Ndoa ya mkataba

ankol

JF-Expert Member
Aug 21, 2012
2,105
3,475
Habari wanaJF.
Muda mwingine nafikiriaga sana kutokana na matatizo mengi ya wana ndoa hasa pale wanapozoeana na kusababisha mabalaa kila uchao.
Hivi Nchi yetu ingeruhusu ndoa za mikataba mfano renewable kila baada ya miaka miwili au zaidi, unafikiri isingesaidia kuondoa haya mabalaa ya wanandoa?
Mabalaa mengi ya wanandoa likiwemo la michepuko linasababishwa kwa asilimia kubwa kuchokana katika mahusiano na kwa vile ushajifunga pingu ya maisha unakuwa hauna njia nyingine.
Mimi naona kila mtu angejitahidi kuwa makini ili mkataba ukiisha aweze kufikiriwa kuongezewa. Chukua mfano ukifaNYA Kazi za mkataba, asee utakua pankcho mpaka basi kwa kuhofia labda mkataba ukiisha hutoweza pewa mkataba mpya.
Pia itaongeza heshima kwani kila mmoja atamheshimu mwenzake kuchunga mkataba huo.
Maradhi ya kuambukiza ie HIV pia yatapungua.
Hata ikitokea ikionekana umeingia chaka katika kutafuta mwenzi wako hutopata taabu saana utasubiri ile grace period iishe then utaachana nae kutafuta unayeendana nae.
Wewe unasemaje kuhusu hili mdau?
 
Mmmmh uzinzi tuu kwa maana hakuna kipya utakachopata hat kwa kuoa kila siku
 
Ndoa yako ndo ina mabalaa huku pengine ni amani na mapenzi kwa kwenda mbele....
 
Back
Top Bottom