Ndesamburo afutiwa kesi ya Uchaguzi Moshi Mjini!

Malafyale

JF-Expert Member
Aug 11, 2008
13,813
11,123
[FONT=Arial, sans-serif]Aliyekuwa Mgombea Ubunge Jimbo la Moshi Mjini kupitia chama cha Mapinduzi (CCM), Justin Salakana, amefuta kesi ya kupinga matokeo yaliyompa ushindi Mbunge wa sasa, Philemon Ndesamburo (Chadema) katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Moshi.[/FONT]

[FONT=Arial, sans-serif]Wakili wa Salakana, Elizabeth Minde, alimweleza Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Moshi, Stella Mugasha, kuwa mteja wake ameamua kuacha kuendelea na kesi hiyo na kuiomba mahakama hiyo kuifutilia mbali kesi hiyo namba mbili ya mwaka 2010.[/FONT]

[FONT=Arial, sans-serif]Wakili wa Serikali, Stella Kachenje, hakupinga maombi hayo na kuiomba mahakama hiyo imuamuru Salakana awalipe fidia ya gharama za usumbufu kwa maelezo kuwa wamekuwa wakitumia gharama na muda kufika mahakamani hapo na mlalamikaji kuamua kuiondoa kesi hiyo mahakamani.[/FONT]

[FONT=Arial, sans-serif]Hata hivyo, Jaji Mugasha aliamuru kila upande kubebe gharama zake ulizotumia katika kesi hiyo na kuamua kuifuta kesi hiyo.[/FONT]

[FONT=Arial, sans-serif]Katika madai yake ya msingi, Salakana anadai jywa Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwaka jana haukuwa huru na haki kwa kuwa ulitawaliwa na kasoro kadhaa za kukiukwa kwa sheria za uchaguzi huku vitendo vya rushwa, kashfa na vitisho vikitawala katika zoezi hilo lililompa ushindi Ndesamburo.[/FONT]

[FONT=Arial, sans-serif]Salakana alidai kuwa Ndesamburo alimkashifu kwa kuueleza uma kwamba hana nyumba mjini Moshi na mtu atakayeonyesha nyumba yake atamzawadia Sh. milioni mbili huku viongozi wa Chadema wakiwamo Madiwani wa sasa Jomba Koyi wa Kata ya Njoro na Steven Ngasa Kata ya Kiusa walitoa maneno ya vitisho wakati wa kampeni kwamba Chadema isiposhinda damu itamwagika ama watu kuchinjwa.[/FONT]

[FONT=Arial, sans-serif]Kufutia madai hayo, Salakana aliiomba mahakama hiyo kutamka kufuta matokeo ya uchaguzi huo kwa madai kuwa haukuwa halali na kutaka Ndesamburo azuiwe kugombea tena kiti cha ubunge.[/FONT]

[FONT=Arial, sans-serif]Hivi karibuni, Salakana katika taarifa yake kwa vyombo vya habari mjini, hapa alisema uwezekano wa kuendelea na kesi hiyo ni mdogo kutokana na kukabiliwa na ukata wa fedha za kuendesha kesi hiyo.[/FONT]

“[FONT=Arial, sans-serif]Nilifungua kesi namba mbili ya mwaka 2010, gharama za kuwalipa mawakili na ikizingatia kwamba patahitajika fedha zaidi hapo mbeleni kesi itakapoanza, kwa maana ya gharama za mashahidi na za mawakili hivyo uwezekano wa kuendelea na kesi ni mdogo,”alikaririwa Salakana akisema.[/FONT]

CHANZO: NIPASHE
 
Ccm imeshindwa kumsaidia?
Coz angeshinda si wangeongeza majimbo na ruzuku pia?
Kaaaazi kwelikweli!
 
Amesoma alama za nyakakati akaona haziko upande wake.
 
Amegundua kuwa hawezi kupata mashaidi wa story zake za kutunga! Nawashauri ccm wenzake waige mfano huu! Ni upuuzi mtupu kuendesha kesi za uzushi zisizo na mashiko huku ukiwalipa mawakili na mashahidi! Waache kuwalipa watu kufanya kazi za kutoa ushahidi wa uongo, majungu na uzushi na kuanzia waanze na hawa waliowatuma humu JF..Hongera sana Mh. Philemon Ndesamburo. Sasa ni mbunge halali wa Moshi mjini. Kesi imeisha, sasa ni kuchapa kazi!
 
Katibu Mkuu 'aliyestaafu' aliwahimiza wafungue kesi chama kitasimamia gharama ilikuwa ahadi hewa?! sasa kama wenyewe kwa wenyewe wanapigana changa la macho sembuse wakazi wa bukyanagandi...hiki chama kweli ni magamba..!!
 
Hii kesi haikuwa ya Salakana thidi ya Ndesamburo bali ilikuwa ya Makamba vs Ndesamburo. Mnaofuatilia mambo mtakumbuka kwamba Makamba ndiye aliyewataka Wote walioshindwa wakimbilie mahakamani kufungua kesi na kwamba ati Yeye Makamba na mafisadi wenzake wangetumia fetha walizonazo kuendesha hizo Kesi.
Baada ya Makamba na akina Rostamu kuenguliwa, equation la mahesabu ni hili :

Makamba - Rostam - Ruzuku ndogo = mapato kidogo = Kufunga kesi !
Mwisho wake : CCM Kwishney
 
Ccm imeshindwa kumsaidia?
Coz angeshinda si wangeongeza majimbo na ruzuku pia?
Kaaaazi kwelikweli!

hata wangeshinda kesi, wasingeshinda uchaguzi. Moshi mjini ni ngome ya upinzani. Kati ya madiwani 20 wa kata zote za Moshi mjini,, ccm ina madiwani wa tatu tu!
 
Walianzisha oparesheni maalum ya kumg'oa Ndesamburo. Wakaja Dar wakachanga fedha nyingi, wakaiita ONO (Operesheni Ndesa Out), Wapiganaji hawakukaa kimya, wakajibu na OMO (Operesheni Mramba Out), haya ndo matokeo. Ndesa hashikiki, ni bora ccm wajitahidi kujiimarisha kwa majimbo waliyonayo, kwa sababu yaliyokwisha chukuliwa na wapiganaji kurudi ni ndoto.
 
Sarakana uniniangusha, na unakiaibisha chama chetu! Em ongea vizuri na makamba, fungu lilishatengwa kwa ajili ya kusimamia hizi kesi. Ndo maana alisisitiza kufungua kesi. au kunamtu keshachakachua hilo fungu!!
 
Njia ya mwongo ni fupi alijua mbele ya safari ukweli utakapojitenga na uongo ataaibika sn,mwacheni aendelee kuweweseka .
 
:happy: :bange:Ni vema. mwenye akili anaona mbali. aache watu wafanye kazi za watanzania.
 
namwomba ndesa, kama mwenyekiti wa cdm kilimanjaro ahakikishe kwamba majimbo ya same mashariki, vunjo, moshi vijijini na siha yakuja cdm kwasababu kwa sasa hivi wananchi wa haya majimbo wanaikubali cdm, hasa katika jimbo la vunjo ambalo lilipotea kwasababu john mrema alichelewa kujitambulisha kwa wananchi.na uzembe kama huu usirudiwe tena katika jimbo lolote, ni vyema kila menyekiti wa mkoa akahakikisha anaandaa wagombea ubunge wasiopungua wawili katika kila jimbo na kuhakikisha pia kila kata ina wagombea wa udiwani kuanzia sasa.

naomba kuwakilisha.
 
Buriana Salakana! Alazwe mahala pema katika historia ya siasa za Moshi Mjini na Tanzania kwa ujumla..
 
na bado watafuta nyingi ambazo zote wamefungua tena na upinzani ulivyo watetea mahakimu na majaji kuhusu mswaada wa mahakama mzee tundu lissu alipambana mpaka mwisho wake
 
Amefuta kwa sababu alielewa kuwa hata kwa namna gani hatashinda! Kwani pesa za wizi zimewaishia ccm?
 
Mh Philemon Ndesamburo"NDESA PESA"hongera sana mwenyekiti wangu.Ninakuhaidi zawadi ya Jimbo la Siha 2015 na Halmashauri yake.PEOPLES POWER.
 
Back
Top Bottom