Ndege wa rangi moja

May 26, 2008
34
6
Wapendwa wanajamii, napenda kuibua hoja kama changamoto kwa jamii yetu kuhusu kauli zetu mbalimbali zinavyoweza kujenga ama kubomoa kwa namna moja ama nyingine.

Wakati wa mchakato wa kusaka wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi wa mwaka huu, kiongozi wa chama kimoja kikongwe ambaye ndiye mtendaji mkuu wa chama hicho alipata kunena haya, "Katika mchakato wa kutafuta wagombea kwa tiketi ya chama changu, wagombea wote walitoa rushwa, ila walizidiana dau tu!".

Nina maswali matatu ya kuuliza kama changamoto kwa wanajamii.

1. Kauli hii inamaanisha kwamba wagombea wote kwa nafasi zote wa chama hicho hawafai kugombea (pamoja na waliopasishwa na tume ya taifa ya uchaguzi kwa kupita bila kupingwa) ?

2. Msajili wa vyama vya siasa anasubiri ushahidi ili apate kuwawekea pingamizi, kama sheria mpya ya gharama za uchaguzi inavyomtaka?

3. Licha ya ukweli kwamba mtendaji mkuu wa chama hicho kukosa imani na wagombea wake, je, wapiga kura bado mna imani na wagombea watoa rushwa?
 
Back
Top Bottom