Kifupi jamaa ana mke na wana miaka 9 hawajapata mtoto, ndipo jamaa kaonelea asije akaondoka duniani bila kopy yake ndo akafanya mpango wa kuzaa na binti mmoja na uzur wana watotot wawil.
Shida ni kua mke kambana wala hawataki watoto wa jamaa hataki kuwasikia na huyo alozaa nae hataki kumwona wala kumsikia.
Jamaa ni muislam na mama watoto wake ni mkristo.
Je, wapendwa mliojaliwa busara tunaomba ushauri wa hili. Huyu mama ambae hakubahatika kuzaa anapaswa afanyaje na yule aliyezalishwa afanyaje? Asanteni sana.