1974hrs
JF-Expert Member
- Oct 27, 2014
- 741
- 536
WanaJF,
Nimetulia na kuamua kuleta kwenu uzi huu ili mnisaidie ushauri!Miaka ya 2002 nilikuwa na uhusiano na binti mmoja ila bahati mbaya tulipoteana kipindi kirefu sana takribanii miaka 10.
Mwaka 2012 nikapata mchumba nikaamua kuoa na tumejaliwa kupata mtoto, sasa ghafla mwaka huo baada ya kuoa tu yule tuliepoteana akaibuka, kwa kuwa sikuwa nimeachana nae kwa shari tulianza mawasiliano ya kawaida pia nikidhani alishaolewa.
Siku nilipokutana nae nikampeleka nyumbani kwetu kumuonyesha tu kwa ndugu kwasababu walikuwa wanajua kuhusu kupoteana kwetu.Sasa baada ya kuonana na dada yangu wamekuwa marafiki kiasi cha uhusiano wake na mke niliye nae umekuwa mbaya sana.
Na mbaya zaidi amemshawishi mpaka mzazi wangu ananilazimisha nioe mke wa pili mpaka imefikia hatua baba yangu tuliyependana sana sasa ananichukia mpaka anasema 'nikiondoka duniani hujamuoa huyu binti siko radhi nawe 'hili linanivuruga akili yangu.
Imefika hatua hata mke wangu hatakiwi na ndugu zangu ila mimi tu ndiye najua umuhimu wake! Naombeni msaada ili nipate uhusiano mzuri na mzazi bila kuathiri ndoa yangu. Kisa ni kuwa mke niliye nae ni masikini na huyo Mwarabu ni mtu mwenye maisha flani hivi.
Mpaka sasa naandika nimefikiria sana mpaka brain imestack
Msaada please nini nifanye na amani iwepo pande zote?
With regard