NDOA: Zamani vs Siku hizi

Kwahiyo babu wewe hisia zako kwa bibi DC zikoje?
Mnaishi kwasababu umemzoea au kwasababu unampenda?

Mhhh,

Very tricky...ila naweza kukueleza kuwa naishi naye kama mwenzangu wa karibu sana.. Lolote lake ni langu ingawa sina hakika kama kweli langu ni lake!!

Ndo maana nilisema huko nyuma kwamba siwezi kumtelekeza mke wangu kwenye tatizo lolote (however simple it might be) hata kama a few minutes ago kanifanyia kosa kubwa au kuniudhi sana!! Nadhani mafundisho ya baba hapa yanachukua nafasi. Alikuwa anatueleza kuwa hawezi kumchapa mtoto hata kama kafanya kosa gani kabla ya kula endapo ni muda wa chakula!! Mtakula kwanza halafu unapata zawadi yako!!

Kama nampenda Bibi DC au la, bado hata mie najiuliza!!!
 
Hahahaha, kwa maelezo hayo babu ni dhahiri unampenda na sio unaishi nae kwa mazoea.

Mmh nimependa hiyo ya kumwacha mtoto ale kwanza (kama ni muda) ndio aadhibiwe.Makes a lot of sense.
 
Lizzy,sijakuelewa uliposema napinga kwa sababu nampinga fulan!Pia sipo hapa kupinga bali naeleza mtazamo wangu!Pia naomba uniambie kupenda kwa tafsiri yako ni nini!
 
Hahahaha, kwa maelezo hayo babu ni dhahiri unampenda na sio unaishi nae kwa mazoea.

Mmh nimependa hiyo ya kumwacha mtoto ale kwanza (kama ni muda) ndio aadhibiwe.Makes a lot of sense.

Ahsasnte sana Lizzy,

Naamini sasa unaweza kuelewa kwa nini yule baba aliyeelezwa na Makaburini kwa maoni yangu hastahili tena kuitwa tena mume (achana na kwamba facts zilizopo hazijitoshelezi)!!
 
Reactions: Mbu

Babu acha tu.........hili neno wengi hatulielewi lakini mie nina ushuhuda wa mdada ambaye ameshakuwa na mahusiano makuu stable mawili) (meaning ndoa ya kwanza, bahati mbaya mume alifariki kwa ajali; amepata mwingine ambaye wanatarajia kufunga ndoa April 2012, kwa sababu tu aliambiwa anapendwa..................meaning yeye anarespond to being approached and loved (kwa kuwa ameapproachiwa/ na kuelezwa kuwa anapendwa) tu. Hakuhusiani na yeye kupenda na bado amekuwa na maisha mazuri sana kimapenzi.
Ukimuuliza anajibu kuwa yeye anampenda anayempenda!!!!
 

Mkwe maisha ya ndoa ya sasa mmmmhhh
taabu tupu ikiwezekana bora kutokuoana
mkwe mie tofauti hahahahahahahaa
hatapata taabu za hawa vijana :lol::lol:
 

Nimempenda huyo dada....Kuna sababu gani ya kuhangaika wakati kuna mtu ambaye amekueleza kuwa anakupenda na kukuonesha upendo kwa vitendo. Actually, hata kwa kutumia common senses, huwezi kuacha kumpenda mtu wa namna hiyo!!

Ngoja kwanza niishie hapa kwani Lizzy keshaanza kunichokonoa!!
 
Ahsasnte sana Lizzy,

Naamini sasa unaweza kuelewa kwa nini yule baba aliyeelezwa na Makaburini kwa maoni yangu hastahili tena kuitwa tena mume (achana na kwamba facts zilizopo hazijitoshelezi)!!

Hahahaha, babu najaribu kufikiria "mume kacheat na nimemfuma jana, mpaka leo hajaomba hata samahani ila kwa bahati mbaya kwake asubuhi ameamka hali sio nzuri au kaanguka akavunja hata mguu" je ntampeleka hosp au la? Katika hali ya kawaida ntampeleka ila akishatoka huko mambo yanarudi kama yalivyokua.

Yule besti wa Makaburini binafsi nashindwa kumhukumu kutokana na namna mke alivyomwaproach shemejie. Plus, lile sio swala la kufa na kupona, angeweza kuomba hata mmoja wa shoga zake wamsaidie.
 
...jamani mtanisamehe siwezi kuwa quote nyote, ila nitaanza kwa michango iliyonigusa zaidi...


...dahhh!



....aiseee!?....Lizzy umegusia mambo ya msingi kabisa niliyokuwa nayategea kwenye mdahalo huu...



...am humbled, mwj1 ubarikiwe kwa ufunguo huu....dahhhh!?
 
Wanawake wasasa maadili yameporomoka kutokana na utandawazi kila nikijitahidi kuoa nashushwa dah.

Hata wanaume bwana nao maadili yao yanaporomoka kwa kasi kiasi kwamba yanakaribia kwenye mstari wa zero!!

Mfano, utajiitaje mwanamume wakati unakimbia kimbia na vitoto vya majirani zako na hata wafanyakazi wao? Au unakwenda kwenye ufuska na kurudi saa 11 asubuhi!!

Wazee wetu walikuwa wanajua kuwa mama watoto ndiye nambari one...Wengine wote ni washika pembe, mama ndiye anayekamua. Sasa hivi mnawafanya wake zenu washika pembe...Is that fair??
 
Ahsasnte sana Lizzy,

Naamini sasa unaweza kuelewa kwa nini yule baba aliyeelezwa na Makaburini kwa maoni yangu hastahili tena kuitwa tena mume (achana na kwamba facts zilizopo hazijitoshelezi)!!

Babu mi nataka kuoa sasa kila nae mpata vigezo havizingatiwi wasasa anapenda sana kushika shika kimeo changu cha mchini na anataka ajue nani kanipigia au kasisms hapa wasiwasi wangu mnaweza kuja kula pilau alafu baada ya wiki nikamtimua na malboro.
 

Ni haki ambazo zinawahusu wanawake ambazo bado hazijawa zao? It doesn't get any asinine than that! Unajua maana ya haki wewe?

Merriam-Webster's Learner's Dictionary

Women's rights - Wikipedia, the free encyclopedia

http://www.thefreedictionary.com/Women+Rights
 


Hapo (blue) tuko pamoja.....Inapobidi unamsaidia kama binadamu mwingine yeyote ambaye ungempatia msaada endapo angepata emergency mbele yako!!

Kwenye red, Makaburini aliitwa baada ya mume kukataa kutoa msaada au nimesahau??
 
Mkwe maisha ya ndoa ya sasa mmmmhhh
taabu tupu ikiwezekana bora kutokuoana
mkwe mie tofauti hahahahahahahaa
hatapata taabu za hawa vijana :lol::lol:

Hhahahahha, ndio unaniingiza mjini hivyo mkwe?Usije ukamnyanyasa wakati mwenzio anakupenda alafu arudi kunililia.
 
Ahsasnte sana Lizzy,

Naamini sasa unaweza kuelewa kwa nini yule baba aliyeelezwa na Makaburini kwa maoni yangu hastahili tena kuitwa tena mume (achana na kwamba facts zilizopo hazijitoshelezi)!!


....swadaktaaaaaaa......!

ila mtazamo wangu nawe unatofautiana kwenye quotes alizoziainisha makaburini;

picha ninayoipata ni kwamba mke alinunua gari kiushindani, na mume kwa gubu lake kama zali vile siku hiyo lilipomgomea ndio naye akatapika machungu yake!

Wadhani iwapo gari hilo kwenye manunuzi yake huyo mume angekuwa ameshirikishwa bado angeendelea kumsusia?
Kumbuka mkuu, sie vijana wa zamani tuna kasumba mke hata akiwa na uwezo vipi, bado anastahiki kupata go ahead toka
kwa mumewe kufanya maamuzi makubwa ya maisha mfano kujenga, kununua gari nk....au?
 
Babu mi nataka kuoa sasa kila nae mpata vigezo havizingatiwi wasasa anapenda sana kushika shika kimeo changu cha mchini na anataka ajue nani kanipigia au kasisms hapa wasiwasi wangu mnaweza kuja kula pilau alafu baada ya wiki nikamtimua na malboro.


Fidel, ukishapata walau mmoja ukahisi anaweza kuwa mwenzi wako, basi hao wengine wape likizo umpe yeye nafasi hadi itakapothibitika kuwa haiwezi uone kama itakupa tatizo.

Sasa unataka uwe na dada wa watu wakati huo umeegesha magari kibao getini....It will never work labda upate mtaalamu wa kucheza usanii kama huo!
 

Mkuu,

Katika mazingira kama hayo, you have to be a human being first and next you call yourself Mbu or DC!!

Huwezi kunipa sababu ya msingi ya mume kutomsaidia mke wake wakati wa shida halafu useme hiyo ndoa haijapata permanent damage!!

Kaka kumbuka ndoa ni ya watu wa 2...an injury to one must be an injury to both...If one is injured and the hubby anafanya tafrija...that is the beginning or even the end of things fall apart!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…