Ndiyo kateuliwa lakini hapendwi na wengi

Ndiyo kateuliwa lakini hapendwi na wengi

NewPage

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2021
Posts
1,380
Reaction score
2,236
Dr Mwigulu Nchemba kati ya Watanzania 10 wanaolitaja jina lake ni wawili au watatu ndiyo wanamwona ni Kiongozi mzuri. Dr. Mwigulu alikuwa mzuri wakati upinzani ulipokuwa imara - yaani Waziri wa Vijembe Vijembe hivi.

Hata nafasi aliyopewa na JPM ndiyo ilikuwa inamfaa. Kwa sasa alipaswa kuwa ile ya Bashungwa sio sijui. Wizara ya Fedha Mwigulu hafai - mnaweza mkawa mnaogopa bure tu.

Bora hata Dr Mkenda au Dr Kimei ana PR nzuri kuliko Mwigulu. Kuna wengi wanafaa nafasi hiyo lakini sio Mwigulu ambaye ni Mwanasiasa mkorofi, mwenye visasi na mjanja mjanja hivi.

Mwigulu bora hata angepewa nafasi ya Mhagama halafu Mhagama akapewa TAMISEMI na Ummy akapewa Utalii au Kilimo. Kwa Mwigulu ambaye ni Mwanasiasa haswa ni hakika uchumi utadorora kwa sababu utakuwa wa kisiasa zaidi na hata usitegmee wafanyakazi kupata maslahi mazuri na hata wafanyabiashara itakuwa hovyo hovyo tu.

Kwa kifupi Mwigulu hafai pale - bora abadilishwe haraka.
 
Back
Top Bottom