Ndoa ya Mkeka inatambulika kisheria?

TANZANNIA

JF-Expert Member
Sep 29, 2015
1,047
384
Sina uhakika vizuri kama ndoa hii ni aina mojawapo ya ndoa zinazotambulika kisheria, aina ninazozikumbuka ni ndoa za jadi, dini na serikali.

Kwa wenye weledi please naomba msaada wenu
 
hii inatakiwa iende jukwaa la sheria
sina uhakika vizuri kama ndoa hii ni aina mojawapo ya ndoa zinazotambulika kisheria,aina ninazozikumbuka ni ndoa za jadi,dini na serikali.kwa wenye weledi please naomba msaada wenu
 
mkuu hapo tutaangalia sasa hiyo ndoa ya mkeka utafungwa kwa mujibu wa muundo upi au mrengo upi...kushikwa ugoni hakumaanishi kuwa hakutofuatwa misingi flani ya ufungishaji ndoa...sasa hapa itategemea kama waliokamatiwa ni waislamu basi sheikh ataitwa na ndoa itafungwa kwa mujibu wa dini hiyo,kama wahusika ni wakabila fulani tena wamekamatiwa katika sehemu ambayo mila katika ufungishaji ndoa ndo zinafuatwa,basi ndoa itafungwa kimila,na vivo hivyo iwapo waliokamatiwa watakuwa ni wadini tofauti basi Wilaya/bomani itawahusu kwa mujibu wa sheria za nchi.
Haina maana ukishakamatiwa/kushikwa ugoni eti ndo taratibu za kawaida za ufungishaji ndoa hazifuatwi.
 
Ndoa ya mkeka ndio kitu gani usiwe mtu mwenye kukariri dini nisheria hakika dini haitaki ujanja ujanja sasa nakujibu ndoa ni ndoa ipite katika misingi ya kisheria ya dini ok.
 
Mkuu ushaambiwa kuishi tu na mwanamke zaidi ya miezi 6 kama sikosei
Tayari ana haki zote na mahakama inaweza kumtambua kama mkeo halali kabisa.
Sasa ya mkeka si ndoa tayari? labda iwe haijafikisha miezi sita utapona kama sheria haiitambui
 
mkuu hakuna sheria ya kukaa na mtu kama mume au mke kwa muda wa miezi sita(6),halafu hiyo ikawa ni ndoa inayotambulika kisheria,bali ni Miaka miwili(2)ndo presumption of marriage inakuwa applicable.
 
Okay okay asante kwa kuweka kumbukumbu sawa...!
 
mkuu hapo tutaangalia sasa hiyo ndoa ya mkeka utafungwa kwa mujibu wa muundo upi au mrengo upi...kushikwa ugoni hakumaanishi kuwa hakutofuatwa misingi flani ya ufungishaji ndoa...sasa hapa itategemea kama waliokamatiwa ni waislamu basi sheikh ataitwa na ndoa itafungwa kwa mujibu wa dini hiyo,kama wahusika ni wakabila fulani tena wamekamatiwa katika sehemu ambayo mila katika ufungishaji ndoa ndo zinafuatwa,basi ndoa itafungwa kimila,na vivo hivyo iwapo waliokamatiwa watakuwa ni wadini tofauti basi Wilaya/bomani itawahusu kwa mujibu wa sheria za nchi.
Haina maana ukishakamatiwa/kushikwa ugoni eti ndo taratibu za kawaida za ufungishaji ndoa hazifuatwi.
kama ni waislamu hakuna ndoa ya wazinifu
 
Back
Top Bottom