nimesoma minazi mirefu banana, nikasoma juhudi seco. tukiwa na kina niki mbishi. nimefanya kazi aviation hapo banana. kwa sasa nipo mkoani mbeya. nilikitana na mke wangu tukiwa ofic moja ya bro. wangu. nilimfundisha kazi, akawa mjuzi sana yy alikua secretary. baada ya hapo tukapanga kuoana na ni mm nilitoa bikra, nikapeleka posa kwao. nikaoa akawa wife. cku tunahamia katika nyumba ya kupanga iliyopo g/mboto ndio mabomu yalilipuka. maisha yakaendelea nikawa nafanya biashara ya cm nanunia cm dar nasafirisha mikoani. baadae nikakamatwa nikataifishwa mali zangu. hapo ndipo dunia ikawa chungu. nikafungu ofic yangu ya stationary, sasa bwana wife akaanza tabi ya
kupigiwa cm ucku nikimuuliza ananiambia rafiki, rafiki gani wa kiume anakupigia cm mke wa mtu saa cta ucku?
hapo haikutosha akaanza tabia ya kurud hme saa saba mar saa tano ucku.kuna cku alirudi saa saba nikaona usenge huu, nikaanza kumpa kibano c ndio msg ikaingi kwa jina la Ambloc anayeishi tegeta, hapo hacra ikazidi. maana msg ilikua inase
a hv. ucku mwema mpenz leo umenifurahisha.
AKAPIGA CM KWA NDUGU ZAKE
baada ya kichapo akapiga cm kwa dada zake na kuwaambia nimempiga bila kosa. hao shemeji zangu c kwanivutia uzi na kuniporomoshea matuc, inampiga mdogo wetu kwa mahali gani uliyo toa, ukiangalia wawo hawajaolewa, hatimaye wakamjaza ujinga.
kesho yake narudi toka job nakita kabeba pesa zote zilizokuwepo home. hapo ndipo nilizimia kwa mara ya kwanza na kutaka kujiua. akaenda kwao kaka kama wiki mbili zen akarudi kwangu. lakini nilikataa kumpokea ikabidi tukutane ndugu wa pande mbili tukazungumza hatimaye akarudi kwangu
MIEZI 3 BADAE
Akarudia tabia akarudi saa8 ucku. kumbe aliletwa na bwana mwingine anayekaa njia panda segerea, cki hiyo nikampa kipigo tena.
ASUBUHI KAPIGA CM KWA MZEE WANGU
asubuhi akapiga cm kwa mshua na kutaka suruhisho la kivunja ndoa yetu, kumbuka alikua na mimba yangu ya miezi2 japo aliamua kuitoa. wazee wakaja wakamuuliza baada ya kuachana anataka nini kutoka kwangu? akachagua vitu vyote. wazazi wangu wakanishauri nimpe kila kitu. ikabidi nitoke mm ktk nyumba kama vle mm ndiye mwanamke nimepewa taraka. nikarudi kuanza upya maisha kwa mzee wangu nikiwa na mabegi yangu.
Baada ya mwaka nikaoa
nikafanya biashara ndogo ndogo, nikapata mtaji wa kutosha, nikanunua gari nikiwa na huyu mke wa pili. sasa kackia nimefanikiwa akaanza tena fujo kutaka kuvunja ndoa ya sasa, ikanibidi nihame dar na kuhamia mbeya. lakini hachoki kunisumbua. hiyo ndio ndoa yangu