Ndoa au bila ndoa chini ya maandiko matakatifu

Ndoa au bila ndoa chini ya maandiko matakatifu

John Achila Mukumwa

Senior Member
Joined
Jan 4, 2024
Posts
113
Reaction score
222
Ndoa au bila ndoa chini ya maandiko matakatifu

Ndoa ni nini
Ndoa ni mkataba unaofungwa katika kanuni timilifu za Mungu, alizozikusudia tangu mwanzo, kati ya nwanamume na mwanamke.

Kifungu cha 1Wakorintho 7:28 cha maandiko

1Wakorintho 7:28: "Lakini, kama ukioa, huna hatia; wala mwanamwali akiolewa, hana hatia; lakini watu kama hao watakuwa na dhiki katika mwili, nami nataka kuwazuilia hayo".

Katika kifungu hiki, Mungu hashinikizi kwamba watu wasioe au wasiolewe. Ndoa ni jambo jema, na lina faida nyingi sana katika maisha, na pia katika huduma, kwa sababu humsaidia mtu akae mbali na uzinzi na tamaa mbaya (1Wakorintho 7:2). Aidha, huondoa upweke (Mwanzo 2:18). Wawili wawapo mwili mmoja, ni nguvu zaidi na faraja.

Hapa, Mungu anatoa uchaguzi kwa mtu, ikiwa anao uwezo wa kujizuia, yaani kutawala hisia zake (1Wakorintho 7:9), akaishi hivyo hivyo, bila shida yoyote, ni vema zaidi kihuduma. Hii ni kwa sababu humfanya asisongwe na mambo mengi ya kindoa.

Mtu aliye kwenye ndoa, ni wazi kuwa upendo wake utagawanyika kwa sehemu. Biblia inasema atatafuta ampendezeje mume au mke wake:

1Wakorintho 7:32 "Lakini nataka msiwe na masumbufu. Yeye asiyeoa hujishughulisha na mambo ya Bwana, ampendezeje Bwana;
33 bali yeye aliyeoa hujishughulisha na mambo ya dunia hii, jinsi atakavyompendeza mkewe".

Lakini pia, atakutana na dhiki, zinazoambatana na ndoa. Dhiki hizo ni pamoja na kutatua migogoro ya kifamilia, malezi ya watoto, kuwagharamikia, kuwasomesha, matibabu, kuwafuatilia, kuivisha familia yako, na mambo kama hayo. Ni dhiki ambazo, zinaongezeka, na hivyo hutinga ufanisi wako kwenye utendaji kazi wa injili.

Paulo huiita “shida iliyo” sasa. Yaani, kusalitiana, upendo kupoa na kupishana. Ni mambo ambayo mara kwa mara hujitokeza katika maisha ya ndoa.

1Wakorintho 7:26 inasema, "Basi, naona hili kuwa jema, kwa ajili ya shida iliyopo, kwamba ni vema mtu akae kama alivyo. 27 Je! Umefungwa kwa mke? Usitake kufunguliwa. Umefunguliwa? Usitafute mke".

Ndiyo maana, 1Wakorintho 7:28, inasema "Lakini, kama ukioa, huna hatia; wala mwanamwali akiolewa, hana hatia; lakini watu kama hao watakuwa na dhiki katika mwili nami nataka kuwazuilia hayo".

Kihuduma, mtu ambaye hajaoa au kuolewa, hujipunguzia dhiki, kuliko yule aliye kwenye ndoa. Yaani, hujipunguzia majukumu. Hiyo haimaanishi kuwa aliye kwenye ndoa hawezi kutenda kazi vizuri. La hasha. Kazi anaweza kuitenda hata zaidi ya yule ambaye hajaoa, isipokuwa tu kwake dhiki na shida (majukumu) zitaongezeka.

Hivyo, suala zima la ndoa au bila ndoa, kupitia 1Wakorintho 7:28, linabaki kuwa la uamuzi binafsi, kati ya kuoa au kuolewa, au la. Cha muhimu, ni mwanandoa kuwa tayari kubeba majukumu, na siyo kukwepa kwa kutoroka.
 
Bila ndoa(useja) ni halali 1 Wakor 7:32 ``Yeye asiyeoa hujishughulisha na mambo ya Bwana…”

Paulo anasema mtu asiyeoa ana uhuru zaidi wa kumtumikia Mungu
Hana majukumu ya kifamilia

Kila mtu ana karama yake (1 Wakor 7:7)
Kama una uwezo wa kujizuia , unaweza kubaki bila ndoa
Kama huna, ndoa ni salama zaidi

Kwahiyo ndoa si lazima kwa wokovu. Useja si lazima kwa utakatifu.
 
Bila ndoa(useja) ni halali 1 Wakor 7:32 ``Yeye asiyeoa hujishughulisha na mambo ya Bwana…”

Paulo anasema mtu asiyeoa ana uhuru zaidi wa kumtumikia Mungu
Hana majukumu ya kifamilia

Kila mtu ana karama yake (1 Wakor 7:7)
Kama una uwezo wa kujizuia , unaweza kubaki bila ndoa
Kama huna, ndoa ni salama zaidi

Kwahiyo ndoa si lazima kwa wokovu. Useja si lazima kwa utakatifu.
Malikia wa ziwa barikiwa sana, ila shida iliyopo ni hayo mambo unayotenda pasipo ndoa huko uliko ziwani!
 
Back
Top Bottom