Ndoa za mashoga zazidi kuitesa KKKT | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ndoa za mashoga zazidi kuitesa KKKT

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ngekewa, Dec 31, 2009.

 1. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #1
  Dec 31, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  na Dixon Busagaga, Moshi

  HOFU imeendelea kutanda kwa viongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), ikiwa ni miezi michache baada ya kanisa hilo nchini Sweden kutoa tamko la kupitisha azimio la kubariki ndoa za watu wa jinsia moja.

  Kutokana na hali hiyo, Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini, Dk. Martin Shao, alisema kanisa halipo tayari kushirikiana na baadhi ya makanisa yenye mwelekeo huo kutoka barani Ulaya.

  Akizungumza katika kikao cha dayosisi hiyo kilichoshirikisha wajumbe kutoka mikoa mbalimbali nchini, Dk. Shao alisema bado kanisa linashikilia msimamo wake uliotolewa mwaka 2004 ambao unapinga ushoga na usagaji kwani ni kinyume na maandiko matakatifu.

  Alisema kuanzia Januari mwakani, maaskofu wa kanisa hilo nchini, watakutana ili kujadili jinsi ya kufanya ushirikiano na makanisa ambayo yamekuwa mstari wa mbele kupinga vitendo hivyo.

  Dk. Shao alisema tamko litakalotolewa katika mkutano huo, ndilo litakalotoa suluhisho la kuimarisha amani na utulivu miongoni mwa waamini wa kanisa hilo pamoja na kuzuia fikra potofu kuhusu ndoa hizo.

  “Wapo washirika wetu Marekani kama Sinodi ya Nebraska, hawa tumekuwa tukishirikiana katika masuala mbalimbali na walikuwa wakipinga haya masuala, lakini wameonekana kuzidiwa na wenzao, sasa sisi tunaangalia namna ya kufanya kazi na watu kama hao,” alisema Dk. Shao.

  Hata hivyo, alisema baadhi ya nchi wahisani zimekuwa zikitoa masharti magumu katika suala hilo ambapo baadhi zimetishia kuondoa misaada yao kwa nchi ambazo hazikubalini na masuala hayo.

  “Zipo baadhi ya nchi zinatishia kusitisha kutoa misaada kwa nchi ambazo hazikubaliani na hili swala, lakini niseme hatuwezi kuendeshwa na kutishiwa kunyimwa misaada, tutakutana ili kutoa tamko la pamoja...kuliko kuukabali ushoga ni bora kukosa hiyo misaada na huu ndiyo utakuwa msimamo wetu,” alisema Dk. Shao.

  Alisema kanisa hilo haliwezi kuwa na maaskofu na wachungaji ambao ni mashoga na kwamba katika kikao cha Januari kitatoa zaidi msimamo ili waamini wasiwe na hofu juu ya suala hilo.

  Mwishoni mwa Oktoba, kanisa hilo nchini Sweden, ambalo linaongoza kwa kuwa na waamini wengi, lilitoa tamko la kukubali kubariki ndoa ya watu wa jinsia moja.
   
 2. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #2
  Dec 31, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Kwani hata mungu wao yalimkuta, sioni ajabu.
   
 3. Abunwasi

  Abunwasi JF-Expert Member

  #3
  Dec 31, 2009
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 3,166
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Sodom na gomorah ndiyo imeshatia nanga wanangojea custom na immigration waingie
   
 4. B

  Bull JF-Expert Member

  #4
  Dec 31, 2009
  Joined: Nov 4, 2008
  Messages: 984
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tunasubiri wachungaji wenu mbariki ushoga alafu tuanze kuwatoa vinyesi, kuna mchungaji mmoja Dar natamani sana nimtoe kinyesi. Ghreeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
   
 5. S

  Sideeq JF-Expert Member

  #5
  Dec 31, 2009
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 2,417
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  DR! unamaanisha nini?
   
 6. Babylon

  Babylon JF-Expert Member

  #6
  Jan 1, 2010
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 1,338
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Anajidanganya kwa kusema hayupo tayari kuyakubali hayo ya ndowa za jinsia moja kwani hizo pesa za kuendesha na kujenga hayo makanisa wanazitowa wapi kama si kuomba omaba kwa hao wenye mamuzi kule ulaya na marekani ,hata bado kufuatia kauli za wazungu wanasema kuwa hata jesus asingekuwa na pingamizi na mabadiliko hayo.
   
 7. K

  Kicheche Member

  #7
  Jan 1, 2010
  Joined: Jan 11, 2008
  Messages: 46
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  na ulaaniwe pamoja nao!!
   
Loading...