Ndege wafananao huruka kundi moja

Ndege wafananao huruka kundi moja

Mzee Chapuuka

Member
Joined
Apr 21, 2017
Posts
97
Reaction score
243
Huwa najiuliza inakuaje mkuu JPM tangu aingie madarakani rafiki zake ni maraisi wenye skendo mbovu katika nchi zao,karibu viongozi wote wakuu wa nchi waliotembelea bongo wanaskendo mbovu katika nchi zao
1.Kagame ana skendo ya kuminya demokrasia na Uhuru Kwa wapinzani nchini kwake

2.Mfalme wa Morocco ana skendo ya kuitwala Sahara magharibi kimabavu hadi AU ikamtenga

3.Museveni nae anaminya demokrasia,kuwabana wapinzani hasa bwana Besigye na kung'ang'ania madaraka.

4.Kabila kazingua kapindua Katiba ya nchi yake na kung'ang'ania madaraka

5.Zuma ndo kachokwa na Wasouth Kwa ufisadi uliotukuka hadi COSATA wamempiga marufuku kuhutubia katika mikutano yao

6.Huyu wa Uturuki na skendo ya kutaka kupinduliwa kuonesha kwamba ana kasoro wamemchoka

7.Ethiopia nako wanali Uhuru wa demokrasia

Hawa viongozi wote washatembelea Kwa mwenzao hapa bongo ,sasa najiuliza ndo mambo ya ndege wafananao huruka kundi moja
Mwisho wa Siku ataiga tabia za hawa rafiki zake !?NAJIULIZA TU NA KUWAZA TU
 
Viumbe wazito!
Binadamu hawana jema!
 
Back
Top Bottom