Ndoa yenye mzozo kila siku, mke ana kasoro

Ndoa yenye mzozo kila siku, mke ana kasoro

Bubu Msemaovyo

JF-Expert Member
Joined
May 9, 2007
Posts
4,189
Reaction score
3,548
Sina nia mbaya ya kuwashambulia wanawake, bali najaribu kukumbusha majukumu ya kila mmoja ndani ya uhusiano huku watu wakitakiwa kufahamu nini maana ya ndoa. Mada hii italenga ukweli, umuhimu na ujuzi anaoweza kuupata mwanamke ili atengeneze ndoa yake na maisha yaendelee mbele.

NDOA NI MPANGO WA NANI?
Kwanza ieleweke kwamba, Mungu alipotangaza ndoa kwa mwanamke na mwanaume hakuchagua kundi! Alimaanisha mwanamke yeyote na mwanaume yeyote wenye akili timamu. Kwa hiyo ndoa ni mpango wa Mungu na si utaratibu wa mwanadamu.

KUSHINDWANA
Kumekuwa na ndoa nyingi zinazovunjika madai yakiwa ‘kushindwana'. Utasikia mke au mume anasema niliachana na mwenzangu, kisa TULISHINDWANA TU! Kwa nini wanandoa washindwane? Ukiwauliza wengi kwa nini mlishindwana? Watajibu tulikuwa hatuelewani ndani ya nyumba. Watu hao ni wale walioapa kuishi katika shida na raha hadi kifo! Wengi wamekuwa wakila hiki kiapo bila kujua maana yake! Wanaongea kwa kukariri.Kuishi kwa shida (tabu) ni pamoja na kushindwana na kutoelewana, kuishi kwa raha ni wakati wa maelewano. Sasa wanandoa wakishafika nyumbani baada ya kufunga ndoa hupenda kuishi kwa raha tu.

MKE NA ITIFAKI YA UONGOZI
Mimi naamini, mke na mume kila mmoja ndani ya ndoa anajua nafasi yake ilipo. Mume anajua yeye ni kiongozi mkuu (kichwa) na mke anajua yeye ni msaidizi, sasa kushindwana kunatokea wapi hadi ndoa ivunjike? Katika safu ya uongozi wa kiserikali kuna itifaki, rais wa nchi naye ana msaidizi wake, kwa Tanzania tunasema makamu wa rais. Haiwezekani hawa wawili wakagombana kwa sababu kila mmoja ana mipaka yake ya kazi na anaijua.

Haiwezekani rais yuko nje ya nchi, makamu akaamua kuteuamawaziri na kuwabadilisha wakuu wa mikoa kwa kadiri apendavyo yeye, hiyo ni kazi ya rais. Lakini ndoa nyingi za leo, kati ya 100, 85 zimevunjika kwa sababu ya migogoro ya kutojua itifaki hii.

Wanawake wengi wamekuwa wakitaka kuwa na nafasi ya urais ili na wao waweze kuchagua wakuu wa mikoa na kubadili mawaziri kwa vile watakavyoona inafaa. Mizozo mingi ndani ya ndoa za leo ni mwanamke kulilia usawa wa kufikia levo yamume kama kichwa! Hivyo kujikuta ndani ya nyumba kunakuwa na marais (viongozi)wawili lakini usukani mmoja! Mh!

USAWA MGUMU
Ziko ndoa, mume anaposema sitaki hiki, mke anasema mimi nataka. Tena wapo wanawake kwa kutojua au kujua na kupuuza wametunga hadi msemo wenye kuwaaibisha wao wenyewe wakisema ‘kama mume ni kichwa cha nyumba, mke ni shingo'maana yao ni kwamba kichwa hakiwezi kugeuka bila shingo.Wamesahau kuwa, ili iitwe shingo lazima kuwe na kichwa ndiyo maana kichwa kikitoka, mwili unaitwa kiwiliwili lakini kichwa kikiwa pembeni ya kiwiliwili kinaendelea kuitwa kichwa.

MANENO YENYE HEKIMA WAMWANAMKE
Yupo dada yangu wa hiyari anaitwa Mary aliwahi kuniambia maneno ambayo sikuamini kama yalitoka kichwani mwake au alimsikia mtu, alisema: "Mimi mpaka mwanaume wangu anipige nitakuwa nimejibizana naye nini? Kama akinijia juu kwa maneno makalinitatulia, baadaye akiwa amepunguza hasira nitakaa naye kwa upole na kuongea naye vizuri, ataelewa tu.

Sasa utakuta mwanamke mwingine, mume anasema yeye anasema, tena yeye kwa sauti ya juu, basi ndani ya nyumba ni kelele tu. "Ukiona hivyo, mke ni tatizo! Kujibizana na mume ndani ya nyumba ni kukosa heshima kwani mume ni kiongozi, huwezi kujibizana na kiongozi wako ndiyo maana Mungu alisema mke mwema hutoka kwake lakini hajasema popote kuhusu mume mwema anakotokea.

"NI KWELI WANAWAKE WAKO KATIKA MPANGO MWINGINE WA KUPINGA MAAGIZO YA MUNGU?
 
kweli mwanamke huivunja ndoa yake kwa mikono yake mwenyewe,umenikumbusha kitu.
Kuna dada mmoja ilikuwa kila akileta dada wa kazi kwake lazima mumewe ampitie,akijua tu anamfukuza analeta mwingine,wengine wamekuwa wakiondoka na ujauzito,tukawa tunamuonea huruma bila kujua tatizo halisi,sasa juzi juzi ndio tukaja kujua kumbe bi dada hafanyi kazi yoyote kwake,dada wa kazi ndio wa kuandaa chakula cha mumewe,amfulie na kumnyooshea mumewe,adeki chumba chao,atandike kitanda chao,kufua mashuka yao,yani nili freeze ghafla na huruma niliyokuwa namuonea ikayeyuka
 
yaap sis wadada tunajisahau hamna mwanume asiyependa kuheshimiwa. ila nyie wanaume siku hizi hamtimizi wajibu wenu kwenye ndoa majukumu yote mna waachia wake zenu wanahangaika mnakula bata tu. halafu utegemee atakuheshimu hebu mke behave kama mama halafu mme behave kama baba uone jinsi mambo yatakuwa mazur
 
umetoa nondo za kutosha mwenye macho na ajifunze hapa...hasa wanandoa wapya-wapya
 
kweli wengi wa wanawake kichwani wamejaza mavi wakienda chooni wanakunya ubongo
 
kweli mwanamke huivunja ndoa yake kwa mikono yake mwenyewe,umenikumbusha kitu.
Kuna dada mmoja ilikuwa kila akileta dada wa kazi kwake lazima mumewe ampitie,akijua tu anamfukuza analeta mwingine,wengine wamekuwa wakiondoka na ujauzito,tukawa tunamuonea huruma bila kujua tatizo halisi,sasa juzi juzi ndio tukaja kujua kumbe bi dada hafanyi kazi yoyote kwake,dada wa kazi ndio wa kuandaa chakula cha mumewe,amfulie na kumnyooshea mumewe,adeki chumba chao,atandike kitanda chao,kufua mashuka yao,yani nili freeze ghafla na huruma niliyokuwa namuonea ikayeyuka
lin
naomba niongezee hapo sio mwanamke...ni mwanamke mpumbavu
 
  • Thanks
Reactions: lin
kweli mwanamke huivunja ndoa yake kwa mikono yake mwenyewe,umenikumbusha kitu.
Kuna dada mmoja ilikuwa kila akileta dada wa kazi kwake lazima mumewe ampitie,akijua tu anamfukuza analeta mwingine,wengine wamekuwa wakiondoka na ujauzito,tukawa tunamuonea huruma bila kujua tatizo halisi,sasa juzi juzi ndio tukaja kujua kumbe bi dada hafanyi kazi yoyote kwake,dada wa kazi ndio wa kuandaa chakula cha mumewe,amfulie na kumnyooshea mumewe,adeki chumba chao,atandike kitanda chao,kufua mashuka yao,yani nili freeze ghafla na huruma niliyokuwa namuonea ikayeyuka
Nasikitika mwanamke mwenzetu umetoa hii comment! Mwanamke kuwa mtumwa wa mume umasikini tu! Watu wana maisha yao, wanahudumiwa, wanapikiwa na cheff, watoto wanalelewa na nurse, usafi unafanywa na kampuni ya cleanes NA WAUME ZAO HAWACHEPUKI,!! Huyo baba msengerema, na mkewe msengerema vile vile kwa kumvumilia! Msiwe mnasapoti upuuzi katika jamii! So kama hafanyi kazi ni halali huyo baba asiheshimu commitment yake sababu mkewe anajipumzisha kidogo? Nyoooo!
Malezi mabovu tu! Mimi mama yangu hana mtoto wa kiume au wa kike! Kupika zamu, kuosha vyombo wataosha, kufagia, sufuria wanasugua tena nje, nguo wanafua, deki wanapiga, na ole wao walipue! Mpaka leo watu wazima wana treat wake zao vizuri!

Mmoja mke akaondoka na beki tatu kamuachia watoto, anawapikia fresh, anawaanda shule fresh, deki anapiga, na kazini anaenda! Weekend anawatoa out, wala hamna neno kabisaa! Kazi gani imshinde ndani? Thubutuuuuuuuu! Mkewe kupelelezza akajua wanaishi fresh akajirudisha mwenyewe! Watoto wakamwambia mama usingerudi tunataka kukaa na baba peke yetu!
 
Back
Top Bottom