mihadarati
JF-Expert Member
- Aug 27, 2013
- 268
- 74
*Ndesamburo "chadema ni sawa na Mti wenye Matunda"
Mbunge wa Moshi Mjini Philemoni Ndesamburo amesema matatizo yanayokikumba chama cha demokrasia na maendeleo Chadema yanatokana na kundi la watu wachache wenye uchu wa madaraka ambao pia wanatumia na chama cha mapinduzi CCM kukivurga Chama.
Ndesamburo alisema kuwa wanaosababisha hali yote ilivyo sasa ni vijana ambao hawana uchungu na Chadema ,hivyo lazima uongozi uchukue hatua stahiki ya kinidhamu kwa watu kama hao.
Ndesamburo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Kilimanjaro alikuwa akijibu maswali ya wananchi kwenye mikutano yake ndani ya jimbo la Moshi,ambapo wananchi walitaka kusikia kwa Mbunge wao nini hatima ya mzozo unaoendelea ndani ya Chama hicho.
Alisema kuwa Kiongozi yoyote wa chadema ambaye anakubali kuhongwa na kusaliti chama ni msaliti mkubwa,na anahujumu maisha ya watanzania million 45 ambao wanakitegemea chama.
Mwananchi aliyejitambulisha kwa jina moja la Mohamed alitaka kujua hatima ya matatizo anayoyasikia kwenye vyombo vya habari ikihusisha chama na Mbunge wa Kigoma Kaskazini wa Zito Kabwe,pamoja na wanachama wengine Dk Kitilla Mkumbo na Samson Mwigamba ambao tayari wamekwishavuliwa uonachama na kamati kuu ya chama (CC).
Aliwaambia wananchi kuwa lazima uongozi wa chama ufanye maamuzi magumu kwa wanachama na viongozi wengine ambao hawatakuwa hawana nidhamu ndani ya chama na bila kufanya hivyo watajiamulia kufanya kama wanavyotaka.
Chadema lazima iwe tofauti na vyama vingine kwanza kwa kuwawajibisha wale wote ambao hawatakuwa wana nidhamu ndani ya chama,ili kuweza kuwepo tofauti na kwa sasabu ni chama cha upinzani hatuwezi kuwa kama CCM ambao wanakumbatia mafisadiAlisema.
Ndesamburo alisema kuwa Chadema kwa sasa ni sawa na mti wenye matunda hivyo CCM haiwezi kuacha kuipiga mawe,lakini itaendelea kupigana na kuhakikisha inafanya vizuri kwa kuwa ni tegemeo la wananchi.
.............................................................................................................................................