Ndoa inaelekea kunishinda

michepuko,ukiingia kichwa kichwa unaangukia pua halafu unaishia kulia mwenyewe
Alafu wamenipenda hutoamini wenyewe tu wameingiwa na huruma na wamemsema Kama nini maana text zao naziona mmoja ndoalimdanganya anapeleka mahari kwao amuoe alikuwa na bwana ake akamuacha kisa huyu baada ya kumpigia naye alihisi kudata maana alisema hadi kwao kuwa kapata mchumba huyu ndompaka alilazwa kwa stress karusiwa juzi hapa ndoanamtishia anaenda kumloga ni mbulu yangu macho walogane tu vurugu ziishe
 
Jamaa kazingua sana, unachepuka then unadanganya upo single? Mwambie mtu ukweli aamue mwenyewe...
 
Nafikiri haya ni maneno yakutoa faraja.

Cha msingi usisahau kujiombea wewe,kumuombe yeye,kuiombea ndoa yenu,kuruhusu Amani na upendo vitawale uwe na roho ya kusamehe na kutokuweka visasi.

Unachokipitia ninakifahamu 💯.

Mtangulize Mungu Kwa kila kitu
 
Simu ya mwanaume ni kama kitunguu ukiichunguza lazima utoke machozi achana nayo.
 
Pole sana ndugu, maisha ya ndoa yana changamoto sana.Jiatahidi kutuliza akili na kuomba Mungu akupe utulivu kwanza umzae huyo mtoto.Baada ya hapo utapima upepo..kama hauelewki ondoka mapema..na kuanzia sasa acha kabisa kushughulika na simu yake.Acha Bora usijue kuliko kuumia kila wakati.
 
Labda tuanze hivi.Je kuna jambo jingine ambalo jamaa anakuudhi nalo? vipi unapata attention na matunzo kwa ukamilifu? Vipi wewe mwenyewe uko perfect kwake?

Iko hiv mwanadamu anayo madhaifu yake.hata wewe unayo maudhi kwake. Kwamba aliamua kukiri kosa na kumpigia mzinzi mwenzie kwamba sasa anasitisha rasmi kuzini naye,nadhani ungemshukuru Mungu hata kwa hatua hiyo. kuhusu hiyo list ya hao wengine ungeendelea kumsaidia hivyo hivyo kuipunguza kwa style uliyofanya awali.Otherwise wapo wachache sana wanaoweza kuchukua ujasiri wa kumpigia mzinzi mwenzie mbele mke wake na kumpa notice ya kusitisha rasm uzinzi.

So mimi naona uko kwenye hatua nzuri ya kuimarisha ndoa yako badala ya kuanza kulialia ni bora ungekomaa uimalize hiyo list ya wazinzi
 
Huu ushauri sasa duu..ila sio mbaya mara moja moja nae apoozee kwa pembeni.
Na wadau wakutoa hiyo huduma wamejaa humu kibao tu.
 
Tambua hata wewe kwa huyo mume ni mchepuko ulichowazidi wengine ni kutangulia kugundua anachepuka usishangae akibanwa upande wa pili na wewe ukaambiwa samahani nilikuwa nimeoa kabla sijaoana na wewe
 
As long as mumeo anakujali na anakupa mahitaji yote ya msingi, vumilia na kazi iendelee!

Hata ukivunja ndoa na ukaolewa na mwanaume mwingine naye atakuwa na michepuko tu mana wanaume tumeumbwa hivyo. Mwanaume anayetosheka na mwanamke mmoja ni masikini asiyekuwa na pesa za kuhudumia wanawake wengi, mwenye afya mgogoro na mwenye upungufu wa nguvu za kiume.
 
Halafu kwanini anapekuwa pekuwa simu ya mwenzake?? Yaani wanawake huwa wanavitafuta vilio kwa makusudi kabisa. Ukisikia mwanamke mjinga huivunja ndoa yake kwa mikono yake ndio hivi sasa!
 
Umeanza vema ila mwishoni umeharibu kumwambia agonjwe nje. Ovyo kabisa wewe!!!!!
 
Pole sana, mambo yake muachie mwenyewe, hayanaga muongozo...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…