Ndoa na mapenzi

Aug 18, 2019
80
177
Kuna tofauti kubwa sana kati ya ndoa na mapenzi, watu wengi wanadhani kwamba kumpenda mtu ama wote wawili kupendana kunatosha kabisa kuingia katika ndoa la hasha.

Mapenzi ni hisia za ndani kabisa ya mtu kutokea kwa mtu mwingine wa jinsia tofauti na inaweza tokea ukapatwa na hisia hizo lakini uliyempenda akawa hana hisia hizo juu yako, ama akawa na hisia kama zako hapo mtakuwa mmependana lakini bado sio sababu ya msingi sana ya kuingia kwenye ndoa.

Mapenzi unaweza mpenda mtu ambaye tabia na mienendo yake haitakiwi kabisa kwenye ndoa, ama ukampenda mtu ambaye mnatofauti kubwa sana ya kimtazamo wa kimaisha hata misingi anayoamini haiendani na ya kwako hapo mkiingia kwenye ndoa tuu kwa sababu unasukumwa na hisia za mapenzi lazima mambo yataharibika sana.

NDOA NI NINI..!?

Lazima tujue kwamba ndoa haina mahusiano ya moja kwa moja na mapenzi, ndio maana zamani wazee waliweza kuwachaguliwa watoto wao mke na akaoa na akadumu nae hii inaonyesha ndoa sio mapenzi.

Ndoa ni makubaliano ya kuishi pamoja mwanamke na mwanaume na kufuata sheria na kanuni zote zilizowekwa katika kulinda jambo hili.

1. Kuheshimiana.
2. Kusaidiana.
3. Kuwajibika kila mmoja kwa mwenzie.
4. Kufundishana na kukosoana na kurekebishana.
5. Kuaminiana na kutokuvunja uaminifu.
6. Kulea familia pamoja.
7. Kuwajibika kwa kila mmoja kwa upande wa mwenzie.
8. Kulindana kwa kila hali.
9. Kushirikiana kwa pamoja kwa kila jambo.
10. Kujua kila pungufu la mwanadamu mwenzio na kulikubali katika ndoa Hanna Mimi Bali kuna sisi na kila mmoja anaheshimu nafasi ya mwenzie kifamilia, kijamii, na kikazi.

Misingi na makuzi ya kimaadili yakipewa nafasi ya juu sana, vijana wengi wanatafuta mapenzi kwanza ndio wanaenda kwenye ndoa wakiamini kwamba ukishampenda mtu basi unaweza kuishi nae, wasichokijua ni kwamba unaweza kumpenda sana mtu lakini hafai hata kidogo kujenga nae familia.
 
Back
Top Bottom