JOMAM
JF-Expert Member
- Aug 6, 2012
- 330
- 139
Naamini mko poa,
Watu wengi tunapata matatizo na hatujui sababu ya matatizo tunayoyapata.
Mara nyingi zinaweza kuwepo sababu mbalimbali ila kuna jambo naona liko sana humu na nahisi ni laana tunayoitengeneza au tuliokwisha itengeneza.
Kwanini tunaona sifa kutembea na wake za watu au waume za watu? Naona thread nyingi hapa watu wanajisifu kwa kuvunja nyumba za watu.
Pamekuwepo mikasa mingi ya vifo vinavyotokana na wivu wa mapenzi. Hivi hii damu mbona tunaiona kawaida? Sisemi msizini nitakuwa napoteza muda hapa, ila heshimuni ndoa za watu.
Ndoa ni zaidi ya mahusiano ya sex, kuna malezi ya watoto pale na makuzi mengine.
Hivi unajisikia vipi mtu anapokuja anakwambia huyu si baba yako, na anakuonyesha jamaa uliyekuwa unamchukia ndio baba?
Mwisho, siwazuii msizini ila epukeni kutembea na wake za watu, watoto wa shule na kuandika thread zinazovunja maadili ya jamii.
Muwe na uzinzi mwema. Msisahau ni jukumu letu kuilinda au kuibomoa jamii yetu.