Ndoa haitaki usanii

Ndoa haitaki usanii

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,579
Reaction score
161,430
Wakati mwingine maisha ya ndoa hayaitaji usanii hata kidogo maana ndoa ukicheza nayo lazima ikupwelepwete tuu.Kabla ya kuamua kuishi na mtu tafakari na ujiulize hivi niko tayari kupambana na changamoto zake usiwaze harusi tuu na kujaza watu ukumbini.Kikubwa mwamini na kumtegemea Mungu kwanza maana kwa akili zako huwezi.
 
Aisee we ndo sasa unazidi kuogopesha vijana kuoa
 
Ndio tena ndoa takatifu ya kanisani. Pia ni mume mwaminifu. Hata nikifa Leo sitaacha wajane sita wala watoto kumi na moja

Hahaaa mbona wampiga kijembe marehem.

Hongera sana kuwa mume mwaminifu.
 
aisee we ndo sasa unazidi kuogopesha vijana kuoa

Wanaacha kumuogopa Mungu wanaogopa ndoa!!!! Kweli majasiri hatunao kabisa siku hizi. Zamani ili uoe ilibidi ufanye tendo moja LA kishujaa ili kuuthibishia umma Kuwa wewe ni mwanaume wa shoka. Wamasai usipoenda ukweni na kichwa cha Simba walikuwa wana kuona kama shoga vile
 
Kuna ukweli fulani, usipokuwa makini na chaguo lako itakula kwako kwa maana kila siku ya maisha yako itakuwa ni jaka moyo kwa kwenda mbele.
Ni changamoto kwakweli usipokuwa jasiri na mvumilivu unakata tamaa mazima.
 
Kuoa ni mtihani ambao majibu yake mpk sasa natafuta..
 
Ndoa haitaki wasanii but wanaoana wote ni wasanii.
 
Ndoa si mchezo ndo wanatufanya tuchepuke mke wangu akiniudhi au akinifanyia kibri natafuta mchepuko wa kutuliza stress
 
Back
Top Bottom