Ndalichako, nini kinaendelea vyuo vya Korogwe na Kasulu?

Lordita

Member
May 11, 2017
16
16
Ndalichako waziri wa elimu tegua kitendawili cha wanafunzi wa vyuo vya Korogwe na Kasulu walioshindwa kwenda field tangu wamalize mitihani yao ya semester ni mwezi na zaidi sasa. Hawa ni wanafunzi waliotolewa UDOM na kwenda vyuo hivyo ili kuendelea na masomo ya diploma maalum ya ualimu wa masomo ya hisabati na sayansi.

Ni mda mrefu wanafunzi hawa walipaswa kuwa field japo mpaka Leo hawajaenda na hamna maelezo yoyote toka chuoni wala wizarani kueleza sababu ya pesa za field kutotolewa ili waende field. Pia kuna wasiwasi kama kweli wanafunzi hawa wataajiriwa kama walimu wa sekondari baada ya masomo yao au wataachwa wanarangaranga kwa kisingizio cha wao ni vilaza. Ndalichako wewe kama waziri wa elimu tumia nafasi yako vizuri ili kuwasaidia wanafunzi hawa.
 
Nina wasiwasi na ndalichaku sijui kama anaweza ifikia hata lengand ya Mulu.go.
Maana huyu daktari jamani mi sioni hasa nini alichofanya pale wizarani zaidi ya kukagua vyeti biasly!!!
 
Vyuo vya ualimu vyote vimesahauliwa sana hasa baada ya awamu hii ya tano kuingia. Mathalani hakuna mwanachuo aliyeenda field mpaka sasa tangu vyuo kuanza kutumia mfumo wa Nacte na wengine tayari wameshamaliza bila kwenda field. Sijui serikali inaandaa walimu wa aina gani sasa. Kwanza mfumo unabadilishwa kila mwaka Mara diploma ya kawaida Mara mfumo wa nacte yaani full mkanganyiko na wakufunzi hawapewi mafunzo yoyote kuhusu mabadiriko haya.
Hawa wanachuo wa vyuo vya Korogwe na Kasulu walitakiwa waanze field mwezi wa tatu na usidhani kama wataenda na bado semester mbili tu wamalize chuo. Wakati huo huo vyuo vya Tukuyu, Morogoro, Songea, Mpwapwa na Butimba navyo sio muda wanachuo wanatakiwa waende field na Ndalichako ni waziri wa matamko tu huku stela manyanya (anajiita injinia japo Si kweli) yeye ndo ni kivuli tu. Mlugo pamoja na matamshi yake yenye utata yupo mbali sana kiuweledi kulinganisha na akina mama hawa.
Ndalichako na serikali yako mmeajiliwa hapo wizarani kutoa matamko tu? Ebu simamieni elimu ipasavyo.
 
Back
Top Bottom