Ndoa ya dini 2 ipi ilio sahihi.......

mahirtwahir

JF-Expert Member
Jan 12, 2013
595
500
Salamu ukumbini, nimerudi wamalenga
Nauliza uwanjani, majawabu sitopinga
Yametokea mjini, msiniifanye mjinga
Dini mbili harusini, ndoa gani tutafunga

Moja ya kuumeni, dini njema imefunga
Kijana ana imani, muislamu kajijenga
Lakini mashakani, mchumba alompanga
Nisharti kanisani, ndoa kwenda funga

Mapenzi yalozaini, hatoweza kujikinga
Yamezama akilini, sukari aita mchanga
Tena ameshabaini, kwa dhana alojenga
Bila yeye kanisani, mapadri wataipinga

Mapenzi ya majinuni, ambayo yamejitenga
Yamesibu na kukeni, mahaba yameviringa
Wako tayari jamani, msikitini kwenda funga
Alovinjari shekhani, kafiri anampinga

Nami niko hatarini, tahadharini malenga
Mnijibu kwa makini, hoja zenu kuzipanga
Jukumu langu idhini, ambayo nnaichunga
Itoke kwamisheni, ndoa njema kuifunga

Lapili haki yanani, kwa dini imenifunga
Naye mwanadani, kaja nawake mnyanga
Atakavyo karibuni, ujanani kujitenga
Kaja na hoja nyingi, zimeleta majanga

Asema yumo hakini, kwa hoja alozojenga
Tafauti hajabaini, mapenzi yamemfunga
Nimpe mume yakini, mchumba nisompinga
Jambo la walakini, makanisa anajenga
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom