Ndoa ni mpango wa mawanaume, ni fursa kwa mwanamke

Youbettersleep

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2019
Posts
944
Reaction score
1,628
Leo hapa kijiweni NYASAKA CENTER. mzee wetu leo kaja na neno la kutuambia vijana kuhusu NDOA.

Ndoa ni mpango mzuri kwa mwanaume na ni fursa kwa MWANAMKE akiwa na maana ya kwamba Mwanaume ili aoe ni lazima awe amependa na ameamua ila MWANAMKE ili aolewe 99% wanaangalia nini atapata kwenye ndoa hiyo, either famia ya MUME inajiweza au Jamaa anajiweza.

Ndio maana wanawake huwashauri watoto wao wa kike kuwakubalia wanaume wenye NACHO na sio MIKONO MITUPU BOY au wale wa INSHALLAH au BWANA ATATENDA.

MZEE WA KIHAYA AKAMALIZA KWA KUSEMA.
"A reason why the ring is put on the left hand is because marriage is not right"

MWISHO.
 
With all the available info on/about marriage kuna wanaume ambao bado wanaoa kwa mapenzi?
 
Ni kweli wanaofaidi kwenye ndoa ni wanawake na sio wanaume
 
Wale ambao mwanamke alimkuta hana kitu akamkubali na wakaanza maisha na wamejipata anawazungumziaje?
 
Hizi Akili sijui huwa mnazitoa wapi??
Ila wanawake hampendi wanaume wakistukia michezo yenu sijui kwann? Sasa huu uovu ina maana hapa wewe haujaelewa hata kimoja alichosema?

Kwamba kuna mwanamke leo hii anaingia kwenye mahusiano kwa dhamira ya kujenga mahusiano na sio kuangalia anapata nini katika huo uhusiano?
 
Wapo wengi mbona!
 
Wale ambao mwanamke alimkuta hana kitu akamkubali na wakaanza maisha na wamejipata anawazungumziaje?
Wachache sana hao siku hizi. Na ukikutana na wa hivyo unakuta ana majanga yake ambayo yanamfanya kuonenaka hana vigezo vya kuwa mke wa mtu.

Aidha ana mtoto au watoto tayari, hana elimu na life lake ni la kuunga unga,anatokea familia ya kipato cha uvunguni,etc

But nadra sana mwanamke mwenye vigezo vyote kujikana awe na mwanaume ambaye ndio kwanza anaanza kujipanga kimaisha.
 
Wapo wengi mbona!
Mbona hawa mnawaona ninyi tu sisi wanaume hatuwaoni wanapatikana taifa gani?

Saa hii mwanamke yoyote anapokutana na kijana anayejitafuta kitu cha kwanza atamuonyesha ni shida zake na kumtaka azitatue halafu ataanza kumuonyesha pia kuwa ana mtu mwingine ambaye atataka huyu mwanaume anaemfukuzia awashindanishe.

Hii si sawa.
 
Labda hapo mjini dar. Tanzania ni kubwa mno boss, tembea kidogo na mikoani huko na vijiji vya Tanganyika uone uhalisia wa maisha.
 
Mbona hawa mnawaona ninyi tu sisi wanaume hatuwaoni wanapatikana taifa gani?
Hapo buguruni inawezekana. Lakini sasa hii nchi ni kubwa mno boss. Hapo Mwanza tu kuna maeneo wapo mabinti wanachuchumaa kidogo wakisalimia mwanaume.
 
Mbona hawa mnawaona ninyi tu sisi wanaume hatuwaoni wanapatikana taifa gani?
Kuna jamaa yeye sifa yake kuu Kwa mwanamke Ni ngozi ya kuteleza,haangalii trako wala sura!
Sasa mwanaume kama huyu kukutana na mizinga mizito Ni lazima,na akishapigwa huko anaanza kusema wanawake Namna gani vipi!
Angalia mwanamke ambae una uwezo nae!
Mbona kuna wanawake ukiwapa 20,000 tu kamaliza mahitaji yake!
 
Wapo ukiwaachia 10,000 kwa siku ukirudi jioni unaoshwa hadi miguu kukuondoa uchovu.
 
ndoa ni utapeli kama utapeli mwingine tu
 
Na siku huna anakuelewa!
Vijana wanapaswa kuwa na wenza wenye malengo wanayoyamudu kinyume na hapo ni kupigwa na vitu vizito na vilio vya kataa ndoa hadi kamasi ziwatoke.

Mtu una kipato cha m1 kwa mwezi unahangaika na binti anawaza kupata mtaji wa kwenda dubai halafu ukishatoboka unasumbua watu na insperational words na mahubiri ya ajabu ajabu.
 
Wasipokusikia Tena basi!!!!
 
Na huyo mhaya atakuwa wa kiseke A
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…