Ndoa ya kulazimishwa yageuka tamu na yenye baraka

Dr Restart

JF-Expert Member
Jul 15, 2021
3,290
17,100
Wasalaam wana MMU.

Nyuzi kuhusu ndoa kuwa ni chungu, yenye mateso zimekuwa ni nyingi sana humu jukwaani.

Leo nimeona nitoe ushuhuda wa maisha yangu ya ndoa ndani ya miaka 14. Kwangu mimi ndoa imekuwa ni baraka sana na yenye furaha.

Natoka katika jamii ambayo elimu haikuwa kipaumbele kabisa. Hata mimi nilisoma tu kuepusha dhahma ya mzee kuswekwa ndani kwa kutokuwa na mtoto anayesoma. Ikabidi anisukumizie huko.

Nilipokuwa kijana wa miaka 22, kipindi hicho nasoma Chuo mwaka wa kwanza, mzazi wangu alinitaarifu kuwa mchumba wangu sasa amekuwa. Na mambo yote yamemalizika. Ni muda tu wa kusubiri nirejee likizo kwa ajili ya kwenda kumleta rasmi kama mke.

Kutokana na kaelimu nilikokapata, nilikataa kata na kupishana na maelekezo ya mzee kuwa sipo tayari kuoa kwa sasa tena kwa mchumba wa kuchaguliwa.

Ukweli ni kuwa, hata mchumba mwenyewe sikuwa namjua hata kwa jina potelea mbali sura. Baba yake nimemsikia tu lakini kamwe sijawahi kumuona.
Binti mwenyewe alikuwa na miaka 14 tu kwa wakati huo.

Kwa hiyo nilijitetea kuwa binti ni mdogo, nipo busy na masomo lakini pia sikuwa tayari kumuoa binti ambaye simjui wala sijampenda.

Mzazi wangu aliniambia, chagua lililobaki ni moja tu. Hakuna lingine, ni kukubali tu kumuoa binti.

Kwa kudiriki kwenda kinyume na maelekezo ya Mzee, niliacha kurudi nyumbani kwa likizo husika. Uzuri ni kuwa hata ada nilikuwa sipategemei nyumbani. Kuna shirika lilijitolea kunifadhili kwa kila kitu kwenye masomo yangu.
Hivyo, jeuri ya kutorudi nyumbani nilikuwa nayo.

Mwaka wa pili ukasonga, nilipata mwanamke ambaye hakika nilimpenda na kujitabiria ya kuwa atakuwa mke wangu bila shaka. Lakini, Mungu anapanga yake.

Tukaendelea kwenye mahusiano huku tukipeana ahadi kedekede kuwa tutaoana punde baada ya kumaliza masomo yetu.

Kipindi hiki ndicho sikutaka kabisa kusikia habari za nyumbani, kwa kuwa kila nikiwasiliana na mzee hunikumbusha juu ya habari za kuoa.

Mwaka wa pili, mwishoni nikawasiliana na mama. Aliyoniambia yaliniacha na butwaa!. Siku chache zijazo wataenda ukweni kumleta binti.

Mzee kakomalia, iwe isiwe binti atakuwa mke wangu. Na kweli, walienda kwa wakakabidhiwa binti wakaja naye.

Sherehe ndogo ilifanyika kumtambulisha binti nyumbani maisha yakaendelea.

Mimi na mwenzi wangu tuliendelea pia kufarijiana. Hatimaye mwaka wa tatu namaliza, namwacha mpenzi wangu akiwa anaingia wa tatu. Sijawahi kukanyaga nyumbani.

Katika watu wenye bahati, najihesabu baina yao. Nilipomaliza tu Chuo, haikuchukua hata wiki mbili. Tayari nilishapata mahali pa kujishikiza. Alhamdulillah, malipo hayakuwa mabaya kwa kianzio.

Matokeo yakatoka na miezi mitano baadae napewa mkataba lakini kwa kuhamishiwa kituo kwenda mkoa wa nyumbani.

Sikuwa na kupinga ila tu mawazo ya kule nyumbani. Mawasiliano ya Mzee yalishakufa rasmi tangu aliponiambia binti ni lazima awe mke wangu. Mara moja moja nilikuwa nikiwasiliana na mama, na kila mara alitaka walau nisalimiane na mke wangu. Wala sikutaka kupoteza muda, hapo hapo ndiyo huwa mwisho wa maongezi.

Hakuna hata nyumbani ambaye alifahamu kuwa nimepata kazi na nimehamishiwa karibu na nyumbani. Muda mwingi nipo busy ofisini, nikitoka narudi nyumbani kupumzika. Sina muda wa kuzurura. Sikupenda kukutana hata kwa ajali na watu wa maeneo ya nyumbani.

Niliendelea kuwasiliana na mpenzi wangu na alikuja nilipokuwa nikiishi. Maisha yalikuwa poa tu.

Kutokana na kuwa huru muda mwingi baada ya kutoka kazini, nilipata nafasi ya kuangalia movie, kujisomea Biblia. Maisha yake yalirutubisha mahusiano yangu na Mungu.

Nikimuimba yeye anionyeshe njia sahihi. Ajabu ni kuwa, kila nilipokuwa nikiomba kuna nguvu ya ajabu ikitaka niwasikilize wazazi. Sauti ile ilikuwa ikinirejea mara kwa mara.

Nitaendelea!
Sehemu ya Pili, soma hapa 👇
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom