Nderemo, vifijo na sifa nyingi kwa mkuu vimetapakaa kila kona. Je watanzania tumeshashinda?

herzegovina

JF-Expert Member
Oct 28, 2015
3,141
4,721
Wakuu, mtanisamehe kwa KUWA pessimistic kuhusu hili sakata la mchanga wa dhahabu.

Kwa kweli ni hatua nzuri kwa kuanza kuangalia na kulinganisha kinachoripotiwa na kilichopo. Kutumbuliwa kwa kina Muhongo pia sio jambo baya lakini.......mikataba ya madini ipo wazi au imefichwa??? Kwanini isiwe wazi??

Kitu kingine kinachonipa hofu ni confidence kubwa waliyonayo ACACIA. wanaipinga ripoti waziwazi kabisa. Mara nyingi hawa wazungu huwa wapo ten steps ahead, wanaishi maisha ya mbeleni. Sidhani kama walikuwa hawajaji-hedge iwapo suala hili(kama ni kweli) litagundulika.

Mahakama za kimataifa nadhani ndio zitasikiliza hii kesi...(hapo sasa)

Maombi yangu kwa watanzania

1. Badala ya kushangilia tu kuzuiliwa kwa mchanga, tuombe sasa mikataba yote ya madini iwekwe wazi ili hata wale wachache waliopo migodini wakiona mambo hayapo sawa waweze kutoa taarifa kwa siri kwa vyombo husika.

2. Tusishangilie sana, tusubiri tuone kama tutashinda basi tumpe sifa Anayestahili na kama tutashindwa basi tumlaumu kwa kutofuata hatua sahihi na kuachia mianya iliyosababishwa tushindwe. (Tuliwahi kumshangilia alipokamata meli ya samaki)

3. Tusiliache hapa suala hili. Tuendelee kufuatilia mpaka mwisho tujue hatua kwa hatua muendelezo wa kesi hii.....tusipende kuwa watu wa MATUKIO tuwe watu wa MATOKEO

AHSANTENI
 
Ni kawaida ya watanzania. Watu wanatumia hisia na ushabiki zaidi ya logic, ndio maana hata taifa stars ikishinda mechi moja tu utasikia wamealikwa bungeni na ikulu, alafu mwisho wa siku hawafiki popote. Vivyohivyo kwenye maswala ya siasa na kijamii, wafuasi wa CCM na CDM wote ni watu wa ushabiki tu na hisia kibao. Ndio maana unaona baada tu ya raisi kupokea ile ripoti na kutoa yale maamuzi kila mtu anamwaga sifa. Wapumbavu wengine wanaenda mbali zaidi na kukufuru eti magufuri aongoze bila kikomo. Hakuna hata mtu anayeona kua huu ni mgogoro wa kimaslahi kati ya pande mbili kwahiyo inawezekana yeyote kati yao akawa mwongo. Iwe ni serikali na tume yake au hao wawekezaji.
 
Na wasiwasi wangu ni kuwa uwezekano wa kushindwa ni mkubwa zaid ukizingatia share za acacia zimeshuka. Mimi naomba tufuatilie hadi mwsho bila kuyumbishwa ili tujifunze. Tusitoke kwenye reli.
Pamoja na nia nzuri ya Rais lakini jambo hili linahitaji umakini mkubwa sana.
 
Viongozi wa Tanzania wanajua sisi ni wajinga na njia pekee ya sisi kuwakubali wao ni kwa wao kutupa habari zinazotia machungu ili hata ikitokea kitu basi tuwatetee hao viongozi

Hii ripoti kiufupi imepikwa na ndio maana hata hao accacia wao wamesema kama hizo concentrates zilizotajwa na hiyo tume ni kweli basi mgodi wao ungekuwa wa kwanza duniani kutoa fhahabu nyingi...
Pia tukumbuke siku ile makontena yamezuiliwa magufuli alitamka kuwa ripoti itakayotoka itaishangaza dunia, maana yake alikua keshapanga kila kitu na hiyo kamati kazi yake ilikua kuandika kile anachotaka mkuu au wameandika ili wamfurahishe

Accacia wasingejitokeza pinga ripoti waziwazi kama haikua kweli na wao wanasema hiyo ripoti imeandika zaidi ya 10times actual value of the concetrates

Kuna kitu kinatafutwa na Accacia wanasubiria wafukuzwe hapo ndio waifilisi nchi yetu
 
Ni kawaida ya watanzania. Watu wanatumia hisia na ushabiki zaidi ya logic, ndio maana hata taifa stars ikishinda mechi moja tu utasikia wamealikwa bungeni na ikulu, alafu mwisho wa siku hawafiki popote. Vivyohivyo kwenye maswala ya siasa na kijamii, wafuasi wa CCM na CDM wote ni watu wa ushabiki tu na hisia kibao. Ndio maana unaona baada tu ya raisi kupokea ile ripoti na kutoa yale maamuzi kila mtu anamwaga sifa. Wapumbavu wengine wanaenda mbali zaidi na kukufuru eti magufuri aongoze bila kikomo. Hakuna hata mtu anayeona kua huu ni mgogoro wa kimaslahi kati ya pande mbili kwahiyo inawezekana yeyote kati yao akawa mwongo. Iwe ni serikali na tume yake au hao wawekezaji.
Umenena.... watanzania sisi ni watu wa kutema big g kwasababu ya karanga za kuonjeshwa.. mhemko kila kona kutafakari kwa umakini kwetu n mwiko.. yaani tunasikitisha!!!!
 
Tumetoka kwenye vita ya madawa tumehamia ya mchanga ngoja tuone kama na hii ya mchanga itamuacha mtu salama !
 
Naona tumeamua kumpapasa faru makalio ngoja revange yake
Nahisi harufu ya TZ kuwa kama Zimbabwe
 
Viongozi wa Tanzania wanajua sisi ni wajinga na njia pekee ya sisi kuwakubali wao ni kwa wao kutupa habari zinazotia machungu ili hata ikitokea kitu basi tuwatetee hao viongozi

Hii ripoti kiufupi imepikwa na ndio maana hata hao accacia wao wamesema kama hizo concentrates zilizotajwa na hiyo tume ni kweli basi mgodi wao ungekuwa wa kwanza duniani kutoa fhahabu nyingi...
Pia tukumbuke siku ile makontena yamezuiliwa magufuli alitamka kuwa ripoti itakayotoka itaishangaza dunia, maana yake alikua keshapanga kila kitu na hiyo kamati kazi yake ilikua kuandika kile anachotaka mkuu au wameandika ili wamfurahishe

Accacia wasingejitokeza pinga ripoti waziwazi kama haikua kweli na wao wanasema hiyo ripoti imeandika zaidi ya 10times actual value of the concetrates

Kuna kitu kinatafutwa na Accacia wanasubiria wafukuzwe hapo ndio waifilisi nchi yetu
Hata mimi nilisikia ile kauli "ripoti itakayotoka itaishangaza dunia" ...halaf akaongeza "watanzania wangeujua ukweli......."
 
Back
Top Bottom