Ndoa ni mitihani kati ya mke na mume

Ndoa ni mitihani kati ya mke na mume

0653400400

Senior Member
Joined
May 13, 2018
Posts
124
Reaction score
38
Ndoa ni asili ya baba yetu Adam na Hawa.
Baada ya Adam kuumbwa kwanza na akawa ni mwenye kukaa muda mrefu akiwa peke yake.

MUNGU akamuona kuwa ni mwenye unyonge mno, ndipo likaja wazo la kuumbwa kwa bi Hawa.

Kisha MUNGU akasema, nimemleta hawaa ili awe tulizo kwako upate kusemezana nae'kwa kuwa alikuwa mnyonge.

Cha kuzingatia hapa:
Kama Adam asingepatwa na unyonge "Hawa hapo inaonekana asingeumbwa.

Hivyo basi, mwanamke anaolewa ila jukumu lake kubwa ni kuhakikisha anamtoa mwanaume unyonge na kumpatia utulivu.

Na kingine ni kumzalia watoto na kumtunzia nyumba yake.

Na MUNGU kamwambia mwanamume, oeni katika wanawake wale mnaowapenda.

Kwa kuwa amri ya kuoa anayo mwanaume na si mwanamke.

Ila sasa karne hii jamani ina mambo,
mwanamke yeye ndio anachagua mwanaume, hapo tu pana tatizo" maana yake hachagui mume bali anachagua vitu tu ulivyonavyo maana yake hakutakuwa na mapenzi ya ndoa hapo ni ishara kuwa hiyo ni shida huko mnakoenda.

AJABU sasa:
Mwanamke ana miaka mingi hajaolewa huko mtaani kwa muonekano wake au tabia zake, akija hapa JF sasa.

Nataka mwanaume mwenye.
Stashahada.
Mwenye Mali.
Handsome.
Awe hajaoa.
Asie na mtoto.
Nk.

Mwisho nasema kuwa, kuwa bila ndoa ni nusu maisha na kuoa ni maisha kamili lazima mitihani iwepo kwani kuoana lengo ni kupimwa vitendo vyenu wote wawili.

Kwa hiyo ndoa ni mtihani na wanawake wa sasa hawataki hiyo mitihani tiari hilo kwao ni tatizo.
 
Back
Top Bottom