Lakini mbona wengine wanasema inawezekana kuvunjwa(rejea posts zilizotangulia).Hiyo ndoa ya Kikatoliki haiwezi kuvunjika hadi kifo! Kuvumiliana katika ndoa kama hii ndio maana halisi ya kupendana katika shida na raha, katika afya na magonjwa, katika nguvu na udhaifu n.k. Kama huyo dada anataka atengane na meza ya Bwana basi avunje hiyo ndoa!
Ninachojua mimi ni kwamba, kanisa haliwezi kuvunja ndoa. Pale inapoonekana kuna mapungufu yoyote kama uzizi, kichaa, uchawi au kutokuelewana kabisa ndani ya nyumba, basi kanisa linaweza kuridhia mtenganishwe na sio kuvunja ndoa maana kanisa linaamini kwamba ndoa inaunganishwa na Mungu. Na alichokiunganisha Mungu, binadamu hawezi kutenganisha!
Chakufanya hapo, kwa mtizamo wangu ni kwamba, huyo dada adai talaka huku akijua kabisa kwamba hataweza kufunga ndoa yoyote ya kikristu. Labda serikalini au dini nyingine. Kwa kweli imekula kwake.
Kuhusu huyu jamaa, aende akawaone madaktari kwanza wamwambie tatizo lake hasa ni nini na kama lina tiba atumie. Wengi walikuwa na tatizo hili, wakapata matibabu wakapona. Kwahiyo akapimwe kwanza. Kama halina tiba, sina la kusema zaidi ya kumpa pole.
Hiyo ndoa ya Kikatoliki haiwezi kuvunjika hadi kifo! Kuvumiliana katika ndoa kama hii ndio maana halisi ya kupendana katika shida na raha, katika afya na magonjwa, katika nguvu na udhaifu n.k. Kama huyo dada anataka atengane na meza ya Bwana basi avunje hiyo ndoa!
ndoa bila tendo la ndoa sio ndoa......hata kwa sheria ya kanisa katoliki ..........anatakiwa kwenda kuwaona viongozi wake wa dini ndoa inawezekana kutenguliwa
kukumbatiana ni tendo la ndoa
kukumbatiana ni tendo la ndoa
heshima wakuu.....
Kuna kisa nimesimuliwa kutoka kijijini kwetu kilichompata binamu yangu wa kike mtoto wa shangazi.
Kafunga ndoa ya kikristo(katika madhehebu ya katoliki) miezi mitano iliyopita. Kwa kuwa hakuwahi kumegwa na huyo jamaa yake kabla ya ndoa hakujua nini kingetokea baadae. Baada ya muda ndipo aligundua kuwa jamaa hana uwezo wa kufanya kazi kabisa(jongoo hapandi mtungi). Hivi sasa anaomba ushauri kwa ndugu na jamaa afanye nini, ameshauriwa arudi nyumbani ili taratibu nyingine zifuatwe lakini yeye hataki anaogopa kumdhalilisha huyo mume wake. Anataka ndoa ivunjwe kwa taratibu na sheria za kanisa ndipo ataondoka.
Naomba kuuliza kwa wajuzi wa sheria za ndoa (kanisa na serikali), je ndoa hii inaweza kuvunjwa???
Mchango wenu tafadhali...
Lakini huyu inaonekana tatizo lake ni la kuzaliwa nalo..alichokiunganisha mungu mwanadamu awezi kukivunja ushaona wameandika mahanithi awatakiwi kuwa na wake??

Ule ni ugonjwa na wakisimama na mungu wanapona kabisa wakiwka imani zao pamoja kama ajamwega anashindwa nini kuvumilia maisha yake yaliobakia kama amevumilia tangu anazaliwa...kuivunja ama kushawishi kuivunja ni kujitafutia uhanithi mwenyewe kumbuka nao wana sehemu ya kuwa na wake ila iwapo utashiriki hili a kuvunja nakwambia hata kama una watoto kuzima ndani ya ndoa easy mwana wapo waliokuwa vidume vya mbegu leo ni superget sio walipenda ...
Hata kama hakuna tendo la ndoa? Hii sheria inabidi iangaliwe upya..Itifaki imezingatiwa!!!!!!!!!!!!!!

Kwa mujibu wa sheria ya ndoa sura ya 29 ya mwaka 1971 kama ilivofanyiwa marekebisho mwaka 2002 kifungu cha 9(1) kimeeleza kuwa "marriage means the voluntary union of a man and woman, intended to last for their joint lives" kwa mujibu wa ibara hii wanandoa wanatarajiwa kuishi kama wanandoa kwa maisha yao yote. Aidha ifahamike pia kuwa ndoa ndio chanzo cha familia na serikali inalinda familia kama taasisi ya taifa kwa namna ya pekee kwa sababu kuwepo kwa taifa kunategemea kuwepo kwa familia.

Kwa hiyo, sheria hii ya ndoa imeeleza sababu ambazo zinaweza kupelekea ndoa kuvunjwa kifungu cha 99 kinasema "such marriage must be broken down irreperable" kwamba ndoa hiyo haiwezekani tena kuinusurika kama tafsiri iko sawa; kwa hiyo kwa sheria ya Tanzania kama huyu mdau ataenda mahakamani ninauhakika hii ndoa hiwezi kuvunjwa kwa sababu kwanza, bwana yake hakufanya willful refusal to consumet ila ameshindwa kutokana na ugonjwa ambao jitihada za kuutibu bado hazijafanyika na ikaonekana imeshindikana. Pili, hili tatizo its tear and wear of marriage inampasa mwanamke avumilie wakati wakihangaikia tiba kwa hilo tatizo na Tatu, talaka kwa mjibu wa sheria ya Tanzania inatolewa na MAHAKAMA kama last option na kamwe mahakama tukufu haiwezi kutoa talaka wakati kuna alternative nyingine!

Mwisho, jamii ielewe kuwa kama ilivo kwasheria hii, kanisa katoliki (RC) haliwezi kuvunja ndoa kwa sababu yeyote ile kwa sababu ndoa inatenganishwa na kifo tu! kama kuna m2 anadhani inawezeka ajaribu then atatueleza hapahapa kwenye jamvi hili. Mie nashauri aanze kuhangaikia tiba kuliko kufikiria kuvunja ndoa ki2 ambacho hataweza kwa mujibu wa sheria!!!!!

atakuwa mnafiki huyo binamu yako, kwani hakumbuki kama alimwambia atakuwa nae kwenye shida na raha? Sasa inakuaje atake kutumia taratibu za kuvunja ndoa? Aache ufala, amvumilie tu mume wake.