Ndoa yavunjika dakika chache kabla ya kufungwa

Ndoa yavunjika dakika chache kabla ya kufungwa

Bujibuji Simba Nyamaume

Platinum Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
78,439
Reaction score
166,897
AIBU:- NDOA YASAMBARATIKA KANISANI DAKIKA CHACHE KABLA YA KUIDHINISHWA.....



1.png


Hili ni tukio la kusikitisha, lakini lenye mafunzo kibao ndani yake.Tukio hilo lilitoke mwanzoni mwa mwezi wa nane mwaka huu ndani ya kanisa la Pentekoste la nchini Kenya ambapo wanandoa wawili walikuwa wakila kiapo cha maisha mbele ya mchungaji wa kanisa hilo.



Dakika chache kabla ya wanandoa hao kuapishwa na kuruhusiwa kuvishana pete, Mchungaji wa kanisa hilo aliwauliza waumini kama kuna yeyote mwenye pingamizi la kufungwa kwa ndoa ya wapenzi hao...

Baada ya swali hilo, mwanamke mmoja alisimama na kuelekea mbele ya kanisa hilo huku akiwa na vyeti mkononi.

Alipomkaribia mchungaji, mwanamke huyo alipaaza sauti yake na kusema kuwa ndoa hiyo haistahili kufungwa kwa sababu yeye na bwana harusi wanamtoto waliyemzaa pamoja na kwamba walikuwa na mipango ya kuoana....

Kilichoendelea baada ya hapo ni VITUKO


TAZAMA VIDEO HAPO CHINI UJIONEE



[video]www.youtube.com/embed/KS1_1X6Pxt4?[/video]
 
Ntaangali vdeo bdaye.lakini kwanini ihairishwe wakati huyo mwanamke walikuwa wanamipango tu ya kuoana na hawakuwa wameoana ama cjaelewa?
 
Ntaangali vdeo bdaye.lakini kwanini ihairishwe wakati huyo mwanamke walikuwa wanamipango tu ya kuoana na hawakuwa wameoana ama cjaelewa?

ipitishwe tu na huku maana mtu anazaa na wanawake wawili mathalani halafu huyooooo anaoa mwingine tofauti na hao bado akiwa ndani ya ndoa anazaa tena nje!!!!

Ingekuwa ukizaa tu huyo ndo mkeo
 
Ntaangali vdeo bdaye.lakini kwanini ihairishwe wakati huyo mwanamke walikuwa wanamipango tu ya kuoana na hawakuwa wameoana ama cjaelewa?

nafikiri hao wachumba hawakuwa na nia ya dhati ya kufunga ndoa. Mahusiano ya kabla ya ndoa na mipango kedekede kwa wenza wengine haiwezi kusababisha ndoa isifungwe.
 
KILICHOVUNJWA SIO NDOA NI UCHUMBA; NDOA NINI?
Ngoja niweke udambwi-udambwi hapa!
Mkuu hata muishi pamoja miaka 40+ HIYO SIO NDOA!
Ndoa ni lazima ifungwe kisheria!
Kidini, tamaduni or kiserikali!
....
Kunakitu kinaitwa PRESUMPTION OF MARRIAGE (Sec.. 166 The law of Marriage Act of 1971):
Prsmpt of mrg ni dhana ya ndoa, ya kuishi pamoja m/me na m/ke kwa muda wa miaka 2 na kuendelea!
just ni presumption kama inavyojieleza! Ukikamilika tu ushahidi kama Hakuna misingi ya ndoa iliyofatwa, hiyo presumption inakua rebutable (+enye kupingika)
...
Hii presumption inasaidia nini sasa?
Hii inasaidia tu, kutoa haki kwa ke or me kutokana na KUTELEKEZANA! Hapa haiwekani uishi na karembo ukigegede weeeee more than 2 yrs, hadi ukafanye matege katoto ka watu, hadi nyonye liwe soksi, hadi nyonya na kiuno vichanganyike pamoja! Eti useme haumtaki! Ukimuacha wewe achukuliwe na nani? Hapa ni lazima utoe mantanance kwa mwenzio + watoto (kama wapo)
....
Sio ndoa coz huwezi kumshtaki m/me or m/ke kwa kuzini na Mpenzi wako! Hakuna fidia yoyote utalipwa hapa!
...
Nadhani umenisoma hapa!
 
sio sawa kabisa basi huyo mdada anatakiwa alipe gharama zote za harus
 
huyu mama mbona siku zote hakwenda kuweka pingamizi mpaka asubiri siku ya kufunga ndoa?
 
nafikiri hao wachumba hawakuwa na nia ya dhati ya kufunga ndoa. Mahusiano ya kabla ya ndoa na mipango kedekede kwa wenza wengine haiwezi kusababisha ndoa isifungwe.

ndio hapo sasa huyo mwanamke cdhani kama alifanya fair angependwa yeye c angeolewa?wivu tu ulikuwa unamsumbua
 
ipitishwe tu na huku maana mtu anazaa na wanawake wawili mathalani halafu huyooooo anaoa mwingine tofauti na hao bado akiwa ndani ya ndoa anazaa tena nje!!!!

Ingekuwa ukizaa tu huyo ndo mkeo

hahaaa kuna watu wana balaa sana....
 
Sasa kama ndo hvyo alievaa shela avue ampe huyo anaestahili kuolewa hapo kelele ziishe jamani watu wanachotaka hapo ni pilau bhaana au..........


Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Lakini hii ni project, yule dada anayeolewa ndio anaonekana ni mastermind. Amekula vitu vya jamaa + mahari then akamwandaa yule dada aje kuvamia wakati ndoa inafungwa. Huyo dada ndani ya shela wala hampendi jamaa alitaka tu ale vitu vyake, na movie ndio imeishia hapo. Hata kama jamaa ajifanye kumwoa dada atakuja kumwacha kwa kisingizio kwamba hajatulia.
 
Back
Top Bottom