Ndoa zina changamoto nyingi mno. Niwape hadithi moja tuliyosumuliwa na padri kanisani siku moja juu ya familia moja iliyoonekana mfano bora kwa jinsi walivyokuwa wakienda kanisani pamoja. Siku moja aliwaona wanandoa hao wakifika kanisani pamoja kwa gari yao ndogo, baba akashuka, akazunguka gari upande wa abiria na kumfungulia mkewe mlango. Kisha wakaingia kanisani na kukaa benchi moja. Kwa kuwa siku hiyo ilikuwa mahuburi ya familia takatifu, padri akaona hii ndiyo familia ya mfano kwa waumini. Wakati wa mahuburi akawaita wale wanandoa mbele, akawaomba wawaeleze waamini siri ya upendo wao kwa jinsi wanavyokaa pamoja wakionekana wamjeaa upendo.
Baba ndiye aliyechukuwa kipaza sauti kueleza siri ya upendo wao, waumini wajifunze, waishi kwa mfano wao, alichokisema yule baba padri alibaki mdomo wazi. Baba akasema; padri, ulivyoniona ninamfungulia mke wangu mlango wa gari ni kwa sababu mlango wa abiria hauwezi kufunguka kwa ndani hadi mtu afungue kwa nje. Na humu kanisani tumekaa pamoja kwa sababu mke wangu anakaa na sadaka hivyo badala ya kusumbuka wakati wa sadaka kumtafuta, tumeona tukae pamoja. Ndoa kwa tunavyoina sisi tuliyo nje inaweza kuwa kama kitanda cha maua ya rose, lakini kwa waliondani ni kitu kingine kabisa! Hata hivyo, vijana tusiogope kuingia katika ndoa, mwanaume na mwanamke, ukiwaacha walioitwa kumtumikia Mungu vinginevyo, hawawezi kuwa watu imara mpaka waingie kwenye ndoa na kuishi kwa mafanikio ndani ya taasisi inaitwa familia. Pia, tukumbuke hakujawahi kuwepo ushahidi, duniani na mbinguni, kwamba kulishawahi kuwepo ndoa ya malaika!.