Ndo nini sasa mbwa kaoa He! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ndo nini sasa mbwa kaoa He!

Discussion in 'Jamii Photos' started by MziziMkavu, Jan 4, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jan 4, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: tborder, width: 100%, align: center"]
  <tbody>[TR]
  [TD="class: alt1, bgcolor: #FFFFFF"]Mwanamke mmoja wa nchini Uingereza ametumia paundi 20,000 (Karibia Tsh. Milioni 50) kwaajili ya kuandaa harusi ya kifahari na gauni la harusi la kifahari kwaajili ya mbwa wake wa kiume. Louise Harris mwenye umri wa miaka 32 alitumbua paundi 20,000 kwaajili ya harusi ya kifahari ya mbwa wake wa jike anayeitwa Lola ambaye aliozeshwa kwa mbwa anayeshikilia taji la mbwa mwenye sura mbaya kuliko wote Uingereza anayejulikana kwa jina la Mugly.

  [​IMG]

  Sherehe hiyo ya kifahari ilihudhuriwa na watu 80 ambapo gharama za kuukodisha ukumbi kwaajili ya harusi hiyo ya aina yake ilikuwa paundi 2,500.Mbwa Lola alivalishwa gauni la harusi lenye thamani ya paundi 1,000 ambalo lilitengenezwa maalumu kwaajili yake na duka la vito vya thamani la Swarovski.

  Mbwa Lola pia alivalishwa cheni shingoni na kikuku mguuni ambavyo vyote viligharimu paundi 750.Maua ya kupamba ukumbi wa harusi yaligharimu paundi 1,000 wakati wapambaji wa ukumbi walilipwa kitita cha paundi 3,000.

  [​IMG]

  Miongoni mwa gharama za harusi hiyo ni mabaunsa waliokuwa wakilinda usalama kwenye harusi hiyo ambao walilipwa paundi 400, madansa na wacheza shoo waliolipwa paundi 500, gari la kukodisha aina ya Bentley kwaajili ya maharusi liligharimu paundi 500 wakati Dj alilipwa paundi 500."Mbwa wangu ni fahari yangu na furaha yangu ni kuwafanyia kila kilicho kizuri", alisema bi Harris.Bi Harris alisema kuwa furaha yake imetimia kwa kuona Lola amefanikiwa kupata mwenza wake wa maisha ambaye amekuwa akicheza naye wakati wote.

  Unaweza kujisomea kwa kisukuma hapa na mitandao mingine; http://www.telegraph.co.uk/news/news...g-for-dog.html[/TD]
  [/TR]
  </tbody>[/TABLE]
   
 2. Chris_Mambo

  Chris_Mambo JF-Expert Member

  #2
  Jan 4, 2012
  Joined: Aug 11, 2010
  Messages: 597
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Duniani kuna vituko, duh!!!
   
 3. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #3
  Jan 4, 2012
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,843
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  majuu hamnazo!
   
 4. Blaki Womani

  Blaki Womani JF-Expert Member

  #4
  Jan 4, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 8,459
  Likes Received: 3,713
  Trophy Points: 280
  walimwengu wanavituko
   
 5. K

  KIJASHO Member

  #5
  Jan 4, 2012
  Joined: Mar 10, 2010
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nilishawahi kuskia kuwa hivi vijibwa vyenye manyoya sura nzima vinaufundi sana wa kuwaingia uvinza hawa wanawake wanavyovibeba sijui kuna ukweli
   
 6. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #6
  Jan 4, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 707
  Trophy Points: 280
  Sasa hii ni laana wala sio bure.
   
 7. chapaa

  chapaa JF-Expert Member

  #7
  Jan 4, 2012
  Joined: Feb 19, 2008
  Messages: 2,355
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  kumbe inshu yenyewe uingereza kwa bw Dave!!
   
 8. urioglory

  urioglory Member

  #8
  Jan 5, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Majuu mnazo kweli
   
 9. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #9
  Jan 5, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,858
  Likes Received: 4,537
  Trophy Points: 280
 10. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #10
  Jan 5, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  Kwa raha zao kwakweli ..
   
 11. Bushbaby

  Bushbaby JF-Expert Member

  #11
  Jan 5, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,577
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  duh... hata dog kanifunika,....Harusi yangu ilikuwa laki tatu!!....
   
Loading...