laii
JF-Expert Member
- Oct 10, 2016
- 857
- 1,126
Nimekuta Mahali nikaona si vibaya nikishea na nyie
JITAZAME MPENDWA YESU ANARUDI HARAKA
ISAYA 33:1 imeandikwa hivi.
Ole wako wewe uharibuye ila hukuharibiwa, utendae hila wala hukutendewa hila! Utakapokwisha kuharibu,utaharibiwa wewe,utakapokwisha kutenda kwa hila,wao watakutenda hila wewe.
Fuatilia ujumbe huu kwa makini.
Kuna watu wanatabia ya kuharibu maisha ya wengine ila wasijue jicho la Mungu liko kila mahali duniani mwote ili amlipe kila mtu kulingana na matendo yake. Yeremia 32:19
Hebu fikiria. Wewe ni mwanamke Mungu amekuumba vizuri tena akakupa urembo mzuri.
Na badala ya kumtumaini Mungu na kumtegemea yeye ili akupe mwenzi wako wa maishani uwe na familia Njema, umeutumainia urembo wako na kuutumia kama kitega uchumi chako.
Tena bila hata haya wala huruma umeufanya urembo wako kuwa sababu ya wengi kulia kwa sababu ya ndoa zao na kusababisha watoto kubaki na kilio na uchungu moyoni na kuishi kama yatima.
Unachukua mume wa mtu anaacha mke wake kwa ajili yako huku watoto wakitenganishwa na mama yao wanaishi wakisononeka na kulia moyoni kwa kutenganishwa na mama yao.
Mwingine anaachwa pamoja na watoto wanaishi Kama yatima unaanza kufurahia Mali ambayo hukuyataabikia,
na kuyafurahia huku uliyesababisha akafukuzwa akililia ndoa yake na kuilaani siku ile aliolewa kwa ajili yako.
Sikia wewe mwenye tabia hiyo yatakayokupata kwa sababu ya uovu wako!
Utaonyeshwa raha ya kila aina sawa, utaitwa majina yote mazuri ya mahaba kwa huyo uliemchukua sawa,
utapewa kila unachotaka sawa, utafurahia na kutumia kila ulichokuta humo kimechumwa tayari sawa,
Utaaanza kumwita mume wangu na yeye kukuita mke wangu sawa, ila yakupasa ufahamu kuwa Mungu anaieshimu Sana ndoa na kwa Mungu Hakuna ndoa mbili.
Ataanza kukuambia Yule alikuwa mshenzi,mjinga, kinyago ndio maana nilimfukuza nikuoe wewe sawa, utaungana nae kumdhihaki na kumtukana aliefukuzwa ili wewe uingie sawa
Utajaribu kumwonyesha mapenzi motomoto na kuonyesha wewe ni mrembo kuliko mke wake aliemfukuza sawa, utajiona wewe ni mshindi sawa
Lakini kumbuka hicho hicho kitanda unalalia aliekuwa analalia alikuwa mrembo ndio maana alikilalia na hayo maisha uliyoyakuta kagaramia yeye.
Hivyo usifikiri Mungu amefumba macho yake ila amekupa muda wa kufanya uovu wako ili akulipe mshahara unaostahili na kumtetea mwenye haki maana Mungu ni wa haki.
Unapofanya uharibifu Mungu huruhusu shetani akupe furaha ya muda na wakati huo huwezi kuona kitu usijue yatakayofuata.
Ni uchungu Sana tena usioelezeka mtu aliepoteza ndoa yake huku akililia watoto wake huku asiejua thamani ya ndoa akifurahia na kuvuna ambacho hakupanda na Mungu amtazame tu!
Na hapo shetani atakupa kiburi na kujiona mjanja huku ukimdharau Mungu na kudharau maonyo yaliyopo mbele yako,
hata kuruhusu moyo wako kumtukana mwenye haki ya ndoa,bila kujua Mungu amekuweka kiporo ili aonyeshe gadhabu zake kwako.
Na hapo ndipo utasema Kama ningalijua, utakumbuka maonyo uliyopewa itakuwa umechelewa
Utatafuta tiba hutaiona utatafuta wahubiri uliowadharau wakikuonya na kukupa neno la Mungu hutawasikia.
Neno la Mungu linasema. Ayubu 20:5-7
Yakuwa shangwe ya waovu ni ya muda kidogo,na furaha ya wapotofu ni ya dakika moja tu.ujapopanda ukuu wake mpaka mbinguni,na kichwa chake kufikilia mawinguni
Hata hivyo ataangamia milele Kama mavi yake mwenyewe.hao waliomwona watasema yuko wapi?
Urembo uliokuwa nao utatoweka kama moshi huku watoto wa uzinzi na huyo uliezaa nae watakapokuwa wakiomboleza yatakayowafikia
wakati saloon zote na vipodozi ulivyojiremba navyo vitakukana na kuikataa ngozi yako.
Wakati rafiki zako walioshabikia uovu wako watakapokukimbia,
wakati vitanda vya hospitalini vitasema unavisumbua huku madaktari wakikutazama wasijue lakufanya maana dawa zimekukataa,
Wakati nywele ulizosuka kichwani kwa gharama aliyetaabikia aliefukuzwa zitakukataa,
waakati waliozunguka kitanda chako wakiomba lakini maombi yao Mungu asisikilize maana ulikataa Maonyo.Mithali 29:1
Wakati ambapo pesa na mali uliyokuwa unafurahia zitakukataa,hayo ndio yatakuwa malipo yako mpaka kuangamia kwako,
huku Mungu akimfariji alieachwa kwa ajili yako na watoto wake maana kilio cha mwenye haki Mungu husikia na kuwatetea.
Ulipokuwa ukifanya ubaya wako ulisema hivi: Isaya 47:10-15
Maana umeutumainia ubaya wako,umesema hapana anionae hekima yako na maarifa yako yamekupotosha,
nawe umesema moyoni mwako Mimi ndie wala hapana mwingine zaidi yangu Mimi.
Kwa sababu hiyo ubaya utakupata,wala hutajua kutopoa kwakwe, na msiba utakuangukia, hutaweza kuuondoa, na ukiwa utakupata kwa gafla usioujua.
Simama sasa na uganga wako, na wingi wa uchawi wako, uliojitaabisha nao tangu ujana wako, labda utaweza kupata faida, labda utaweza kushinda.
Umechoka kwa wingi wa mashauri yako, basi na wasimame hao wajuao falaki, watizamao nyota, watabirio kila mwezi mambo ya mwezi huo wakakuokoe na mambo yatakayokupata.
Tazama watakuwa Kama mabua makavu, moto utawateketeza hawatajiokoa na nguvu za mwali wa moto.
Urembo wako na majivuno yako pamoja na kiburi chako kitakapokuwa kimefika mwisho utakapokuwa ukipokea mshahara wako utalia utaombolea utatafuta Wale waliokudanganya hutawaona tena.
Wale wachawi uliowaendea ili wakusaidie kufanya uharibifu wako hawataweza kukusaidia wakati gadhabu ya Mungu itakaposhuka juu yako.
Neno la Mungu linasema ndoa iheshimiwe na watu wote kwa maaana wazinzi na waasherati Mungu atawasukumia adhabu. Waebrania 13:4
Na alichokiunganisha Mungu mwanadamu asikitenganishe.wewe u nani utenganishe alichounganisha Mungu? Mathayo 19:5-6
Na ninyi wanaume mnawaowafukuza wake zenu kisa umepata mrembo unaona huyo ulie nae kazeeka wakati wewe ndie uliemzeesha
wacheni niwaambie msidanganyike Mungu anawaona mtalipwa kiasi kitimilifu cha matendo yenu.
Unaona unapewa mapenzi ya nguvu kuliko mke wako sawa.
lakini ujue mke wako ndie alie na uchungu na ndoa na familia uliyo nayo na Mungu anamheshimu ndio maana umefanikiwa ukafika hapo ulipo.
Ila nataka ufahamu kuwa huyo ulie nae ukamwacha Mkeo ni kahaba na ni mwizi na ni mtafutaji Hana huruma na familia yako hata, kama unaona anajipendekeza kwa sasa
Siku atakapomaliza kilichomleta ndipo utamkumbuka mkeo uliemdharau na kumfukuza na kuona umuhimu wake kwako.
Namuomba Mungu kama uko hapo na ni wewe utambue hili mapema kabla hujachelewa umrudie mke wako uliepewa na Mungu usije ukasema sikuambiwa.
Wanaume wengine ni waajabu. Mungu kakupa mke ukiwa huna hata mahali pa kulala umefanikiwa na amekuzalia watoto wazuri unaanza kumdharau
aliekufanya ufanikiwe unadharau hata watoto wako kisa umepata mrembo usijue Hakuna zaidi ya mke wako zaidi yake jua ni kahaba tu.
Sasa mali yako uliyochuma na mke wako imeanza kufilisika unasema yule mke wako kakuendea kwa waganga unaanza kuzunguka kwa waganga bila kujua mchawi ni wewe mwenyewe na huyo ulie nae.
Wanaume wote niwaambie kuweni makini Sana na wake zenu na kuwaheshimu na kuwapenda.
usione Mali ulizo nazo ukafikiri ni akili au ni nguvu zako. Unapaswa kujua Mungu husikiliza maombi yetu na kutumwagia baraka tunapoishi na wake zetu vizuri.1petro 3:7-9
Na ikiwa ungependa ndoa yako isiharibike basi achana kabisa na mpango wa kando ishi na mke wako vizuri kumpenda na kumtunza atapendeza tu!
Usitembee na mke wa mtu kwani kwa kufanya hivyo Mungu atakuharibu na wewe vile unavyoharibu ya wengine.wengi wanapitia mateso na uchungu katika ndoa zao kwani wanavuna walichopanda.
Kama wewe ni mwanaume au mwanamke na hujaoa au kuolewa usiharibu ndoa za wengine kwani kwa kufanya hivyo
Mungu hatakupa wako na yule utakaepata huyo ndie wa kutimiza gadhabu ya Mungu kwako kwani lazima uvune ulichopanda.
Na ili Mungu akuepushe na hayo yote unamwitaji Yesu ili uweze kuushinda ulimwengu
kwa kuwa bila Yesu huwezi kuushinda ulimwengu. Kumbuka kuwa na Yesu ni faida kubwa.
Na wewe uliyefanya mambo hayo na sasa kuna mambo unapitia kwa sababu hiyo unahitaji toba na kumruhusu Yesu atawale maisha yako atakusamehe na kuyafanya yote kuwa mapya kisha utapata uzima wa milele.
Natumaini wewe unaesoma ujumbe huu umebarikiwa na unaweza kumsaidia mwingine mwenye tabia hiyo,ili Mungu amrehemu na kuiacha tabia hiyo na kujiokoa katika uharibufu uliyo tayari kuijilia dunia yote kwa watu wa tabia hiyo.
Na wewe ambae unamwitaji Yesu ushauri au maombi nifuate inbox nitakuongoza jinsi ya kumpokea Yesu na nitakushauri na kukuombea na Yesu ambae ndie jibu la mambo yote atafanya.
Share na wengine na Mungu atakubariki hakika
*PASTOR CONRAD CONWELL*
*THE GRACE OF CHRIST ASSEMBLIES CHURCH (MOROGORO)*
*0753391634*
*(WHATSAPP)*