Nimewahi kusikia juu ya utafiti fulani (sijui unaitwaje na wa mwaka gani) ila nilisikia katika chombo kimojawapo cha habri kinachoheshimika katika mataifa kadhaa kwamba ndoa kutengamaa (kwa maana ya mke na mume kuondoka katika misuguano na misukosuko) inachukua hadi miaka 7!
Nikajaribu kuitathmini ya kwamngu yenye umri angalau miaka 17 sasa na watoto kadhaa nikabaini ukweli wa kiasi kikubwa maana mwanzoni mawimbi yanakuwa mengi mmno.
Kwa hivyo dada hongera sana kwa kuurejesha uimara wa ndoa yako katika mstari, muombe MUNGU kama research hiyo ni ya kweli inaonesha unakaribia sana ku-graduate.....