🚨 Ndio Ilikuwa Ijumaa…

Samatime Magari

Senior Member
Feb 10, 2017
103
387
FovHiqvWcAESsFu

.
Siku ambayo vijana wengi wala bata wanaikubali sana sababu ni siku weekend inaanza, wanaachana na kazi then wanapumzika, Ijumaa hii Agnes alikuwa bado yuko ofisini anamalizia vimeo vyake, Wenzake walikuwa washatoka wanaelekea Kidimbwi kula bata..
.
Agness akawa bado anapambana na hesabu zikae sawa. Huyu dada ni Banker halafu ni Agnes zile type za Masogange so as a banker pesa uliyopokea, uliyotoa na iliobaki lazima Ibalance nikimaanisha ubalance na mzigo uliochukua kwenye vault wenyewe wanaita cash scroll..
.
FovJCJTWYAAMt2O
FovJh18XsAAGVUS

.
Na hili ndilo Bi Agness alikuwa analipambania, Mungu si Athumani mida ya saa 2 akamaliza, Agnes akakabidhi mzigo kwa incharge then akatoka nje ili aanze safari Kufata wafanyakazi wenzake, akaingia kwenye Nissan Dualis yake kitu Push to start akabofya machine ikaitika..
.
Akatia tia gear pale akaachia brake mafuta yakafata machine ikaanza kusogea. Hapa alikuwa anatoka Baroda Bank Posta anaelekea Kidimbwi anapitia Salender bridge.To make long story short Agnes alivyokaribia kumaliza daraja mbele akasikia kama harufu ya kitu kuungua..
.
Mwanzoni akadhani ni tyre za gari za wengine maana kuna time wanashika brake tyre zinateleza zinatoa harufu ya muunguo. Ila harufu ikawa kali then akaona Moshi unatoka kwa Bonnet, ikabidi asimame then ashuke kuchunguza tatizo ni nini. Ile Anashuka tu moto ukawaka aisee..
.
FovKby5WIAItz3I
FovLD8ZWYAEjdbi


.
Kuna Vijana walikuwa pale wakachukua fire extingusher ya gari puliza ikaiisha na haikusaidia ndani ya Dk 10 tu machine yote ikaputika fire wakaja pale wakazima moto ila tayari mzigo ulishakua skeleton ikiwa na nyama kidogo, The good thing Agness alikua ameikatia gari BIMA comprehensive so at least mhaho haukuwa mkubwa sana..
.
Basi Watu wa BIMA kitengo cha claim wakataarifiwa, Agness kuna mwamba akajitolea kumpeleka Nyumbani akapumzike kwanza. sasa hili tukio baadaye lilifanyiwa utafiti kubaini chanzo cha moto ni nini Na hili ndilo la muhimu sana kushare na wewe..
.
Kaa vizuri ndani ya dakika moja utaenda kula madini adimu ambayo yatabadilisha mtizamo wako. Kwa Irene chanzo cha moto kilikuwa ni alarm na android radio + Music system alivyofunga pale kwa Fundi Michael..
.
Fundi Michael aka mkali wa Sound East Africa Mashariki na kati pale chini ya mwembe. Wataalamu wanaendelea kusema kwamba wiring iliyofanywa ilikuwa ya viwango vya chini Ikitumia material za bei rahisi plus ikiwa na loose ends za wire plus tape za hovyo hovyo..
.
FovMWmhXwAAyGtm
FovMzPqWYAIiNI5
FovM-TlXsAEwE-4


.
Tape za hovyo ni zile fundi anaunga wire then anazitape vibaya baada ya muda wire ukipata joto tape inaachia wire unakua uchi. Wakaendelea kusema mafundi pia waliunganisha wire bila kujua uwezo wa hizo wire kupitisha moto [current] ndo issue ikaanzia hapo..
.
Sasa Nissan Nyingi za Kisasa zina kitu inaitwa intelligent power distribution module [IPDM] ipo kwenye fuse box ya gari, Hii kazi yake ni ku manage flow ya umeme na kukata pale inapoona kuna sehemu flow ni kubwa au ndogo sababu ya fault flani..
.
Kwa Lugha nyepesi inafanya smart check au diagnosis ya matumizi na flow ya umeme wa gari na kuhakikisha yako sawa na kama kuna shida inakata. Ni kifaa flani kiko computerized na kina control na kumonitor distribution ya umeme kwenye gari kwa vitu kama power window, door locks, taa na components za engine..
.
FovOVGKX0AAxj_Y
FovN15MWAAEqvh1

.
Baadhi ya Mafundi hawaijui hii kitu hasa wale mafundi wa tester na wire, ukipeleka gari yako hapo kuwa makini hasa hizi gari za kisasa kuwa makini. . gari ukishapeleka kufunga vitu kama Music, taa za booster, Android radio, taa za vimuli muli ndo mara nyingi shida inaanzia hapa..
.
Mafundi wanakata wire bila mpangilio na ku by pass hii system [IPDM] hence inashindwa kufanya kazi yake kwa ufanisi [self-diagnosis]. Hapa ndo unakuta kuna wire zinatakiwa kubeba umeme mdogo ila zinabeba umeme mkubwa kama nilivyoelezea hapo awali..
.
Hii inaleta joto kali baadaye inaleta cheche na kama unavyojua cheche na mnunurisho wa petrol lazima moto ukuje tu ndugu. Na hii sytem ni nzuri sana sababu ikiwa active huwezi pata short kwenye gari, Kwa Toyota sijaona gari yenye nazo nimeona kwa Nissan tu, Toyota Fuse inakata fundi anachomoa anaunga wire maisha yanaendelea ila kuna baadhi ya gari usifanye hivyo utachoma gari..
.
FovO9rMX0AAfzyp
FovPIyHWcAIXT5p

.
Toyota hawanaga mambo mengi wao kikubwa ufike tu unapoenda ndo maana Afrika wanafanya vizuri, maana wao kuna relay na fuse tu hakuna hio IPDM, Sasa ukiona fuse imekata ni muhimu Kujua kwanza kwanini imekata then suluhu ipatikane na sio ku force umeme upite kwa nguvu..
.
Tena hizi Dualis ndo hazitaki kabisa kuforce issue za umeme, Nikushauri tu kama unamiliki Dualis ikiwa na issue ya umeme tafuta Fundi Yani tafuta fundi mzuri ambaye anaujua umeme vizuri na mifumo yake plus ana vifaa vya kupimia matatizo ya umeme, acha ubahili hapa utachoma gari lako..
.
Hizi nyaya zikiunganishwa za uwezo tofauti moto ukipita ile yenye uwezo mdogo itaungua sababu ya high current inatengeneza resistance kubwa na itaipa joto wire. Wakaendelea kusema kwa case ya Agness kuna wire ulizidiwa moto na hivyo kusababisha kupata joto plus joto la engine ukaungua ukachubuka ukawa uchi..
.
FovPnmLXEAAWrz4
FovP0fNX0AE-a8G

.
Baada ya wire kuwa uchi ukaleta cheche na cheche zikaleta moto kama nilivyoeleza hapo awali Yani ni kama Suzuki Carry Inabeba robo tani [kg 450], then wewe unaiwekea Tani moja [Kg 1000] so ni swala la muda tu italeta shida.. .
.
Sasa kuna sababu zingine kama kutumia vifaa aftermarket fake, wiring mbovu, wear and tear ya mfumo wa umeme [hii ni mara chache] nk . Unachotakiwa kujua ni kwamba Hizi gari latest kibongo bongo hasa 2010++ umeme wake uko complicated kidogo na hazitaki kubahatisha..
.
FovQCEgXwAIjzAR
FovQKbEX0AE7rJH

.
Gari ikishikwa na Fundi Michael kwenye umeme hachelewi kukuchanganyia wire huko gari unapiga starter unashangaa wiper zinawaka badala ya gari kuwaka Kikubwa Kama kuna vitu unaongezea vya umeme kwenye gari yako tumia vitu genuine na wataalamu sahihi wa kazi hizo ili kuwa salama wewe na chombo chako..
.
Natumaini umejifunza kitu kama jibu ni ndio basi usisahau kushare kwa ajili ya wengine hasa wamiliki wa Dualis hili ni muhimu kwao.
1676987555081.png
1676987619988.png

.
Kama unahitaji kuagiza gari Japan, karibu, tuko na network ya trusted dealers kwa Japan, UK, Singapore, Thailand etc., Dealers wanaotupa gari zenye ubora wa juu kwa bei safi kwa ajili yako Tutafanya mchakato wako wa kupata gari kuwa rahisi salama na unaojali muda wako..
.
WhatsApp Image 2023-02-21 at 4.34.57 PM.jpeg
WhatsApp Image 2023-02-21 at 4.34.58 PM.jpeg
WhatsApp Image 2023-02-21 at 4.34.58 PM (1).jpeg

.
Ofisini Posta Mpya Phoenix House mkabala na Mkapa tower tutaku assist + kukushauri, kama uko mkoani na unahitaji kuagiza gari karibu utatupa hitaji lako tutakupa Ushauri pia then tutakutumia options za gari ukishachagua utapewa invoice..
.
Utafanya malipo at cost [no extra cost] huko huko ulipo mpaka gari itafika na utakuja kuichukua au kuletewa ulipo. Hata kama umepoint gari mtandaoni share, tutakupa Gharama za hiyo gari mpaka unaishika mkononi at a discount price tunayopewa kama dealer..
.
Pia kama unahitaji huduma ya clearing karibu tutakupa huduma nzuri kwa gharama nafuu huku tukijali pesa yako na muda wako..

WhatsApp Image 2023-02-21 at 4.34.59 PM.jpeg
FovRFZcWcAI71oC
FovRW_GXoAIg62d

.

Asante
Samatime
0714547598..
 
Mtiririko umetulia vizuri hata mwanafunzi wa magari lazima aelewe Tu..
Kwa kifupi wenye magari ya nissan dualis hawatafanya makosa ya kizembe
 
Back
Top Bottom