kuoa lazima ni hitaji la kila mwanadamu unaweza ukabishaaaa weeee but iko siku tu utaoa na kutulia cha msingi usichoke kuwa na mawasiliano naye inakuwa rahisi sana kurekebisha tatizo mapema linapoanza tu kujitokeza. maana sisi ni binadamu sasa yeye akinuna ukiona hivyo lazima kuna jambo lako limemkwaza na kuzungumza anashindwa inabidi atumie lugha ya vitendo. so kuwa makini kusoma lugha yake ya vitendo na mzungumze haraka muwezavyo na siyo na wewe unaamuwa kununa haitosaidia. benteke
Hahahaa benteke ni mapema sana kutoa tathimini ya ndoa kwa sasa, anyway hapo bado unaonjeshwa utamu subiri baada ya miaka mitatu uje utuletee thread km hii ya leo.
akinuna wiki moja wewe unaongeza zako mbili akuu heshima iwepo
Hahahaa benteke ni mapema sana kutoa tathimini ya ndoa kwa sasa, anyway hapo bado unaonjeshwa utamu subiri baada ya miaka mitatu uje utuletee thread km hii ya leo.
mkuu hamna jinsi..nimeona niowe tu..liwalo na liwe.
mimi nimejiandaa kila mwaka na diary ya kazi za kawaida ya mume wangu ... akifanya jambo nankuuuu mazuri na mabaya.. yale mazuri nayaulizia akikataaa nalianzisha timbiri mpaka akome 😡
Hongera kwa kuamua kutulia.
Kuhusu whether hizo "hubby hivi, hubby vile" zitaendelea au la,wewe ndio mwamuzi mkuu.Kuwa mume mwema na wema wako utalipa, tumia hekima na busara kutatua matatizo yenu na sio mabavu ili upendo uzidi kuishi kati yenu. Zaidi ya hapo, tegemea majanga huko mbele.
Ni kweli mkuu. Na pia nimegundua life after marriage is not the same..Nikwambie,ni taasisi ambayo ina changamoto nyingi sana,hutakiwi kukata tamaa na kila mtu ana formula yake ya kuhandle ndoa yake,usijekujaribu kutaka kuishi kwa kuangalia ndoa ya mwenzio utafell mapema,kila ndoa ina formula yake,mtu asikudanganye hatufanani katika kuhandle ndoa,mwombe Mungu akupe mwongozo katika ndoa yako changa.
Hahaha..sijisifii hata mama na dada zangu walisema mwanamke nitakayemuoa atakua na raha sana...sijui kununa mimi...pia ni mcheshi sana.. hata wife ananiambia kuwa amepata bahati sana kuolewa na mimi maana mda wote tukiwa pamoja tunacheka.
Hongera sana kwa kuwa ni uamuzi mzuri. Life is how you make it. Ukiamua maisha yako ya ndoa yawe ya furaha itakuwa hivyo, ukiamua yawe machungu itakuwa hivyo. Wewe unatakiwa uplay role kubwa ingawa mke pia anatakiwa ashiriki kwa nafasi yake katika kuimarisha furaha katika ndoa.
Angalizo: Sikiliza single ya marehemu TX moshi (OTU JAZZ, Ndoa - ndoano!
Dah ukiona mwanaume amekoma hilo timbwili linakuwa sio la kitoto, ila angalia utoke mangeu