Ndoa zaidi ya ndoano!

Museven

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2011
Posts
629
Reaction score
452
Heshima kwenu wana JF nyote.
Ukweli nahitaji sana msaada wa mawazo yenu. Mimi nimeoa na nina watoto 2. Tatizo kubwa ni huyu mama-watoto wangu. Ukweli ananifanya niujutie uamuzi wangu wa kumwoa. Na hakika kama ningejua ndoa yangu ingekuwa hivi, kamwe nisingemuoa na pengine nisingeoa kabisa. Kwa miaka 8 yote nimeishi kwa kuvumilia tu lakini kero mtindo mmoja. Mwanamke mbishi,mwenye dharau, mgomvi, mwenye kupenda kushindana, hana shukurani na neno "samahani" ni mwiko kwake. Akikosa badala ya kuomba radhi utamsikia "kwani wewe hukoseagi?" Ni mchokozi, mjuaji na asiye na dogo na asiye na unyeyekevu kabisa. Hapendi tuongozane njiani na wakati mwingine anaanzisha ugomvi au ubishi barabarani. Anakosoa karibu kila ninachokifanya. Mfano nikileta mboga nyumbani utasikia "sasa ndio nyama gani umeleta?" tunapokwaruzana kwa maneno, anataka ninyamaze yeye aseme na awe wa mwisho kusema. Mimi ni mwalimu na yeye ana elimu ya drs la 7 ila ninapowafundisha wanangu nyumbani yeye hujifanya anajua zaidi yangu na kusema nawapotosha watoto akitaka niwafundishe anavyotaka yeye. Mara kadhaa nimewahi kumwambia kuwa asipojirekebisha nitamrudisha kwao lakini hunijibu kwa dharau ati "kwani ulinitoa kwenye mti?" Haya ni kwa uchache tu. Ana kero nyingi, nyingi, nyingi sana. Nimeshawahi kumwita dada yake akatukalisha na akamsema sana mdogo wake lakini alitulia wk 2 tu, kero zikarudi palepale. Japo nimefunga naye ndoa kanisani, hiyo sio kinga dhidi ya kummwaga. Nahofia tu malezi ya wanangu 2: mkubwa yuko drs la I na mdogo chekechea. Ukweli naumia sana na mwanamke harekebishiki. Nifanyeje jamani?
 
nenda kavute thread la lara 1, mwanamke wa ukwee umprintie afu mwekee asome kimyakimya asikuone
 
Nilidhani wenye elimu ndio wenye viburi...pole kaka; hiyo ndio tabia yake jifunze kuizoea; kama ana maneno ya kejeli wewe mpotezee tu...huwezi jua unaweza oa mwenye tabia mara mbili ya hizo.

Nimeshangaa kukataa msiongozane...mkeo ana mvuto sana nini??? Na wewe una kitambi nini??? (natania)

Haya mambo ya kukimbia kuongozana na mwenza yako sana upande wa wanaume...sasa nikiona mke anamkwepa mumewe napata shida saaana kuelewa...ni more likely kuwa anakuona si wa type yake.
 


i missed u
 
pigaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa! Chiniiiii! Acha ubwege! We ticha wa wapi! Watoto ki2 gani bwana hata housegirl wanalea! Au umepewa libwata!!!!!
 
Nzi na ujanja wake wote hatui juu ya kaa la moto. Nadhani kosa namba moja ulilofanya ni kukubali kuishi na mtu asiyejali hisia zako. Tuachane na hilo, kosa lishafanyika na kwa kutambua hilo ndio itatupa namna rahisi ya kupata suluhisho.
1. Je huwa unamsugua kisawasawa na kumridhisha wakati wa kupiga push ups za kiuno?
2. Kuna jambo lolote la fedheha ushawahi kulifanya na likaishia kuiaibisha familia yako au mkeo?
3. Anapokosea huwa unamwelekeza kwa ukarimu au ukali(wanawake wakorofi hupenda sana mashindano).
4. Kalelewa na wazazi wa kumzaa au wa kufikia?

Ushauri
Jaribu kufanya mambo ambayo mlikua mnafanya wakati wa uchumba.
Kama hakuna msaidizi yoyote nyumbani basi tafuta mtu wa kusaidia kazi(wanawake wengi huwa wakichoka, huwaza kwa kutumia medula oblongata)
 

yeye ni bonge kuliko mm japo namzidi umri. Frankly speaking, ikifikia tukaachana, i'll never remarry, ameshanijeruhi psychologically hivi kwamba naogopa naweza pata mwinghne akaniumiza pia
 
yeye ni bonge kuliko mm japo namzidi umri. Frankly speaking, ikifikia tukaachana, i'll never remarry, ameshanijeruhi psychologically hivi kwamba naogopa naweza pata mwinghne akaniumiza pia

Mwanaume chuma cha reli hupaswi kuogopa, hivi we unadhani kuna mwanaume aliyewahi kujeruhiwa na mwanamke zaidi ya Adam(baba wa wanadamu). Pamoja na kurubuniwa na Hawa lakini waliishi pamoja hata miaka mia nane na kenda.
 
ni bonge. Kamoja tu analalamika amechoka.

aah kumbe anakupenda sana huyo. hiyo kuongea kwa dharau ni tabia yake tu. wewe unataka unyenyekewe mwenzio hawezi kunyenyekea, ila anakupenda . sasa ukitaka abadilike labda afe.. afufuke awe mpya. kule shuleni kwako huna wanafunzi wagomvi.. wenye ***** ***** ? mnawafukuzaga shule?

yote unayoyasema hapo yanazoeleka wala si ya kukata tamaa na kumuacha mke wako. hivi angelikuwa ni bosi wako ofisini hashukuru utendaji wako anaongea kwa ukali ungeliacha kazi?. kama mumeishi miaka 8 na hujamzoea mimi ninakuona wewe ndo tatizo, jifunze kuzoea mtu. uanaume wako hauta yeyuka..akisema nyama mbaya wakati anakupikia chakula unakula. watoto anaangalia wewe tatizo iko wapi?. ungesema mkeo mwizi, malaya, mchoyo hapo ningekupa pole, lakini haya unayosema hata pole sikupi. sasa anasema "lione kwanza, kichwa kibaya", lakini miguu anapanua na kiuno anakukatikia. unataka kiroba cha miba?
chukua huu ushauri wagawie na wengine
 

Qn. 1 Yes.
Qn. 2 No
Qn. 3 I always do my best but sababu ya dharau zake huwa ugomvi wowote haupati suluhisho. She never says Sorry.
Qn. 4 Kalelewa na wazazi na wote wawili wako hai.
NB. Wazazi wake wana hali nzuri kiuchumi kuliko wangu. Lakini wakwe zangu wananiheshimu na kunipenda.
 

hatuna msaidizi nyumbani ila nakusudia kumpatia probably next month. Ila pia nakusudia kumwanzishia petty business, currently she's just a house wife.sasa akianza kupata hela yake sijui kama ndio dharau itazidi au vp, i don't know
 
kama ni ndoa ndo imefika kwenye chorus, vumilia mkuu ivyo ndo vijimambo vya ndoa vina muda wake, usitegemee mambo yakawa incredibly smootoooooth wakati wote yashinde majaribu, ukipita phase hiyo hakika utaishi miaka mingi na mkeo...afu we jaribu kujitwist na kucheza na akili yake si ushajua ni bongo lala, cheza na akili yake....mwelekeze akizingua mpotezee ili aone umuhimu wako, kamwe usimwache mkeo utajuta, watoto wanamwitaji mama yao hata kama kibri kimemjaa, si unajua mother is a mother even if is a coolie cart
 

We mpotoshe mwenzio! Yaani hako kamoja amechoka! Anataka ashuke maana anamtia shombo! Mkuu tafakari chukua hatua! Ukiona hivyo kunaye amtiaye kichwa! Yaani mkeo hataki mwongozane! Akili ni nywele na kila myu ana zake!
 

hapo kwenye nyekundu ndio ulipokosea sana kaka
 
Experience yako kaka ime prove wrong watu wenye theory zao humu JF...wanasemaga wenyewe wanawake wanene siyo wakorofi ni wapolee...wanasemaga wanawake wasomi ni jeuri...nadhani hii itawafanya wafute imani zao...tabia has nothing to do with umbo (isipokuwa ufupi. Lol)

ni bonge. Kamoja tu analalamika amechoka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…