Ndi-Ndi-Ndi ( Lady Jay Dee)

TheMeek

JF-Expert Member
Mar 12, 2016
460
400
Ndugu zangu Wanajamvi,

Salaam!

Napenda kuchukua nafasi hii kutoa ushauri kwa huyu Dada mwanamziki, na kwa wale wote wanaopenda au kutamani kuwa na maisha kama yake.

Ndugu zangu, mara nyingi nimekuwa nikimsikiliza huyu Dada na nyimbo zake ; na kumuonea huruma sana kwa maisha anayopitia.

Kipindi chake cha "The Daily Of Lady Jay Dee" kwenye EATV, kilimuweka wazi kabisa kuwa maisha anayopitia ni magumu sana ( only the noble men saw this)

Nimeusikiliza wimbo wa "Ndi ndi ndi " muda si mrefu ; Hakika alichoimba ni vidonda moyoni, maisha magumu na mateso anayopitia.

Watu wengi wamekuwa wakifikiri kuwa pesa ndio msingi Mkuu wa Furaha, Amani, Upendo na Ulinzi katika maisha. Lakini ukweli ni kwamba, pesa ni sehemu ndogo sana katika maisha. Namaanisha kwamba, ukiweka nguvu zako nyingi na akili nyingi kutafuta pesa, basi utakuwa unapitwa na sehemu kubwa sana katika maisha.

Mfano wa vitu vitakavyokupita ni kama Amani, Upendo, Huruma, Msamaha na Nguvu za kuushinda mwili wako (Vitu hivi ni vya Muhimu sana katika Maisha ya Mwanadamu ).

Ukivikosa- maana yake, Utakuwa unaishi chini ya Hisia zako na utakuwa unafanya vitu pasipo kujitambua. (Utajiona upo sahihi kwa unayoyafanya, but kwa watu wenye Uelewa, watakuwa wanakushangaa na kukuhurumia tu , na pia watakuwa wanaielewa safari ya mwisho wako vizuri pasipo wewe kujitambua).

Kiufupi, Kazi kubwa ya pesa ni kutengeneza Utu wa nje tu wa Mwanadamu na Mazingira yake, pamoja na vitu vilivyomo kwenye Mazingira yake ; Pesa ni sawa na Hekima au vazi.

Pesa inaouwezo wa kutibu Magonjwa au vidonda vya nje tu ya mwili , lakini sio vya ndani ( moyoni/rohoni); Pia inaouwezo wa kujenga kuta au Nyumba nzima ya kuishi lakini haina uwezo wa kujenga kuta za moyo wa mwanadamu .

Pesa ni Adui mkubwa wa Moyo na Amani; pia Pesa ni rafiki mkubwa wa Hisia ( Pesa ni sabuni ya Hisia za mwili, sio Moyo/Roho).

Hakika huyu Dada, ana majeraha makubwa sana katika Moyo wake; Naufananisha Moyo wake sawa na chungu kilichovunjika au chupa ya Pepsi iliyopotendeka.

Yeye ana amini kwamba, pesa au Mwanadamu , vinaweza kuunganisha huo Moyo wake; lakini ukweli ni kwamba, hataweza kumpata mwanamme yeyote wa kuutibu Moyo wake isipokuwa YESHUAH HAMASHIACH "Yesu Kristo"


Hivyo basi, Namshauri na kuwashauri kwamba, njia pekee itakayowapa Amani, Furaha, Upendo, Dhamira njema na matumaini ya kweli, ni kuishi katika njia za Mungu na kuyafanya matendo/mapenzi yake katika Jina la Yesu.

Bila kufanya hayo, mtazidi kuumia sana katika Maisha, na itafika mahala, shetani atawadharirisha katika Jamii kwa kuwaanika vibaya.

Asanteni na Mungu Awabariki sana.

Angalisho; ACHENI KUPOTEZA MUDA WENU KUPIGA SELFIE NA NYOKA.

85e8e7fe6f6d7659c08ab2a7902fd089.jpg
 
Ukiwa na Yesu ukakosa pesa/mapenzi utakua na furaha?
His Mercy, Love and Grace Endure forever! Yeye atakupa Uvumilivu na Furaha ambayo Huwezi kuipata kwa wanadamu. Utaridhika na utakua mtu mwenye Amani na mwenye matumaini ya kweli, confidence na mwenye uhakika na maisha yako
 
mbona huongelei kazi yake kama ni nzuri au sio nzuri umejikita kwenye personality yake?!! appreciate japo kazi yake.unless you have something personal with her.
Kazi yake sio nzuri; bali inatoa uchochezi wa ukatili wa kijinsia na kuwapa dharau, viburi na jeuri wanawake , wasiziheshimu ndoa zao. Pia inawapa wanawake na vijana kwa ujumla kutokuthamini suala la mahusiano / ndoa.

Hii ni hatari sana katika Taifa letu , hasa kwa vijana wetu.

Kumbuka, Familia ndio msingi Mkuu katika Jamii, na pia Jamii ndio Nguzo kuu inayojenga Taifa.

Kwahiyo basi, endapo tutakuwa na wasanii wanao hamasisha vijana wasipende mahusiano/ndoa.. Basi tutakuwa na Taifa Ovu , ; Amani , Umoja na Mshikamano havitakuwa nasi tena.
 
Kazi yake sio nzuri; bali inatoa uchochezi wa ukatili wa kijinsia na kuwapa dharau, viburi na jeuri wanawake , wasiziheshimu ndoa zao. Pia inawapa wanawake na vijana kwa ujumla kutokuthamini suala la mahusiano / ndoa.

Hii ni hatari sana katika Taifa letu , hasa kwa vijana wetu.

Kumbuka, Familia ndio msingi Mkuu katika Jamii, na pia Jamii ndio Nguzo kuu inayojenga Taifa.

Kwahiyo basi, endapo tutakuwa na wasanii wanao hamasisha vijana wasipende mahusiano/ndoa.. Basi tutakuwa na Taifa Ovu , ; Amani , Umoja na Mshikamano havitakuwa nasi tena.


Ona sasa hahaaaa
Ungesema tu toka mwanzo kwamba huo hujaupenda tungekuelewa kuliko kuzunguka wee hahaaa umebugi!

Ndi ndi ndi ndo habaree yenyewe ati
Acha kulazima negativity!
 
Ona sasa hahaaaa
Ungesema tu toka mwanzo kwamba huo hujaupenda tungekuelewa kuliko kuzunguka wee hahaaa umebugi!

Ndi ndi ndi ndo habaree yenyewe ati
Acha kulazima negativity!
Acha kusifia Uovu , dogo!
 
1459830900346.jpg
1459830913903.jpg
1459830920353.jpg
1459830927684.jpg


Nimekuta sehemu tu... kama ni kweli Mola azidi kumbariki Komando huyu. Ndi ndi ndi
 
Bwana TheMeek , Shaloom. Niwachache sana wanaweza elewa kile ulichoandika, sitaki kuchangia mengi lakini huo ndo ukweli wa maisha.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom