyaiga toka kwa wazungu yamechangia kwa kiasi kikubwa udhaifu katika ndoa nyingi za siku hizi. Hii kujidai unataka kufall in love ndo uoe/olewe imetupelekea kuiumbia na kuikubali counterprt ya falling in love ambayo ni falling out of love. Siku hizi si jambo la kushangaza kujikuta unaitwa kwenye kusuluhoisha ndoa ambayo mmoja wa wanandoa hao alilala tu usiku na kuamka asubuhi akiwa ameshafall out of love na sasa anadai talaka au anataka kuvunja ndoa. Na ajabu sana kuna kila aina ya justification ya hii falling out of love ambayo mwisho wa siku tunalazimika kukubaliana na muota ndoto huyo.
Wazee wetu wa zamani hawakuwaga na falling in love bali walikuwa na Growing in love...it just keep on growing hakuna kufall out na ndio maana walikuwa wavumilivu. Kwa kuwa unaishi kwenye ndoa ambayo kadri siku ziendavyo love inajijenga, kukua na kukomaa hata ukifanyiwa kosa gani wewe unajihisi kumpenda zaidi ingawa kwa manung'uniko kwa ndani! Ndoa za siku hizi kwa kadri unavyokosea mwenzio ndivyo anavyoendelea kuizungusha door knob ya love na mwisho anaufunguua na baaam amefall out.
Samahani imekuwa ndefu.
hilo swala la kuishi kwenye ndoa linatakiwa liwepo,ila itawezekana?amegundua kuwa hakupendi na anao uhuru wa kukuachaMkuu suala la kuishi kwenye ndoa linatakiwa liwepo tu pale panapokuwa na maelewano na amani. Hili ni jambo la muhimu sana.
Enzi zile, jamiii nzima ilihakikisha ndoa inapewa msaada mkubwa ili idumu. Lakini kama ilionekana kuwa haiwezekani, basi wahusika walipewa pia msaada ili waachane salama!!
Hadi sasa principle ni hiyo hiyo ila kinachokosena ni social system ya kusaidia wanandoa pale ambapo wanahisi hawawezi kuishi pamoja. Kwa mfano, sababu zinazotolewa na baadhi ya watu wanaochana ni za ajabu ajabu ukilinganisha na huko nyuma!
Mtu anamwacha mwenzake eti amegundua hakumpenda...Je anafikiria nini kuhusu maisha ya mtu ambaye anamwacha??
Wanataka kula ila wasiliwe...very pathetic!!
huo uvumilivu mwenzio atakuwa nao?
babu DC kwa wtoto wa dotcom ukiwa realistic wanakuona umepitwa na wakati na ni mnoko.Hao vijana wenu wa dot com wanayajua hayo?? Au wao wanamind kumwagiwa misitu ya maua, vocha za kumwaga, simu na sms kila sekunde, ..... na vidume kupewa ngono hadi wavimbiwe??
Kuna swala nikuulize hapo kwnye kuoana, nnavojua kwenye usilam kijana wa kiume anapoozeshwa huambiwa " UMEKUBALI KUMUOA FULANI BINTI FULANI and so on" hakuna kitu mnaona, Je hii ibadilike nayo au imekaaje?