Ndoa, Familia na Jamii

Ndoa, Familia na Jamii

Nundu_Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 19, 2019
Posts
811
Reaction score
350
Ndoa ni msingi na chanzo cha familia ambapo familia ni kilele cha jamii.
Ndoa huleta familia na familia hufanya jamii. Tokeo la familia na jamii ni ndoa.

Ndoa inahusu mtu mwanaume na mtu mwanamke ambao wanakubaliana kadiri ya akili.

Uhusiano huu baina ya watu wawili, mwanaume na mwanamke ni tendo lililo katika akili na linaloendelea kwenye akili.

Kama tokeo la familia na jamii, ndoa imeshikiliwa na mambo makuu matatu. Hayo ni haya yafuatayo: moja, Uwepo wa hali ya juu yenye akili tunayoiita Mungu. Mbili, sheria ya maumbile na tatu, sheria ya maadili.

Tangu historia ya kuanza kwa mtu ndiyo pia kuanza kwa historia ya ndoa.

Mambo haya mawili la mtu na la ndoa yana chanzo chake Katika Mungu.

Kuanza kwa ndoa kunaanzishwa na Mungu. Hali hii imeendelea nyakati zote ndoa imekuwa ni jambo la kidini.

Karne zote katika jamii, ndoa imekuwa jambo nyeti lisiloweza kukubaliwa isipokuwa taratibu za kidini zimefanyika.

Wakati wote toka historia ya mtu, ndoa imekuwa ni sakramenti.

Hatahivyo, kwa sababu ya kukosa maarifa, elimu na uelewa wa dini/imani na mambo kwa ujumla, makosa yamekuwa yakifanyika dhidi ya sakramenti ya ndoa.

Mwelekeo huu wa watu kutotambua ndoa kama sakramenti umesababisha vurugu na kasoro nyingi kwenye familia na jamii.

Kuna madhara makubwa ndoa isipochukuliwa kama sakramenti. Ndoa, kama haijawa sakramenti maana yake i kinyume cha Mungu.

Madhara yatokanayo na ndoa kutokuwa sakramenti ni yote ya akili na mwili.

Itaendelea.......
 
Back
Top Bottom