Mwanaukweli
JF-Expert Member
- May 18, 2007
- 4,786
- 1,710
Mimi nilisafiri kwa ndege ya 540 ambayo ilikuwa iondoke Mwanza tarehe 21/5/2011 siku ya Jumatatu saa 7 mchana. Abiria walianza ku check in tangu saa 5 na nusu na kusubiri. Muda wa kuondoka tukaambiwa ndege ina tatizo dogo la kiufundi ambalo linashughulikiwa na hivyo tutarajie kuondoka saa 9.
Ilipofika saa 9 msemaji wa shirika hilo la ndege alikuja na kutuambia kuwa tutarajie ndege itakuja saa 11, na akatupatia soda moja moja na maandazi mawili mawili. Baada ya hapo ikawa kimya mpaka saa 1 jioni tulipoambiwa kuwa ndege itakuja ila itabidi ipitie Zanzibar.
Ndege ilifika muda huo, na saa mbili na nusu tukaondoka kuelekea Zanzibar njiani tukapewa glas ya juice na korosho kidogo na biskuti kama 4 hivi. Tukatua zanzibar kama saa 3 na dak 40. Baadaye tukarudi kwenye runway kuondoka kwenda Dar, lakini rubani akagundua shida nyingine ndogo ya kiufundi. Akaahidi kuwa itashughulikiwa kwa muda mfupi. Baada ya dakika 40 ya kutengeneza, rubani akatuambia tushuke na kuwa ndege haitawezaa kuendelea na safari.
Hatimaye kwenye saa nane tukapelekwa hotelini na kulala bila kupata chakula. Kesho yake tukakodiwa ndege ya Costal Aviation na kufika Dar saa 5 asubuhi, karibu masaa 24 tangu tu check in.
Inaonekana wana ndege moja tu inayofanya kazi Tanzania, ambayo ni mbovu.
Huduma kwa wateja ni mbaya mnoooooooooooo.
Nauli iko juu zaidi ya Precision na Air Tanzania
Jihadhari kabla hujaamua kusafiri na 540