Ndoa jambo muhimu sana

Molembe

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2012
Posts
9,933
Reaction score
11,865
Kwa mila zetu waafrika mtu mwenye ndoa anaheshimika sana sasa sijui ni shetani kawapitia vijana wenye elimu na wale wenye uwezo wa kifedha wasioe na kuolewa.

Fedha na magari ni vitu vya kupita tu lakini ndoa ina raha yake bhana hasa ukimpata mwanamme/mwanamke anayejitambua na mwenye upendo wa kweli, kuna raha ukitoka kazini ukapokelewa na mke/mme na watoto halali wa ndoa.

Sasa sijui ni ushamba au ulimbukeni maana wakishazipata hawataki ndoa tena jiulizeni ingekuwaje kama mama zenu na baba zenu wangekataa kuolewa/kuuoa, mtu miaka 30's umo tu hutaki kuoa au kuolewa acheni kuwabania wenzenu wana hamu ya kuja kula upepo na raha za duniani.
 

Hahahhaa.. mkuu Molembe vipi tena. Mbona unajazba hivyo...we tulia kwene ndoa yako bwana tuache sisi. Ivi unafikiri hayo yote hatuyajui. Tunajua sana, tena sana tu. Mchana mwema mkuu. hehehehhe..Dah.!
 
Last edited by a moderator:
Hahahhaa.. mkuu Molembe vipi tena. Mbona unajazba hivyo...we tulia kwene ndoa yako bwana tuache sisi. Ivi unafikiri hayo yote hatuyajui. Tunajua sana, tena sana tu. Mchana mwema mkuu. hehehehhe..Dah.!

Mkuu muoe bhana nina hamu ya kucheza kwaito.
 
Last edited by a moderator:
siredi kama hizi wakati huu wa mchana hata kama umenuna unacheka tu, aya niwaache muendelee kucoment.
 
mi naimba tuuu...

Ni​muoee naann...nimuoee....eee, nimuoeeee aaaaa? x 2
we siunajua wazuri ni wengi ila kumpata mwenye mapenzi ya kweeli ndio balaa,
wengi ni wajanja watoto wa mjini wamejawa utapeli tamaa x2
Yasiwe kama ya Kasinde kila sikuu car crush, ajue nidhamu na mila ya kweetu mjuzi kupetipetii,
usimtake kama lara1 ni mtemi ana hasiraa, mpole kama misschagga
Na quotes kama mwalu akiwa na DEMBA , utani kama wa Queen Horse ,
naogopa sana vijana wasasa wasije wakanitenda, nikazama na huba mapenzi ya kweli wakaniacha wakaendaa...
.....................................nimuoe naaani nimuoeeee...eeee nimuoeee naaaani ........aaaaaa.

 
watakusikia na kuamua

ila mimi BADO NIPO NIPO kwanza mkuu

ndoa ni maamuzi na kukubali majuumu.
sio kuvaa shela...
sio kuolewa kisa umri umefika...
sio kuzaa kisa unatamani mtoto.....
sio kuolewa/kuoa ili jamii ikueshimu.....

noooooooooooooo
 
Ndoa ni ngumu sana..unatakiwa ujipange haswaa kiakili ,kimwili na kinafsi ili uweze kukubali mabaya na mazuri ,shida na raha za ndani ya ndoa
Ndoa si lele mama aisee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…