Kila deva na kasri yake

Kila deva na kasri yake

Poppy Hatonn

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2021
Posts
3,966
Reaction score
6,658
Wale watu wa Magharibi hawajui maana ya haya maneno ya Mashariki.

Deva ni mungu mwanaume na devi ni mungu mwanamke.

Lakini watu wa Magharibi utawasikia wanasema deva Rihanna au deva Beyonce ambayo siyo sahihi. Wanapaswa kusema devi Rihanna.

Hata hapa utawasikia watu wanasema deva Kajala Masanja au deva Elizabeth Michael au deva Wema Sepetu. Hii ni makosa.

Kwa hiyo kila deva ana kasri yake. Yaani kila Mungu ana kasri yake. Kila mtu ana nyumba yake.
Kwa hiyo unapomfikiria Yesu mfikirie Yesu pamoja na kasri yake. Unapofikiria kuwa na utukufu kama Yesu lazima pia uifikirie nyumba yako( yaani nyumba yako ya Manzese pia imegeuka nayo Ina utukufu kama kasri ya Yesu

Kwa hiyo wewe siyo nyumba yako na nyumba yako siyo wewe. Matatizo ya nyumba yako yanayokukwamisha lazima yarekebishwe. Kama tatizo lako ni mke wako au watoto,basi lazima uwaelimishe. Matatizo hayo hawawezi asilani kuondoka Kwa wewe kujitakasa.
 
Back
Top Bottom