Ndoa ipo mashakani

sindani

Member
Joined
Sep 13, 2013
Posts
89
Reaction score
71
Hawa wanandoa wameoana toka 2017 kipindi hicho mapenzi yalikua mubashara, (hadi nikatamani kuolewa
)ila 2018 baada ya kubarikiwa mtoto wao wa kwanza cousin yangu akaanza kukipata cha mtema kuni.

Mwanaume alibadilika kwa kasi ya 4G, harudi nyumbani, ulevi kupitiliza, mara mida ya kurudi ikawa saa nane au hata kumi na mbili, siku nyingine saa nne asubuh ndo jamaa anapatikana, na vipigo juu.
Huyu cousin wangu mara nyingi nipo nae tumekua pamoja, mambo yake mengi ananiambia,so do l.
Kuna kipind hata wakishiriki tendo la ndoa jamaa anamuita jina la mchepuko, ila kwa sasa huyo mchepuko kaachwa, kapata mchepuko mwingine MKE WA MTU.(cjui mumewe atakua ni member huku)sasa penzi ndo limedamshi, kurud nyumban ni mida mibayaa saa saba hadi kumi, alishampiga ndugu yangu kisa alimuonya kuachana na mke wa mtu, haambiliki haskii, cousin aligundua haya baada ya kushika simu ya mumewe na kukuta charting wanavyoelezana wanavyopendana, mara guest na lounge wanazoendaga, na miamala wanavyotumiana hela,
Hapo ndoa bado mbichi kabisa, mke analalamika mumewe akishanunua chakula basi tena kwa kusumbuana sana, mahitaji yake muhimu hana mpango nayo, kila siku hana hela(huwa najiuliza iweje shemeji alewe kila siku, kwenda guest na kumuhudumia mke wa mtu, afu nyumbani kwake aseme hana hela?)

Me nilichomshauri ajitafutie mchepuko tu ajiliwaze, cyo kwa stress hizo kukesha usiku kusubiri mtu hujui kama atakuja au analala huko, ila akiwa na mpango wa kando atamliwaza.


Wanajamvi, mnamshauri nini huyu.
 
Huyu hakujisahau, huwa anajipenda sana, kimwili yupo vilevile hata baada ya kujifungua, nyumban kwake pasafi sana, labda mambo mengine ya chumbani huko sijui, lakini pamoja na hayo shemeji hapaswi kufanya hayo
Tatzo huwa linaanzia kwa wanawake wenyewe pindi wanapojifungua mara nyingi huwa mnabadirika sana mnasahau majukumu yenu n mnakuwa rafu sana
 
"Mjue sana Mungu, ili uwe na amani; Ndivyo mema yatakavyokujia."
AYUBU 22: 21.
 
Kwenye issue kama hizi wanawake wengi huliwa na rafiki wa waume zao. Inaanzia shemeji ongea na rafiki yako, unamueleza kuwa mahitaji nyumbani hayataimizi. Shemeji anaanza kukupa laki mbili uweke sawa mahitaji ya nyumbani, anakupigia simu muda mibovu wakati mume yuko kwa mchepuko.
 
Naona mkuu unafurahia ndoa ya mwenzio kuyumba naona hadi viemoji vya kucheka anyway tuachane na hayo

Mimi Siku zote nawaambia acheni kujiingiza kweny matatizo kama nyama na maziwa unapata kila siku kwa nini ufuge
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…