Ndege ya kijeshi ya Urusi yaitishia ile ya Marekani Baltic

Econometrician

JF-Expert Member
Oct 25, 2013
16,059
29,048
_96572886_usrc135.jpg

Ndege ya Marekani ya ujasusi aina ya US RC-135

Ndege ya Urusi ilipaa futi tano juu ya ndege ya ujasusi ya Marekani katika anga ya bahari ya Baltic siku ya Jumatatu, kulingana na maafisa wa Marekani.

Hatua hiyo ilionekana kuwa isio salama kutokana na kasi ya ndege hizo mbali na udhibiti mbaya wa ndege hiyo, maafisa hao walisema.

Lakini Urusi imepinga malalamishi hayo ya Marekani ikisema kuwa ndege hiyo ya Marekani iliichokoza ndege yake.
Siku ya Jumatatu Urusi iliionya Marekani kwamba ndege za Marekani zinazopaa juu ya anga ya Syria zitalengwa.tangazo hilo lilijiri ili kujibu kuangushwa kwa ndege ya Syria baada ya kulenga waasi wanaoungwa mkono na Marekani.

Siku ya Jumanne, Jeshi la Marekani liliiangusha ndege isiokuwa na rubani inayomilikiwa na Iran nchini Syria na hivyobasi kuongeza wasiwasi kati ya Washington na Moscow ambayo ni mshirika mkuu wa utawala wa Syria.
_96572889_russiasu27.jpg

Ndege ya Ursui aina ya Su-27 ilipaa futi tano juu ya ndege ya Marekani

Uchokozi huo wa siku ya Jumatatu ulifanyika kilomita 40 kutoka eneo la Urusi la Kalinigrad katika maji ya kimataifa.

Msemaji wa Pentagon Nahodha Jeff David aliambia maripota kwamba:Tulikuwa tukipaa katika maji ya kimataifa na hatukufanya uchokozi wowote.Ndege ya kijeshi ya Urusi yaitishia ile ya Marekani Baltic - BBC Swahili

Chanzo,vyanzo vyote vya habari kasoro TBC
 
  • Thanks
Reactions: MC7
Naona michezo hii ya kulahumiana mwishowe watakuja kufanya miscalculation wakajikuta wanaingia vitani bila kutegemea, hapa wanazungumzia ndege ya kijasusi ya USAF kuwa escorted na ndege ya kijeshi ya Urusi, cha ajabu mara zote Amerika ulalamika kwamba marubani wa Urusi wanakosa kuwa wangarifu, sijui USA wanakuwaga na maana gani? Wao wanalalamikia Urusi as if marubani wa Urusi na America wanasoma chuo kimoja cha Urubani!!!

Leo hii kwa mfano ndege ya jeshi la Marekani ilikaribia kwa karibu sana ndege iliyokuwa imembeba Waziri wa ulinzi wa Urusi akitokea kwenye ziara ya kikazi, sina shaka America ilijua ndege ya Urusi ilikuwa imebeba Waziri wa ulizi kulikuwa na ulazima gani wa kuikaribia, je kama an armed Sukhoi-27 hisingekuwa karibu kungetokea nini? Binafsi naona as if NATO inatafuta sababu ya kuanzisha vita na Urusi 4 some reasons that beats me! Hivi NATO inafikiri inaweza kushinda vita hii kweli?
 
Acha , KGB Putin afanye vyake.
Hapo, mziki ufunguliwe awachezeshe style ya kiduku na Komandoo Mr Kim Un na Iran wamsaidie Putin mbona NATO forces na USA wataomba pooooo asubuhi mapema sana!!

I wish, I could be KGB Putin and Commander Kim Un or working with them , I would have eliminated the USA.
 
Acha , KGB Putin afanye vyake.
Hapo, mziki ufunguliwe awachezeshe style ya kiduku na Komandoo Mr Kim Un na Iran wamsaidie Putin mbona NATO forces na USA wataomba pooooo asubuhi mapema sana!!

I wish, I could be KGB Putin and Commander Kim Un or working with them , I would have eliminated the USA.
Mkuu ni Balimi peke yake au umechanganya Don Nyati?
 
Duh! Futi 5 juu ya mwenzie si mwonekano kama amemlalia mgongoni! Akutukanaye hakuchagulii tusi nimeamini.
 
uzuri Urusi hana analoweza fanaya yeye anawasindikiza tu wenzake
Mkuu unaelewa maana ya tukio hilo la ku-escort ndege ya kijasusi ya adui yako?
1. Maana yake tunaziona ndege zako(Teknologia yako ya kuifanya ndege ya kijasusi isionekane haifanyi kazi dhidi ya radar zetu).
2. Tukitaka kuzilipua ndege hizo tunaweza sekunde hiyo hiyo.
3. Usijaribu tena kuleta vindege vyako karibu yetu.
4. Kule Syria tunaweza kuzilipua ndege zako tukipenda(sio kwamba zinaposhambulia ndege za Syria hatuzioni).
Hayo makelele ya marekani na NATO ni kutafuta huruma na kinga wasitunguliwe au kutafuta kuhalalisha kuishambulia urusi kitu ambacho kitakuwa na madhara kwa dunia kuliko WW2.
 
Marekani na nato wana jiona amekuwa!wakimchokoza mrusi atapigwa na makombora aina ya shetan,hao bado hawana uwezo Wa kupambana na mrusi
 
Acha , KGB Putin afanye vyake.
Hapo, mziki ufunguliwe awachezeshe style ya kiduku na Komandoo Mr Kim Un na Iran wamsaidie Putin mbona NATO forces na USA wataomba pooooo asubuhi mapema sana!!

I wish, I could be KGB Putin and Commander Kim Un or working with them , I would have eliminated the USA.

Mkuu licha ya General Putin kuwa na mahesabu makali kimedani, IRAN vile vile si mchezo nakumbuka Amerika walivamia Iraq na kuikalia kwa muda Wairan waliwapatia silaha waasi za kulipua magari ya deraya na vifaru vya USA - silaha hizo ziliwatia hasara USA mpaka wakafikia hatua ya kuyarudisha USA magari kufanyiwa marekebisho makubwa kwenye bodi, ilikuwa balaa mpaka Serikali ya Amerika ililamikia Iran kwamba isitishe kuwapatia waasi silaha kali - baadae Wamerika walisema wanasanyansi wa Wairan si mchezo, wangapi wanalijua hilo?

Juzi hapa baada ya magaidi kumshabulia Bunge la Iran na makao makuu ya Ayatolla - Iran ilivurumisha makombora kwenda Syria, makombora yenyewe yana range ya maili 750 yakatua kwenye ngome ya waasi(ISIS) with a pinpoint accuracy - Waasi zaidi ya 50 wakauwawa on the spot na wengine kujeruhiwa, walivurumisha makombora kulipiza kisasi dhidi ya magaidi lakini binafsi nadhani operation hiyo ilitekelezwa kuwapa msg Saud Arabia kwamba wakirudia kuwapatia msaada magaidi kuvamia IRAN basi Saudia ibaki ikijua kwamba wapo within range ya makombora ya IRAN.

Mkuu unacho sema upo sahihi kabisa Uncle SAM akiendelea na adventures zake akafanya makosa ya kufanya mashambulizi kwenye moja ya Mataifa yenye uwezo kijeshi i.e Uchina, Iran, Urusi na Korea Kasikazini basi watalazimika kumchangia na kumchakaza vilivyo, kwa nini nasema hivyo: Mataifa hayo yanajua kwamba Marekani ikishambulia moja ya mataifa tajwa hapo juu hawewezi kujua kesho atamshambulia nani kwa kuwa USA ni highly unpredictable mwenye erratic behaviour - sasa kumaliza donda ndugu ni afadhali waka deal naye once and for all - maoni yangu, I might be wrong lakini nadhani niko sahihi.
 
Back
Top Bottom