ng'ombo
JF-Expert Member
- Dec 1, 2014
- 418
- 619
Ndege hiyo itasafirisha abiria kutoka mji wa Blantyre hadi Dar-es-Salaam nchini Tanzania na itatua kwa muda Lilongwe kabla ya kuelekea Dar .
Taarifa kutoka kwa shirika hilo la ndege, lilisema lengo ni kufanikisha ulimwengu ambao "unakumbatia jinsia zote".
Bi Mwenifumbo, 24, alisomea taaluma ya uchukuzi wa ndege mjini Addis Ababa,
Shirika la ndege la Malawi Airlines lilianzishwa Julai 2013 baada ya kuvunjwa kwa shirika la awali la Air Malawi Februari mwaka huo
"Lengo la hatua hii ni kuwahamasisha wasichana ambao wangependa kufanya kazi katika uchukuzi wa ndege lakini kwa njia moja au nyingine hufikiria ni vigumu au kwamba ni kazi ambayo wanawake hawaiwezi," taarifa ya Malawi Airlines ilisema.
Ndege hiyo aina ya Bombardier Q-400 itapaa kutoka Blantyre saa nne asubuhi Alhamisi.