Ndoa ni chachu ya maendeleo?

Ndoa ni chachu ya maendeleo?

KENZY

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2015
Posts
36,631
Reaction score
89,393
Natumai mpo vyema na wenye afya,

Hoja kuu hapa ninayotaka kujua ni kama kichwa cha habari kisemavyo; "je, ndoa ni chachu ya maendeleo"

Natumai nitapata majibu maana humu kuna wanandoa na wanajua maswala haya.

Karibuni
 
Sio lazima. Inaweza ikawa ya mme mmoja na wake wengi... Right??
Okay hizo ni aina tu sasa turudi kwenye swali husika wewe waonaje..? hasa mme na mke 1 maana hizi ndo zipo kwa asilimia kubwa
 
Inategemea na wahusika wenyewe mliofunga ndoa namna mungu amewabariki.

Haina uhusiano wa uliempata anafaa au hafai,kwa mfano unaweza kupata mke\mume bora lakini ishu ya maendeleo ikawa na mushkeri hata kama unafanya juhudi kujikwamua.na mwingine akapata kimeo na mambo yakawa yanakwenda safi,au ukapata mtu safi na maendeleo safi,au bomu na maendeleo bomu pia.

Kwa upande wangu imekuwa chachu ya maendeleo kwasababu kila ninalofanya nafanya kwa juhudi nikizingatia kuna mtu pembeni yangu.

Mwisho kabisa MUNGU anahitajika kuweka mkono wa baraka kati yetu kwakuwa yeye ndiye mtoaji na muweza wa yote.
 
Kivipi..?
Swali lako halikuhitaji maelezo kiongozi. Ulivouliza inaelekea ulikuwa unataka jibu la ndio au hapana...

Sasa kama unataka maelezo hebu lipe nyama swali lako.

Namalizia chai hapa, ntakujibu.
 
Swali lako halikuhitaji maelezo kiongozi. Ulivouliza inaelekea ulikuwa unataka jibu la ndio au hapana...

Sasa kama unataka maelezo hebu lipe nyama swali lako.

Namalizia chai hapa, ntakujibu.
sawa lkn kumbuka hii ni sehemu yakuhoji pia mtu anaweza kuhoji as kama majadiliano yatahitaji...

nasubiri
 
Maendeleo ya vipi mkuu?
-Unaweza kujenga nyumba, kumiliki gari, shamba, biashara, watoto bila ndoa.
-Pia ndani ya ndoa unaweza kumiliki gari, shamba, biashara na watoto.

*USHAURI: vijana tusiache kuoa ukiwa una 'uwezo' wa kuoa sababu ndoa ni heshma na ni stara.
 
Namaanisha hayohayo uloyataja hasa maendeleo ya kiuchumi
 
Yes, ndoa ni chachu Ya maendeleo hasa ukimpata mwenza mnaeelewana nae na kusikilizana. Ila ukimpa mtu ambae ndani hakuna maelewano khs maendeleo sahau. Utayasikia kwa jirani tu.
 
Back
Top Bottom