Ndoa ni ya watu wangapi?

Sibonike

JF-Expert Member
Joined
Dec 23, 2010
Posts
17,297
Reaction score
18,053
Leo uzalendo umenishinda imebidi nilete kwenu wana JF hili suala. Nipo ndani ya ndoa miaka mingi na tumejaliwa binti mkubwa yupo sekondari. Mimi na wife tunashukuru mungu, wote ni graduates na tuna kazi nzuri tu.

Wife kwao wapo watatu yeye ndio wa kati. Kwao ndio msomi pekee huyo dada mtu kamaliza form IV zile ambazo ni kama la saba tu. Division four karibu na zero.

Amekuja kuolewa wakati wadogo zake wana watoto wakubwa na kwa maelezo ya wife mwenyewe mahari alitoa mwenyewe! Katika ndoa au mahusiano mengine mikwaruzo ya hapa na pale ipo lakini tunai solve bila shida. Lakini miaka hii mitatu imekuwa na mtihani sana.

Tatizo nimegundua hamna kitu wife anafanya bila kupata ushauri kwa dada yake. Nimegundua hata sms na email zangu ana zi-forward kwa dada yake. Kubwa yake nimegundua anajenga kisiri na kiranja wa mpango huo ni dada yake.

Tayari nyumba ipo kwenye lenta na nina picha ya kila hatua. Huyo dada mtu hapatani na mdogo wao maana yupo ngangari hakubaliwa kuingiliwa mambo yake na mumewe.

Tofauti na wife, za kuambiwa anachanganya na zake na kama jibu halimpi hakubali. Sasa imefika mahali najiuliza hivi nimeoa wangapi? Ni kama nakula chakula kisicho na ladha yoyote.

Mwisho nimekuwa mteja wa Massage Parlour moja kujiliwaza na sikosi happy ending hapo. Hapo Massage Parlour nimekuwa nikihudumiwa na binti mmoja tu. So far nime resist kuchukua number yake ya simu wala kumpa yangu.

Isingekuwa binti yetu, na jinsi mama mkwe anavyoniheshimu, ningekuwa nimeishamtema siku nyingi. Najiuliza mtihani huu hadi lini?
 
Pole.
Mkeo ameshikiwa akili,inauma ila bado yanaongeleka na kama mkeo hakuwa na nia mbaya ni ushauri mbovu tu wa dada basi mtalivuka hili salama.
Mh! Hako ka bint ka massage parlour hako!!! Kaa nako mbali maana ni kama umeanza kukafikiria kuhuisha furaha iliyokufa ndani yako. Kama ni lazima upate huduma ya massage parlour basi isiwe moja tu kama mboni ya jicho,jaribu kuchanganya leo ikiwa hapa basi next time iwe pale au kule!
Zaidi ya kumtumia dada yake kama mshauri mkuu mpaka kufikia kujenga kwa siri,kuna mapungufu mengine hasa huduma za kinyumba?
Tafuta suluhu kaka,yeye ameshamwaga mboga sasa nawe ukimwaga ugali bint yenu ndio atakayelala na njaa!!!
 
Aisee kabla sijaweka mchango wowote hebu nitupie namba ya simu ya huyu kigoli wako...

Nahitaji mtu wa kunikanda mishipa na misuli baada ya kutoka kwa mkoloni...

Mkuu, wewe jimwage Massage Parlour yoyote wapo wengi hao. Pale utachagua mwenyewe
 
Inategemea na aina ya ndoa. Umasaini mke ni wa ukoo.

Sijajua ndoa yako ni ya aina gani, labda wanakuita 'our husband'.

Mkeo hajiamini tu, ni tatizo lake. Ila mie nigundue mke wangu anajenga bila kunishirikisha?? Siku hiyo hakuna jiwe litabaki juu ya jiwe lenzie, bora kurudi babylon. Yaani umewezaje kukaa nalo unajisukumizwa kwa massage palo? Mahari si ulitoa kabisa?

Afu na wewe, hujaoa heshima ya mama mkwe, umeoa mkeo, act as a man.

Ila kila uhusiano una alfa partner wake, huwa ndio aaendesha show mwingine anafuata.
 

Asante. Nimeongea naye sana kuhusu dada yake lakini natwanga maji kwenye kinu. Hata mdogo wao ananisapoti kwa hilo. Kweli hilo la Massage Parlour nitalifanyia kazi maana mazoea hujenga tabia. Mapungufu ya kinyumba yamekuja baada ya hizo issue za dada yake, kabla ya hapo ilikuwa yeye ndio analalamika apumzimke. Kila nikumuwaza binti yangu, najirudi kumwaga ugali. Na buy time. Binti akiwa mkubwa wa kutosha na bado hali haijaeleweka, nitakuwa sina namna.
 
Inawezekana wewe huna tabia ya kukaa na kupanga mipango ya maisha ya kesho na mkeo, wajanja wamekuwahi na kumpa somo la kujiandaa kwa ajili ya kesho na kazi ndio imepamba moto. Wewe ni kichwa cha nyumba kuwa macho... ukiacha upenyo wowote... wajanja wanatia timu... wanawake wengi wanapenda mume anayeweza kusimamia na kuhimiza mambo ya future... usikae na kushangaa tuuu elewa aliwazalo mkeo.

swali la kizushi... una mtoto 1 tu? kwa nini? isijeikawa ni uzembe wako tuuu wengine watakuongezea watoto!!!! ha ha ha ha
 
Aisee pole mkuu Vuta subira kwani yavuta kheri , but swala la kujenga pembeni mpe makavu hati za mjengo zisome majina yenu wote kwanini ajenge kivyake ????
 

Wala hawapo maskini kihivyo lakini nakubaliana na wewe kuwa ni mtu asiyejiamini tofauti na mdogo wao. Ingekuwa tuna rewind mbona ningechukua mdogo mtu. Full kujiamni. La mama mkwe si issue sana kuliko la binti yangu. Mama mkwe ni uhusiano wa muda mbona. The only thing huwa kila wakati namwambia be yourself
 
Aisee pole mkuu Vuta subira kwani yavuta kheri , but swala la kujenga pembeni mpe makavu hati za mjengo zisome majina yenu wote kwanini ajenge kivyake ????

Mkuu la nyumba nimelifanyia mkakati mzito tu. Sioni sababu ya kuiharibu japo kuna wakati nilitaka kufanya hivyo.
 

Ni ushetani wa dada mtu tu. Mbona tuna vijumba viwili na ya tatu inajengwa japo kwa mwendo wa kobe. Na vyote hivyo tuna plan na kutekeleza wote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…