ndoa ni nini

KIDHEHA

Member
May 21, 2012
51
14
Hi, naombeni wana jf tujuzane katika hili labda litasaidia....maana ya ndoa ni nini na inajengwa na nini ili iweze kudumu? karibu
 
Unauliza ndoa nini au unataka kujua kinachoifanya idumu?Sidhani kama hayo mambo yanahusiana kiufafanuzi!
 
Ndoa ni makubaliano ya watu wawili ya kuishi pamoja kama mke na mume ili kujenga familia. . . . Kinachofanya ndoa idumu ni mambo mengi sana ila lililo la msingi ni kama wanandoa wanamalengo yanayofanana kwenye uhitaji wao kwenye ndoa!
 
Makubaliano ya wawili pasipo kumshirikisha kiongozi wa dini je ni ndoa?@eiya
 
...Ndoa ni muungano kati ya mwanamke na
mwanamume kuishi pamoja kama mume na mke
muda wote wa maisha yao. (Sheria ya ndoa –
mwaka 1971 kifungu cha 9).

i) Wanaooana wawe wamekubaliana pasipo
kulazimishwa na mtu.

ii) Ndoa ni ya mwanamke na mwanamume.

iii) Ni ndoa ya kudumu maishani.

...hapo kwenye KUDUMU naomba niparuke...L.O.L...juhudi binafsi zinahitajika...kama ni kwa MUNGU sana,piga goti...kama ni kwa WAGANGA wa kienyeji...wewe tu na imani yako!
 
upendo
heshima
utii
uaminifu
ni baadhi ya vitu vinavyodumisha ndoa.....kumbuka 'baadhi'.....
 
Hivi we toka umezaliwa na mpa umeanza kutype JF, hujui nini mana ya ndoa.
 
NDOA NI KUTOA
1. Ndio sio mkataba wa kijamii bali agano la kiroho. Waefeso 5:31-33 Kwa sababu hiyo mtu atamwacha baba yake na mama yake, ataambatana na mkewe na hao wawili watakuwa mwili mmoja. Siri hiyo ni kubwa, ila mimi nanena habari ya KRISTO na Kanisa.
Lakini kila mtu ampende mke wake kama nafsi yake mwenyewe, wala mke asikose kumstahi mumewe.
Hapa tunajifunzai) Ndoa ni fumbo la ajabu la kiroho linalowaunganisha watu wawili, mwanamume na mwanamke (mst.31)ii)
Ndoa ya kikristo inaliganishwa na uhusiano uliopo kati ya KRISTO na Kanisa (mst.32)
iii) Mpango wa MUNGU katika ndoa unahitaji upendo wa kujitoa sadaka kama KRISTO anavyofanya kwa Kanisa (mst.33)2. Ndoa ya Kikristo ni kujitoa sio kupokea.
Wafilipi 2:3-4 Msitende neno lolote kwa kushindana wala kwa majivuno, bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenzie kuwa bora kuliko nafsi yake mwenyewe. Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo ya wengine.
Hapa tunajifunza
i) Kutokuwa wabinafsi
ii) Unyenyekevu
iii) Roho ya kutoa na kujitoa.
 
Ndoa ni mwanaume kusaini mkataba,
1:Ndiye atakeye mtunza mwanamke na familia yake,hata kama mwanamke ana mshahara kuliko mwanaume.
2:Ni mwisho kwa mwanaume kusaidia familia yake,na ndugu wa mwanume mwisho kumtembelea mwanaume.
3:Hela ikipungua,penzi litapelekwa kwa mtu mwingine na kila ukifika nyumbani tegemea kununiwa.
 
Back
Top Bottom